Sunday, March 8, 2009

SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE DUNIANI.

Tribute to the Women of the World
This is a humble sampling in tribute to some of the great women throughout history ... set to the song, Hero, by Mariah Carey.

Kila mwaka wanawake na walimwengu kote ulimwenguni huadhimisha SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE DUNIANI ambayo husherehekewa tarehe 8 Machi.
Mamia ya shughuli na matukio hufanyika ndani ya mwezi mzima wa Machi kusherehekea na kuadhimisha harakati za wanawake duniani katika Uchumi, Siasa na ukombozi wa Jamii ambapo Serikali, Vikundi vya wanawake na mashirika mbalimbali huchagua kauli mbiu kuakisi masuala ya kijinsia katika jamii husika na ulimwengu kwa ujumla.
Kauli mbiu ya mwaka huu kutoka Umoja wa Mataifa ni WANAWAKE NA WANAUME KWA PAMOJA KATIKA KUSITISHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA.
Kati ya matukio makubwa yaliyofanyika kwama huu ni kongamano lililoshirikisha zaidi ya watu 400 huko Liberia lililofunguliwa na Rais wa kwanza mwanamke kuchaguliwa barani Afrika Bi Ellen Johnson Sirleaf ambalo pia litahudhuriwa na marais Tarja Halonen wa Finland, Rais Abdoulaye Wade wa Senegal na Rais Paul Kagame wa Rwanda.

Katika kuadhimisha hili, NAUNGANA NA WANAWAKE, WASICHANA NA WALIMWENGU WOTE KATIKA KUKOMESHA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WASICHANA.
Naungana na Lucky Dube pia katika kuwaombea wanawake kwa MUNGU. Nawaacha na kibao chake GOD BLESS THE WOMEN ambacho mashairi yake yako hapo chini. Sikia anavyowaombea na kuwashukuru. Akiwaita HEROES
HESHIMA KWENU KINAMAMA NYOTE

In the middle of the night I heard her pray so bitterly and so softly yeah...
She prayed for her children
She prayed for their education,
Then she prayed for the man that left her with her children.
We, praise heroes everyday
But there are those that we forget To praise
The women of this world.
They do not run from anything
They stand and fight for what's right
They do not run from anything
They stand and fight for what's right


Chorus
Oh oh oh...
God bless the women

Even when times are so hard
They are so cool, calm and collected.
They do not run from anything,
They stand and fight for what is right
They do not run from responsibilities
They stand and fight for what Is right

Chorus till fade...


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nami nawatakia wanawake wote duniani siku njema.

Subi Nukta said...

Asante kwa kutukumbuka.
Nawaombea afya tele, ujasiri mwingi, hekima na maarifa pamoja na upendo daima, wanawake wote ili waweze kuwa chachu ya utu na ubinadamu mwema. Mungu na atubariki pasina kipimo.

Albert Kissima said...

Ukatili dhidi ya wanawake na wasichana naupinga vikali na naungana na walimwengu ktk kupinga ukatili huu.

Kuna changamoto hapa. Kuna wanawake wanaonyesha ukatili kwa wanawake wenzao,wanaonyesha ukatili kwa wasichana, kwa hiyo watu wasifikiri wanaume tu ndio wanaowakatili wanawake na wasichana.

Elimu juu ya ukatili na manyanyaso kwa jinsia zote ni muhimu,watu wafundishwe kuishi kwa amani na upendo. Watu waelimishwe kuhusu kuachana na dhana potofu za kizamani kama zile za ktk familia baba ni kichwa na mama ni mkia, nk, matabaka haya yanachangia sana ukatili wa wanawake ktk jamii.

Amani,upendo,umoja,wote tupige vita ukatili wa wanawake na wasichana duniani.

ERNEST B. MAKULILO said...

Binafsi naungana na wote wanaosherekea siku hii.Hii si kwamba wanawake pekee ndio siku yao, la hash, huwezi kuwa sherehe au maadhimisho kama haya bila wanaume kushirikishwa pia….maana kuna haki zao ambazo zinashikwa au “zinabakwa” na wanaume, hivyo wanaume nao wahusike ktk kufanya mabadiliko ya mfumo dume kupungua au kuisha kabisa.

Kwa uapnde wa Tanzanzia ambapo mimi nina mifano mingi.Inapokuja suala la haki za kijinsia, GENDER…watu wengi wanachukulia ni upande mmoja, si kweli.Na limepewa upendeleo fulani.Mfano chukulia sheria ya ubakaji.Kwa sheria ya Tanzania, definition ya ubakaji ipo wazi na imesema ni kitendo cha kuingiza uume kwenye uke bila ridhaa ya muhisika.Maana yake ya haraka haraka ni kwamba mwanaume hawezi kubakwa.Sasa sheria hii ipo upande mmoja.Hapa Marekani hata mwanaume anabakwa.Hivi nini maana BAKA?au KUBAKA?

Mfano mwingine wa wazi ni kile kitendo kumtangaza nani awe Tanzania One ktk matokeo ya kidato cha sita mwaka 2005. Kulikua na yule dada, simkumbuki jina, kwasasa yupo UDSM anasoma sheria mwaka wa nne, alipata division One yenye points tatu, lakini alipara ktk combination yake ya HKL A ya History na Kiswahili, lakini kwenye English akapata C, lakini alifanya Divinity (just like bible knowledge kwa O-Level) alipata A. Na kulikua na jamaa mmoja, Moses Mwizarubi, sina uhakika na spelling za jina lake la pili alipata Division one yenye 3 points, A tatu ktk subject combination yake ya PCM. Ikumbukwe huyu Moses alikua Tanzania One tena wakati amemaliza Form Four.Sasa cha kushangaza NECTA ikatangaza kuwa huyo dada ndio Tanzania One na Moses Mwizarubi ni wa pili, sababu ndio hiyo Gener empowerment.Nijuavyo ni kwamba, unapofanya Divinity au Islamic Knowledge ni kama pili pili hoho kwenye chakula, haiwashi ni apetizer flani tu, maana yake haina effect, impact ktk kutathmini na kuchagua nani bora.Ndio maana hata katika vyuo vikuu kipindi cha admission mtu hachaguliwi kwa vigezo vya masomo hayo ya Divinity au Islmic Knowledge kuingia chuo kikuu.Na hakuna combination Tanzania yenye hayo masomo.

Mifano hiyo miwili ni kuleta changamoto kuwa tunapozungumzia mambo ya wanawake na kuondokana na mfumo dume, isitumike kigezo cha kupindisha sheria, kitendo cha kupendelea jinsia moja nk.

Pia napenda kjuwapongeza wanawake wengi wa Tanzania ambao wamefanya mambo makubwa sana hapa duniani….Dr.Migiro, Prof. Anna Tibaijuka, Mama Mogela.Hawa kwa upande wa Tanzania na dunia wamefanya mambo mengi mazuri kwa uwezo wao, ni mfano tu kati ya wengi ambao siwezi kutaja listi yao yote hapa.Ila wanaibua hamasa na kuwa role models wa wanawake na wanaume wengine kwa Tanzania na dunia nzima.

Kwa upande wa nchi zingine, tunaona uwezo wa Bi. Angela Mackel, kiongozi wa Ujerumani, Bi.Cond Rice, Bi. Hilary Clinton, Bi.Scott, Bi, Bhutto, Bi. Michelle Obama na wengine wangi ambao wa[po si tu kwenye anga ya siasa.Hawa wanaibua changamoto kubwa sana kwa watu wengi na kuondokana na mfumo dume, au hata gender discrimination, maana kipindi kingine wanawake kwa wanawake ni vita kali.

Ktk siasa zetu za Tanzania na Afrika kwa ujumla, wanawake wasitumiwe kama chambo cha wanasiasa kujinufaisha wenyewe.Hii inaonekana ktk kipindi viongozi wakiingia madarakani huwasahau kabisa kutunga sheria au policies ambazo zinaweza kuwasaidia.Lakini ikifika karibia na uchaguzi ndio kuwarubuni kwa kanga, chumvi nk ili wapate kura waingie madarakani.Tupingane nalo hili wandugu.

Siku njema
MAKULILO Jr,
West Virginia, Marekani
http://www.makulilo.blogspot.com

ERNEST B. MAKULILO said...

WANAWAKE KUWENI NA MOYO WA DA SUBI

Mzee wa Changamoto,
Mi nauliza hivi wanawake wengi wa kitanzania wangekua na moyo wa Da Subi wa kujishughulisha na kuendeleza PUGU ingekuwaje???Naamini kabisa utegemezi ungepungua, umoja, amani na upendo ungeongezeka kati ya wanawake, na wanaume pia.Kitu kingine ni maendeleo ya jamii zetu yangepatikana.

Napenda wanawake wen gi wawe Da Subi, mambo yatakuwa shwari.

Nawasilisha hoja wandugu
MAKULILO Jr,

Ivo Serenthà said...

Let me remind

Miriam Makeba his music and his songs against apartheid in South Africa.

Benazir Bhutto to be returned to his country in Pakistan,have been killed for his ideas.

Anna Politkovskaya.la Russian journalist killed for his investigations in Chechnya.

Happy March 8 to all women

Marlow

Subi Nukta said...

Makullilo Jr,
Tangu siku nilipomsikiliza marehemu Baba wa Taifa mwl. J.K.Nyerere (Mungu mlaze pema) na kauli mbiu yake ya PUGU (Pata Ujuzi Gawia Umma), siku zote ninajitahidi kuiishi. Huwa najisemea, siasa si hasa bali visa na mikasa ni bora kuPUGU - ndiyo mojawapo ya siri ya mafanikio, tizama nchi zilizoendelea ndiyo utagundua kuwa ni kwa njia ya PUGU wameweza kuwa na wajuzi wa mambo mbalimbali katika fani kedekede. Daima dumu nita-PUGU, kauli mbiu na urithi wa thamani alioniachia marehemu J.K.Nyerere (pumzika pema Babu).