

Bahati mbaya Justine aliondoka na kwenda nje ya nchi kwa zaiara ya kimuziki na aliporejea hakukaa muda mrefu akakutwa na mauti.
Ni katika kipindi kifupi saana tangu afariki, wasanii mbalimbali wa muziki wa Reggae Tanzania walikusanyika na kuandaa wimbo maalum (na baadae tamasha) kumuenzi mfalme huyo wa Reggae. Katika kutengeneza hilo, wasanii hao walitumia midundo ya nyimbo zake na mashairi toka katika nyimbo za Kalikawe toka katika albamu mbalimbali na kuunda wimbo HAKUNA.
Huu ni kati ya nyimbo bora za reggae kuwahi kuandikwa nchini Tanzania na ni kwa sababu mbalimbali zikiwemo.
1: Ulijumuisha wasanii nyota karibu wote wa muziki huo nchini akiwemo Inno Galinoma, Jah Kimbuteh, Ras Inno Nganyagwa, JhikoMan, Carola Kinasha, Athanas Sajula na wengine wengi.
2: Ulifanyiwa mazoezi kwa muda mfupi na kuimbwa kwa ufasaha.
3: Ulijumuisha midundo na mashairi ya Kalikawe ambayo yalikuwa yakisimuliwa na wasanii hawa
4: Ulionesha umoja wa wasanii wa Reggae nchini
Mbali ya hayo yote, pia uliweza kushinda tuzo na pia kutumika kwa muda mrefu zaidi.
Nami leo nawaletea kundi hili la Tanzania Reggae Family katika wimbo huu HAKUNA ambao ulikuwa maalum kumuenzi nyota wa Reggae nchini Tanzania Justine Kalikawe.
Kama alivyosema (Justine) na kama ilivyokaririwa na wanamuziki hawa, nami nawakilisha kwako kuwa "hakuna atakayekuja kukufanyia yale utakayo yafanyake, hakuna atakayekuja kukuletea, yale utakayo uyapate. Itabidi ufanye mwenyewe"
Swali kwa wana Tanzania Reggae Family ni kuwa mu-wapi na mbona hakuna kilichoendelea baada ya hapa? Watu walitoa nyimbo na albamu lakini hatuoni umoja uliooneshwa hapa na uliodhamiriwa kuendelezwa.
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
3 comments:
kalikawe bwana, namkumbuka akipita mitaa ya kwetu kwa miguu kwenda town ezi zile nakaa kwenye vilima vya kashula
kifo chake majamaa wanakiema mengi sijui kama ni kwli kwamba mshikaji alifanywa kuwa msukula na matajiri fulani?
Astareha kwa amani, Na pia nimekipenda kipande hiki kizuri cha reggae kwani ni miziki yangu. Ijumaa njema pia
hapa kuna mambo kadhaa.the system haipendi watu wajue au kusikiliza nyimbo za hisia badala yeke wanahamasisha nyimbo za mapenzi.
rasta hapa.
amani.
Post a Comment