Thursday, May 14, 2009

Asiyewajibisha na awajibishwe

Wenzetu waJapan wanawajibishana saana. Na ni nchi nyingi zinazofanya hivi pia. Lakini kwa Tanzania inakuwa ni jambo la aibu kuona watu hawataki kuwajibika hata pale inapotoea kuna umuhimu wa kufanya hivyo. Kibaya zaidi ni kuwa hata kuwajibishana nalo ni jambo la nadra kutokea. INASIKITISHA.
Kuanzia sandakalawe ya MAFISADI mpaka sasa hakuna anayeonekana kuwa tayari kuwajibisha mtu, na pia hakuna aliye tayari kuwajibika. Sasa leo nimesoma kwa Kaka Evarist Chahali kuhusu WIZI ULIOTOKEA IKULU ambao haukushitukiwa mpaka baada ya mtu kunyakua ua tena (kwa mujibu wa mtuhumiwa) kwa lengo la kupima usalama wa rais bofya hapa kuisoma. Kisha nikasoma namna ambavyo KOMPYUTA YA MKUU WA POLISI NCHINI NA YA OFISI YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI zilivyoweza kuibiwa bofya hapa kuisoma.
Na mpaka sasa hakuna linaloonekana kuendelea katika kuwawajibisha wahusika.
Natamani kuamini kuwa hakuna anayejua lolote kuhusu chochote kinachoendelea juu ya wizi huu wa (pengine) sehemu nyeti kuliko zote kwa usalama na usiri wa mambo mengi ya nchi lakini nashindwa. Najua kuna wanaohusika na sitoshangaa kujua kuwa ukweli wa wahusika unawahusisha waheshimiwa ambao wanataka kupoteza baadhi ya data ambazo wanaamini zitaweza kuwaumbua.
Kama ni kweli kuwa hakuna wa kuwajibika katika wizi wa Ikulu, basi Rais awajibike kwa kutojijali na vivyo hivyo kwa Mkemia mkuu na IGP kuwa wakikosa wa kuwawajibisha basi wao wenyewe wawajibike.
Ni aibu, ni dharau na ni kuendekeza mambo yanayozidi kuhatarisha ukuaji wa nchi yetu.
NAACHA

8 comments:

Fadhy Mtanga said...

Hawana utamaduni huo. Nd'o maana hata baada ya tukio la milipuko, wapo bado wanadunda.
Ni hayo tu!

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli ni aibu na inasikitisha na inaonyesha kwa nini nchi yetu haina maendeleo.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hivi kompyuta au tarakishi zao ziliibiwa au ziliibwa? kipi kiswahili sahihi? wajibika kwa kosa hilo tafadhali

Mzee wa Changamoto said...

Sina hakika na kiswahili sahihi juu ya hili Kamala. Ntyamuuliza Prof Matondo na ninaamini kwa lolote litakalokuwa sahihi, kuna atakayejifunza. Lakini naamini pia kuwa hiyo haikuwa msingi mkuu wa maelezo ya post hii.
Shukrani kwa kuniwajibisha

Anonymous said...

kamala ndio unakosoa wenzako? kweli nyani haoni kundule. Mbona blog yako ina makosa kibao na hawakusemi

Ivo Serenthà said...

Hello Laurel,commented on the post of work below

Good evening to you

Marlow

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

anony, wasionisema ndio wanaosababisha makosa yaendelee kuwapo. naamini mzee wa C/moto hawezi kurudia kosa hili kwani mwisho wa kosa ni pale unapolitambua na kulikubali hivyo tayari kurekebisha.

ndio maana jamaa wanaendelea kuwa mafisadi kwa sababu hamuwasemi.

we sema tu na matokeo ni makuubwa tu!

Mzee wa Changamoto said...

Ni kweli Kamala. Kwangu haijalishi umeniambia kwa "tone" na madhumuni gani, lakini as long as nimeelewa nilichokosolewa, jitihada itakuwa ni kuhakikisha sirejei kumpa mkosoaji nafasi ya kunikosoa. Haimaanishi kuwa sitaki kukosolewa, LA HASHA. Ninalomaanisha ni lile nililofundishwa na mwalimu wangu kuwa "pale unapoweza, usimpe mtu nafasi ya kukukosoa" na pia wangu wa moyo amekuwa akiniambia mara kwa mara kuwa "unakuwa mjinga ni wakati wa kwenda, wakati wa kurudi unakuwa mwerevu". Maana yake ni kuwa unapofanya makosa unajifunza na kisha unahakikisha halirejei.
Asante kwako Kamala kwa kukosoa na kwako Anon kwa kuuliza kwani kumemfanya muulizwa aeleze la maana.
Blessings to y'all