Thursday, April 16, 2009

Namtafuta RENATHA BENEDICTO

Yaweza kuwa binafsi lakini ni kwa kuwa nahitaji msaada.
Desemba mwaka 1999 nilikuwa miongoni mwa wasafiri waliokuwa kwenye hilo basi la Tawfiq ambalo kwa bahati mbaya lilipata ajali na kuua watu wengi alfajiri ya tarehe 23. Wengi tulijeruhiwa japo wengine tulihitaji huduma zaidi kulingana na majeraha yetu. Katika safari hiyo nilikuwa nimekaa na binti mdogo ambaye baadae alijitambulisha kwangu kama Renatha Benedicto. Alikuwa kidato cha pili shule ya sekondari Kibasila, Dar. Kuwa mdogo ama mwanafunzi, si sababu ya kumsaka leo. Namsaka kwa kuwa alikuwa shujaa katika siku hiyo na ninasikitika kuwa juhudi zangu nyingi za kusaka mawasiliano naye (zikiwa ni pamoja na kutumia redio) zimeshindwa kunirejeshea mawasiliano naye.
Katika ajali hiyo, nilijeruhiwa vibaya. Nilichubuka sehemu kubwa ya uso upande wa kulia. Nilipasuka juu ya jicho, ndani ya mdomo, sehemu mbili za kidevu, michubuko ya magoti. Pia nilikatika ulimi na kunifanya nishindwe kuongea kwa siku nilipokuwa hospitali. Pia ilinitibua mgongo ambao kwa miaka 9 iliyofuata nimekuwa nikipita kwa wataalamu mbalimbali kupata matibabu. RENATHA alikuwa zaidi ya mhudumu kwangu. Alitafuta dawa, kuhakikisha natibiwa, pia alihangaika kusaka mawasiliano ya kuwajulisha walio nyumbani kuwa tukingali hai (bahati mbaya mawasiliano hayakupatikana). Alihangaika wakati wote ambao nilikuwa siwezi kusema lolote kutokana kushonwa ulimi. Alitengeneza "chakula" kilichoweza "kushuka" kunipa nguvu na kuwa msemaji wangu akitumia taarifa nilizomuandikia kwenye karatasi na passport (kwa kuwa hatukuwa tukifahamiana kwa majina). KWA HAKIKA ALIKUWA MSAADA MKUBWA KWANGU.
Baada ya likizo tuliendelea kuwasiliana na mpaka alipomaliza shule mwaka 2001 na mara ya mwisho kuonana naye alikuja kuniaga (2002) akisema anakwenda Songea kusomea ualimu. Aliahidi kuwasiliana nami baada ya kufika huko na kwa bahati mbaya nami nikahama. Baada ya hapo nikaanza pilika za maisha zilizonifikisha huku nilipo, lakini kila nikifikiria "njia" ya maisha nauona mchango mkubwa alioweka maishani mwangu na najaribu kumtafuta bila mafanikio..
Nimeona leo niweke hapa ili kama kuna anayemtambua anisaidie kurejesha mawasiliano naye.
Ni Renatha Benedicto. Alisoma Kibasila Sekondari kati ya 1998- 2001 kisha akasema anakwenda Songea TTC.
Njia rahisi ya kuwasiliana nami ni barua pepe ambayo ni changamoto@gmail.com

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Pole sana kwa ajali hii mbaya, Ila namshukuru mungu kwa kukujalia uzima. Kwa kweli Mungu yupo. Na nakusifu kwa kumtafuta Renatha, lakini nakuomba kama hutaweza kuwasiliana naye basi kaa china na umwombee kwa sala kwani itakuwa zawadi nzuri sana. Nasema pole sana kwa mateso uliyopata.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

fuatilia chuo alichosomea labda wana rekodi za alpangwa wapi. njia ya pili ni kutafuta kwa utumia nguvu za ziada labda kama unaweza.

ajali huunaginisha watu pia.

Anonymous said...

Kweli ni stori ya kusikitisha pole sana kaka yetu kwa yaliyokupata,ninaamini utampata huyo binti,wasiliana na chuo alichokwenda kusoma.

Subi Nukta said...

Pole sana kwa ajali.
Renata huyu, ni hivi, Renata uliyemwona wewe na akakuhudumia bado yupo na wewe. Jichunguze na utagundua ni kwa nini mwili wa Renata huuoni lakini mawazo, hisia na akili za Renata bado unazo. Hatimaye utapata jibu ya kuwa Renata yupo na wewe, usikubali kuwa mwenye macho asiyeona bali mwenye heri anayeamini bilaya kuhitaji kugusa kwa macho ya mwili. Renata yupo na amekusikia we sema naye, mwambie yote na roho yako itaridhika na ndiye anayekugusa kwa kuwa anataka mzungumze lakini wewe umekuwa ukimsikia na kumtafuta kusikotakikana. Mwili wa Renata kwa kweli sina hakika uliko kwa kuwa wenyewe ulitenda wema na kwenda zake, huenda unafanya kazi nyingine kwa Mubelwa mwingine kadiri ya karama na vipaji ulivyojaliwa.
Sifa na utukufu una Yeye, Aliyekuwepo, Aliyepo na Atakayekuwepo. Kumjua Yeye ni hazina na raha ya pekee! Njia zake kuzitambua ni vigumu mno!

MARKUS MPANGALA said...

nipo upande wa pili nawasoma kwanza, mnasemaje. nawasalimia tu jamani, nimepita hapa leo

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Du Pole sana. Hadithi ya kusikitisha na kufurahisha. Wazo la Kamala ni zuri ingawa sidhani kama utapata jibu. Jaribu kwa Michuzi ambako kuna vichwa vingi zaidi, jaribu kila njia. Mtafute Renatha!

Fadhy Mtanga said...

Pole sana. Mungu alikuwa na makusudi kukukutanisha na dada Renatha Benedicto.
Naamini mtakutana tena.

Anonymous said...

Renatha Benedicto,huyu ni yule Renatha aliyekuwa anaishi Kawe karibu na CCM? Nilisoma naye mafundisho Kawe kanisani miaka hiyo ya tisini. Ushauri wangu unaweza ukatafuta ndugu zake maeneo ya Kawe CCM (Kama bado wanakaa huko) au try Kawe kanisani maybe wana-data zake au mtu wa karibu anayemjua. All the best