Niliwahi kuandika kuwa nia ama malengo ya Reggae si kuburudisha pekee, bali kuelimisha na kuzikomboa akili toka katika UTUMWA WA KIAKILI. Na hilo ndilo kubwa ambalo wanamuziki wa Reggae wamekuwa wakilifanya. Ni hilo linalowafanya waimbe UKWELI NA UKWELI MTUPU ambao huwafanya waendelee kutumikia jamii zao katika harakati zao. Ni JAMII ZA WANYONGE, WANAOONEWA, AMBAO HAWANA WA KUWALINDA NA KUWATETEA na ambao WANAUAWA PASIPO HATIA.
Lakini pia si kuwatetea hao tu, bali kuwarekebisha viongozi ambao wameamua kupuuzia mengi ya maana na kuwasahau wengi wenye uhitaji na ambao wamewaweka hapo (kutokana na sera zao za kuwasaidia) na sasa wanawasahau na kujilimbikizia yale watakayo.
Tumeona yanayoendelea nyumbani na mauaji ya ALBINO na ambavyo wanasiasa wameendelea kutumia ubaya huo kujitafutia umaarufu badala ya kutatua tatizo. Wanabishana ndani ya bunge wakiwa na ulinzi uliosheheni wakati Albino hawezi hata kumsikiliza maana hawezikutoka ndani ya nyumba kununua betri maana anahisi atauawa.
Ndio maana leo namleta kwenu NASIO (kwa mara mengine) katika wimbo huu wa NO LOVE. Namnukuu hapa anapowazungumzia viongozi akisema "them talking about Love, yet they got no love at all, they talk about peace, yet all i see is war". Na kama haitoshi, anaendelea kusema "wicked man ain't got no love for humanity, yet they got so much love for their vanity, their need for way is rising high, while the sufferers are left to die". Nani anayeweza kupinga ukweli wa nini kinaendelea hapa? Nani anaweza kusema viongozi wetu wamefanya kila wawezacho na kuwajibisha kila astahiliye kukomesha haya? Kinachosikitisha zaidi ni kwamba aliimba juu ya UNAFIKI wa baadhi ya viongozi wa ki-dini ambapo anasema " while heads of churches, standing in their false pretences" Tumesoma na kushangazwa na habari za Mchungaji aliyekutwa na viongo vya Albino (SOMA HAPA)
Sina shaka kuwa kama kuna kitu ambacho ni cha kufanya sasa ni KUWAWAJIBISHA WENYE DHAMANA ya kulinda usalama wa ndugu zetu hawa maana wamesema mengi, wamepanga mengi lakini hakuna litendekalo. Wanazungumza Upendo wakati twaona mauaji.
Sikiliza NO LOVE ya Nasio kutoka albamu yake ya LIVING IN THE POSITIVE
">**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment