Saturday, January 10, 2009

CHEMSHA BONGO. No Woman No Cry

Kama kuna nyimbo ambazo takriban kila ajuaye Reggae anaujua ni huu wa No Woman No Cry ulioandikwa na kuimbwa na Bob Marley na kundi lake la Wailers. Lakini ukisoma lyrics zake unaweza kuwa na utata wa nini alichokuwa akizungumzia hapa alipoimba hili. Pia ni moja kati ya nyimbo amazo video zake zamuonesha akiwa na hisia kali kila aimbapo. Unaweza kuhisi alikuwa akimaanisha nini aliposema NO WOMAN NO CRY?
Hii ni video yake na chini ni audio yake
(sababu ninajua si kila sehemu unaweza kusikiliza ama kuangalia You Tube) kisha Lyrics zake na ukiweza jiulize na ama nieleze unadhani alimaanisha nini aliposema No Woman No Cry





No woman no cry, no woman no cry
No woman no cry, no woman no cry

Say, say, said I remember when we used to sit
In a government yard in Trenchtown
Obba, obba, serving the hypocrites
As the would mingle with the good people we meet
Good friends we have, oh, good friends we've lost
Along the way
In this great future,
You can't forget your past
So dry your tears, I say

No woman no cry, no woman no cry
Little darling, don't shed no tears, no woman no cry

Say, say,
Said I remember when we used to sit
In the government yard in Trenchtown
And then Georgie would make the fire light
As it was, love would burn on through the night
Then we would cook cornmeal porridge
Of which I'll share with you
My fear is my only courage
So I've got to push on thru
Oh, while I'm gone

Everything 's gonna be alright, everything 's gonna be alright
Everything 's gonna be alright, everything 's gonna be alright
Everything 's gonna be alright, everything 's gonna be alright
Everything 's gonna be alright, everything 's gonna be alright
So woman no cry, no, no woman no cry
Oh, my little sister
Don't shed no tears
No woman no cry
I remember when we use to sit
In the government yard in Trenchtown
And then Georgie would make the fire lights
As it was, log would burnin' through the nights
Then we would cook cornmeal porridge
Of which I'll share with you
My fear is my only courage (pengine imeandikwa my feet is my only carriage)
So I've got to push on thru
Oh, while I'm gone
No woman no cry, no, no woman no cry
Oh, my little darlin'
Don't shed no tears
No woman no cry, No woman no cry

Oh my Little darlin', don't shed no tears
No woman no cry
Little sister, don't shed no tears
No woman no cry

10 comments:

Unknown said...

Mimi naona nikupe mji maana, mwenzangu wewe ni mtaalamu wa haya mambo.

Nimepita kukutemeblea kaka, je uhali gani?

Anonymous said...

Nadhani nilishawakwambia Mzee wa Changamoto kuwa Upeo wangu mdogo mbaya zaidi hata kiinglish changu pia ni ile mbovumbovu,ok tuachane na hayo kusema kweli song hili watu wanalipenda sana kama vile haitoshi wanalitafsiri vibaya kwa kusema No Woman No Cry wakimaanisha pasingekuwa na wanawake pasingekuwa na vilio huku wakitoa mifano mambo mengi yanayofanyika sababu ni mwanamke,Jambazi anaua ili akastarehe na mwanamke,vigogo wanakula rushwa ili wakaonge wa wanamke,pia HAWA ndiye aliyempotza ADAM hiyo ni mifano tu ya watu katika kudhibitisha maana ya song hili, LAKINI kwa upande wangu nikilipitia hili songi Naona BOB alikuwa anaelezea hali halisi ndani ya Jamaica kipindi cha ukoloni ya kwamba mambo yakuliwa si shwali WAZUNGU walikuwa wakishakula wanatuba mabaki kwenye mto unaoelekea TRENCHTOWN ambapo palikuwa na makazi ya kina BOB,pia kina BOB walikuwa wanashindwa kupiga hata ugali kwa kuhofia unga utaisha wakaona bora wapike Uji ambao watashea na siku zitasonga,Kikubwa alikuwa anawaamasisha Wasikate tamaa ,wasikubali kushindwa ipo siku mambo yakuwa poa Everything gonna be alright.
ebwanaee nimejitutumua vya kutosha acha niishie hapo,nisubiri mawazo yako na wadau wengine.

Mzee wa Changamoto said...

Asanteni sana Shabani na Salu. Nami nasubiri wadau wengine nao wajuvye yao kisha nami nieleze huko. Lakini pengine nitoe ka-tip kengine kuwa kwa kiingereza cha Jamaica na Carribean kwa ujumla, NO yaweza kumaanisha NO na pia ikamaanisha DON'T. Kwa hiyo upo uwezekano wa kuimba NO WOMAN, DONT CRY.
Ntarejea kujifunza toka kwa wadau wengine

Anonymous said...

habri mzee mziam
mi kwa mtazamo wangu au kwa jinsi nilivyoelewa wimbo huu,alikuwa anawaimbia wanawake wa jamii ya rasta ambao walikuwa wanaonekana kubaguliwa sana kutokana na wanjamii hao kutafsiri vibaya maagizo ya agano la kale ambapo kuna misingi mingi ambayo wanajamii wa rasta wanafuata kama mwanamke kutoruhusiwa kumuhudumia mumewe wakati akiwa hedhini na kadhalika.kwa hiyo kwa wimbo huu Bob alikuwa anataka kuwahakikishia wanawake wa jamii ya kirasta kuwa wanawajali na watashare kila kitu pamoja,atamsaidia kuwasha moto na kupika na pia kuishi pamoja kwa amani na kusaidiana....
nimejaribu kutokueleza mstari kwa mstari wa rylics lakini kueleza kwa sumup jinsi ninavyoelewa.
peace
Mdau
Man Lion

Mzee wa Changamoto said...

Thx alot Man Lion. Nashukuru kwa mtazamo wako. Kama lisemavyo jina la blog kuwa namna uonavyo tatizo ndlo tatizo ikimaanisha kuwa utatatua tatizo kulingana na ulionavyo, ndivyo hata vitu kama tafsiri ya nyimbo tata kama hizi ilivyo. Pengine tip nyingine ni kuwa yasemekana wimbo huu licha ya kuutunga yeye Bob, aliu-credit kwa Vincent Ford ambaye yasmekana akiwa mgonjwa saana taabani alimuona mkewe akilia kutokana na hali yake, naye akanyanyua uso na kumwambia "no woman, no cry". Utakumbuka ile tip ya kwanza kuwa kwa lugha ama matamshi yao NO yaweza kuwa don't na hapo ndipo inapoanza ku-make sense kuwa "No woman, don't cry" pengine akimfariji mkewe kuwa "everything is gonna be alright".
Ngoja niwasubiri wengine nao waseme

Anonymous said...

ha ha ha, daah!NO woman DONT CRY kwa mimi binafsi Hii kwangu imekaa kushoto.UFAHAMU WANGU hapo BOB anapigana anataka kufanya Mapinduzi,U know during colonization many people suffer a lot BOB anasema u can't forget past, anaendelea kwa kusema Wamepoteza marafiki wao wema,Good friend we have Good friend we Lost a long the way. Kuwa kuna marafiki wamewapoteza katika mapambano zidi ya wakoloni au mabebari,So dry ur tears kwahiyo hakuna haja ya kulia au futa machozi,pambana ipo siku kila kitu kitakuwa poa

Mzee wa Changamoto said...

Kwa kumaliza ni kuwa wimbo huu bado una utata juu ya kilichoimbwa. Lakini japo utunzi wake Bob ulitokana na maneno V. Ford kwa mkewe wakati akiumwa saana kitandani, pia kuna tukio kama hilo linalosemekana kumkumba yeye ambapo alimwambia Rita (mkewe) neno hilohilo. Lakini pia wapo wasemao alikuwa akiwaeleza wanawake wote kuwa maisha yao yataboreka siku moja hivyo hakuna haja ya "shed no tears" maana "everything is gonna be alright".
Vyovyote iwavyo, wanawake wana nafasi ya kujimboa zaidi iwe ni mmoja mmoja ama kwa ujumla hivyo hakuna haja ya Kulia kwani kila kitu kitakuwa OK

Subi Nukta said...

Mzee,
'everything's gonna be alright' lini?
Au ndo Edo alishakuzoeza 'tutafika tu?'
Miaka 47 hatujajua tunakoelekea seuze 'everything's gonna be alright' na 'tufike kabisa?'. Madereva wetu wanasogoa na abiria badala ya kusoma ramani waelekeze usukani sawa tujue tunakoenda. Kila leo ni kugongana tu huko mabarabarani na kuanza kunyoosheana vidole pasina sababu.
Kazi ndo kwaanza imechiupa. Eh, tunalo WaTanzania!

Anonymous said...

TAFUTA JIBU LA UHAKIKA MKUU

HAPA WE MWENYEWE UMEBAHATISHA HUNA HAKIKA

Mzee wa Changamoto said...

Karibu sana Ras. Nimefurahi kuwa nawe na kwa hakika nakubali ulichosema kuwa "nimebahatisha" na nina sababu kuu mbili za kufanya hivyo. Kwanza ni kwa kuwa mpaka anakufa Bob hakufafanua hasa alichokuwa anaimba katika wimbo huu, hivyo hakuna na narudia tena kuwa HAKUNA anayeweza kuhakiki alichosema Bob zaidi ya kufanya nilichofanya kuhusianisha na yale aliyowahi kusema. Kwa hilo nakubali. Lakini pia naamini kuna ambalo umeshindwa kulitenda nalo ni kutotoa maana ama mtazamo ama fikra zako juu ya hili. Na si lazima uwe katika kile tuaminicho, maana hapa ni namna unavyoona hilo.
Blessings mankind