Wednesday, March 11, 2009

Ningekuwa wao

Mwendo huu ulistahili kuelekea kutafuta suluhisho la matatizo ya wananchi
Miaka inakimbia saana. Ni kama juzi juzi tu ambapo tulishuhudia Mhe Rais wetu akitwa madaraka ya nchi kwa kishindo na kuahidi mabadiliko mapya kwa kasi na ari mpya. WELL! Wala sitaki kujua kinachoendelea katika ARI, KASI NA NGUVU MPYA maana kama inakutana na maandalizi mabovu haina inachoweza kufanya. KWA KIFUPI NILIDHANI MPANGO MZIMA NI KAMA NDOTO YA KUSUUZA MAJI MACHAFU AMBAYO NI MENGI KULIKO YA KUSUUZIA NA MATOKEO YAKE NI KUWA YOTE HUCHAFUKA.
Lakini hilo si tatizo maana hakuna aliyetegemea kuona miujiza toka kwa Rais Kikwete. Nchi imevurugika vibaya na hiyo si awamu moja wala mbili kusafisha hayo. Ila kinachouma ni kwamba mpaka sasa tukiwa mwaka mmoja na ushehe toka uchaguzi ujao, hakuna jitihada za wazi zinazooneshwa na viongozi wengine kutaka kujiweka katika nafasi nzuri ya kuielewa nchi na mahitaji yake.
Tumekuwa na tatizo la viongozi wetu kukurupuka muda mfupi kabla ya uchaguzi na kuelekea kwenye kampeni wakitegemea watatumia muda huohuo kujua matatizo ya wananchi. Na wakati huohuo wanakuwa na "ilani" za kuiendeleza nchi kwa kutatua matatizo wasiyoyajua.
Hizo ni ndoto ambazo hata mtoto anajua kuwa haziwezi kutimia. Na la kusikitisha ni kuwa licha ya kutokuwa na maandalizi yoyote kuhusu watakalo kufanya, bado wakishindwa tena kwa asilimia kuuubwa wanalalamika.
Pengine niwape CHANGAMOTO YETU wananchi wa kawaida hapa. Kuwa kama NINGEKUWA WAO ningeanza maandalizi sasa.
1: NINGEANZA KUTEMBEA MIKOA YOTE NINAYOTEGEMEA KUKAMPENI ILI KUJUA MATATIZO YAO SASA.
2: KUCHANGANUA MAHITAJI YA WANANCHI NA KUPANGA KULINGANA NA KIPAUMBELE NA KUJUA NINI CHA KUFANYA NDANI YA MUDA GANI WA UONGOZI WANGU
3: KUSOMA UONGOZI WA VIONGOZI WENGINE KUJUA NANI ANAWEZA KUSAIDIA KATIKA NAFASI GANI NINAYOWEZA KUMTEUA KAMA NITACHAGULIWA.
4 : KUSOMA MATATIZO YA SEHEMU MBALIMBALI NA KUHAKIKISHA INAPANGWA MIPANGO TEGEMEZI YA KUITATUA KWA KUTUMIA RASILIMALI ZILIZOKO HUKO KABLA YA KUGEUKIA MISAADA.
5: KUBWA ZAIDI KUJIULIZA TUJIULIZAYO SISI NA WALIMWENGU WENGI ULIMWENGUNI BAADHI YAO IKIWA NI:
(i)Kwanini watu wanaendelea kuumia huko vijijini licha ya kuwa na rasilimali zote?
(ii)Kwanini watu wanakosa upendo na imani kwa serikali?

(iii)Kwanini walio madarakani hawajui uhalisia wa matatizo yawakumbao wanakijiji ilhali wao ndio wawakilishi wao?
(iv) Kwanini licha ya sheria nyingi bado silaha zimetapakaa mitaani na zaendeleza mauaji na uporaji na kuteteresha usalama?

(v) Kwanini UKIMWI waendelea kusambaa na kuteketeza nguvukazi ya taifa licha ya mamilioni kumwagwa kusaidia kuutokomeza?

(vi) Kwanini thamani ya shilingi yazidi kushuka ilhali gharama za maisha zazidi kupanda bei lakini kwa wenye kipato cha chini?

(vii) Kwanini mauaji yanatendeka kwa wingi kama vile hakuna sheria?
Kwanini watoto wa vijijini hapati elimu sawa na wale wa mijini?
(viii) Kwanini watu waendelee kubabimbikiziwa kesi wakati hawana hatia?

(ix) Kwanini tofauti ya maisha ya wenyenacho na wasionacho inazidi kuongezeka?
(x) Kwanini mauaji ya ndugu zetu albino yanazidi kuongezeka?
(xi) Ni nini kilichopo kati ya serikali kuu na wananchi ambacho kinazuia malengo na habari baina ya "vituo" hivi viwili vikubwa?
Kisha ni kupanga mikakati iliyo sahihi kujua namna ya kukabiliana na matatizo hayo na kwa kuwa na sera na ilani zinazoweza kuonesha njia halisi ya kutatua matatizo mengi ya wananchi walio wengi na ambao ndio wanataabika, sio tu kutaweza kuwapa nafasi ya kuingia IKULU, bali hata atakayeingia atajua kuwa kuna wenye mipango madhubuti ya kutatua matatizo ya watanzania na kama atazembea basi wananchi watakumbuka kuwa SULUHISHO LINALOSUBIRI NAFASI YA KUTATUA MATATIZO YAO.

Nawaacha nao Morgan Heritage ambao katika wimbo wao huu TELL ME HOW COME wameuliza maswali mengi kama haya kuhusu hali ilivyo nchini kwao na wakaja na waonavyo wao katika kiitikio wanaposema
It's cause life is so unfair (in this sweet paradise),
This is what we swear (out of many one people),
Can't you seem to see that anywhere (everyone treated equal)
And this is why,so many die,leavin' so many to cry."Tukutane Next Ijayo"
Uchaguzi Tanzania ni "label" inayozungumzia namna niionavyo nchi yangu ya Tanzania ijiandaavyo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Kwa maandishi mengine juu ya mada hii katika "label" hii BOFYA HAPA

4 comments:

Koero Mkundi said...

Kaka Mubelwa

Yanahitajika mapinduzi makubwa ya kifikra.
Mungu ibariki Tanzania

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mubelwa, hivi unahitaji kuwa wao ili ukomboe nchi hii? na je mpaka sasa umekata tamaa kwamba hutokaa huwe wao?

hata wao walipo kuwa hawajawa waoa, walisema hivyo kumbuka.

wanasema inaanza na wewe. ni rahisi sana kuwalaumu kwa sababu umewapata wa kulaumu lakini ikijakwako ninoma. jiangalie hapo ulipo yawezekana na wewe kuna wakulaumuo na wanatamani kuwa wewe (wao)

hata hvyo nchi yetu siyo yetu!!

Mzee wa Changamoto said...

Ni kweli Kamala. Kuna wanilaumuo na pengine kutaka kuwa mimi.
Lakini hapa lengo si kutamani nafasi walizonazo wala kusema kuwa sina la kuisaidia nchi bila kuwa kama wao, ninalosema ni kuwa kwa vile najua WATATAMANI kugombea kama ambavyo wameshafanya hivyo, basi wakumbuke kuanza maandalizi. Majua makdhaa yaliyopita hawa Republican wanaojiita conservatives walifanya mkutano ama kngamano ambalo ni kama lilianza ku-set stage ya nani anaanza kuonesha mikakati na mipango madhubuti ya kugombea 2012. Yaaani mipango ya uchaguzi ujao inapangwa mwezi mmoja baada ya rais wa sasa kuapishwa wakati kwetu mwaka mmoja kabla ya uchaguzi hata mwenye nia hajajulikana. Kwa hiyo hapa sitamani kuwa politician, lakini nawaeleza kuwa kama ningekuwa natamani kuwa katika nia wanayotarajia kuwa nayo ya kugombea ningeanza harakati mapema.
Nashukuru saaana kwa CHANGAMOTO YAKO Kamala maana naamini wapo ambao wanaweza kutonielewa katika maandishi hayo na umenisaidia kuweka mambo sawia.
Blessings

Yasinta Ngonyani said...

Nami nasema Mungu ibariki Tanzania