Tuesday, April 14, 2009

Kuna mwisho / kikomo cha kufikiri?


Nakumbuka msemo wa "shida huongeza maarifa". Niliusikia saana japo sikuwahi kuwekea mkazo sentensi hii. Kaka Kaluse aliwahi pia kusema kuwa bila matatizo ulimwengu huu ungekuwa "unaboa". Nimekuja kutambua kuwa watu wengi waliofanikiwa walianza harakati za mafanikio yao baada ya kukumbana na matatizo fulani. Wapo ambao baada ya kufiwa na wapendwa wao wakaanzisha vikundi kusaidia wenye matatizo kama hayo, wapo ambao kwa hofu ya kupoteza kazi wanaamua kujikita kwenye biashara kidogokidogo mpaka wanakuwa na uwezo wa kuacha kazi na kuendeleza biashara zao, na hata ambao kutokana na shida mbalimbali wanajikuta wakilazimika kutafuta njia za kujikwamua katika lindi walilomo.
Ukweli unabaki kuwa bila huo "msukumo toka nje" kuna uwezekano watu hawa wasingekuja kuwa jinsi wanavyokuwa kwa kuwa wanakuwa wamejiwekea kikomo cha uwezo wao wa kufikiri.
Najiuliza kama kuna kikomo cha uwezo wa mtu kufikiri?????

3 comments:

Simon said...

hallow,nice blog you have out there,
meet my blog too at
http://samvande.blogspot.com

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

najiuliza ulichokisema juu ya mafanikio ni nini? mtu aliyefanikiwa yuko je na anafananaje? na asiyefanikiwa je? kweli kuna ambaye hajafanikiwa maishani?

Anonymous said...

wanasayansi wanaamini kwamba uwezo ambao anautumia mwanadamu ni 1/1000 ya uwezo wake halisi. Hii inamanisha kuwa mwanadamu anaweza kuongeza upeo wake mara 1000.Vile vile wanaamini kuwa binadamu anapo ongeza mara 1000 si mwisho.uwezo huo huendelea mara elfu mmoja tena na tena na tena. From those finding we can conclude there is no limit of thinking for humam being