Thursday, March 19, 2009

Kufikiria upya kwa kila nafasi uliyonayo

Nakumbuka wiki kadhaa zilizopita nilikuwa naangalia kipindi cha Larry King Live na waalikwa walikuwa baadhi ya abiria ambao walibahatika kutoka salama pale ndege yao ilipolazimika kutua katika mto Hudson huko New York.
Mmoja kati ya walioalikwa na ambaye bado anasafiri takribani kila wiki akipita hapo alieleza mengi juu ya namna walivyoogopa na jinsi ilivyokuwa ngumu kuamini kuwa kuna kupona, lakini baada ya kutoka salama na kumaliza taratibu zote za kimatibabu, amerejea kwenye shughuli zake za kila siku ambazo zinamlazimu kusafiri kila wiki.
Swali likaja kuwa "unajisikiaje kila unapopita juu ya mto ule ambao maisha yako yalikuwa nusu ndani nusu nje?" na alichojibu ndicho hasa kilichonipa msukumo wa kuangalia upya na kutaka kushauriana na wanajamvi hili juu ya namna ya kuangalia MIANGUKO YETU ya maisha.
Alisema ANAJITAHIDI KUTOFIKIRIA NAMNA ALIVYOOKOKA NA HATA ALIVYOKARIBIA KUFA NA SASA ANAELEKEZA NGUVU ZAKE KWENYE KUJIPANGA UPYA NA KUANGALIA NAMNA YA KUTUMIA VEMA NAFASI HII NYA PILI NILIYOPATIWA.
Ni fikra ambayo kila mmoja anapaswa kuitambua na kuitumia. Badala ya kulala na kusema hutasafiri tena ilhali unajua kuwa ndicho kinachomfanya asonge. Angeweza kuamua kukaa na kuogopa kusafiri na kisha kudumaza maisha yake, lakini akawa na mtazamo chanya wa maisha na kutambua kuwa kuna uwezekano wa kubadilika na kutumia vema nafasi ya pili aliyopata.
La muhimu ni kutambua kuwa kila siku ni siku mpya na kila sekunde ni sekunde yenye nafasi ya ziada maishani mwako, kwa hiyo kwa kutambua hilo utaishi maisha mema na ya liyo chanya.
AMANI KWENU
Sasa tukitaka kuzungumzia nafasi za ziada, tumwangalie huyu Kaka hapa chini kisha ujiulize kuwa ungekuwa wewe ungeyabadili vipi maisha yako (kama unaona kuna ulazima wa kulazimika kubadilika) ili kutumia vema nafasi unayopata?
Ni ajali kama hizi ambazo wengi wetu huzitilia maanani na kusahau kuwa hata tunapomaliza siku yetu bila makwazo kunakuwa na mengi tuliyojaaliwa kuepuka. Angalia jinsi huyu fundi alivyojiona "akizaliwa kwa mara ya pili" kisha jiulize kama si nafasi ya ziada aliyopewa na Mungu wake, angewezaje kupona?

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kusafiri kwataka moyo ukianza kufikiri jinsi ajali zinavyotokea basi huwezi kusafiri. Ni kukaza moyo na kumwomba Mwenyezi Mungu basi.

Ivo Serenthà said...

I hope too that our planet becomes more human as the image of keeping monkeys.

but man is a nasty beast widely, unfortunately

Good night, I go to sleep

Marlow


P.S.

really incredible that the worker has been saved on that terrible accident