Tuesday, May 12, 2009

Tanzania yangu na ELIMU YA UKARABATI

Unapojitahidi kutumia mfumo wa fulani katika kujifunza jambo fulani, basi ni vema ukajiandaa kupambana naye katika SOKO LA KAZI. Na pia ukitegemea yeye akufundishe kila kitu ili uje tishio la soko lake la kazi, kuna uwezekano wa kutoiona siku hiyo ikifika. Lakini tatizo ni kwamba wenbye mamlaka hawalioni ama hawatilii mkazo hili. Na limekuwa likisemwa saana na wengi wenye kuliona. Sijui kama kuna mwenye "blog ya akili" ambaye hajaandika kuhusu elimu yetu, mfumo wake, utolewaji wake, uwezeshwaji wake, ufanisi wake na hata umuhimu wake kwa "watahiniwa."
Binafsi nimepitia elimu ya ufundi kutoka Chuo Cha Ufundi Stadi kilicho chini ya VETA kilichopo Dodoma ambapo nilisomea ufundi wa kukarabati mitambo na kutengeneza vipuri (spare parts) mbalimbali. Na bado naendelea na kazi iliyo katika fani hiyo hiyo. Lakini tofauti kubwa niliyoiona ni kuwa mafunzo na vitendea kazi tutumiavyo (ambavyo kwa bahati mbaya ndivyo vitumikavyo mpaka sasa) haviendani na ukuaji wa teknolojia ya kisasa. Mashine tutumiazo zinatumika zaidi katika kufanya ukarabati na si uzalishaji. Na bado najiuliza kuwa ni wapi tunapotaka "wataalamu" wetu waende kufanya kazi? Ni kweli kuwa twategemea kuwafunza teknolojia ambayo itawafanya (kama watapata ajira) wawe wakarabati? Sina hakika kwenye fani nyingine kama utabibu na kwingine wanavyoweza kuoanisha elimu yao na wale washindanao nao. Lakini kwangu nimekutana na haya.....
Lathe Machine nilizojifunza ni hizi Zitumikazo kwa uzalishaji wa kisasa ni hizi
Milling Machines nilizofunzwa ni hizi
Zitumikazo kwa uzalishaji wa kisasa ni hizi
Ukweli ni kuwa unapokutana nazo kwa mara ya kwanza unajihisi kuwekwa kwingine, ulimwengu mwingine na kwa hakika uzalishaji wake ni wa haraka na ulio na makosa kidogo sana.
Lakini kwangu swali ni kuwa kwanini wahusika hawaangalii mahitaji ya ushindani wa kazi na kuwekeza katika masomo yaendanayo na mahitaji hayo?

6 comments:

Anonymous said...

Ukipata jawabu la swali lako tafadhali unipasie ili nami nijue sababu.
Maswali uliyouliza na 'kwa nini zako zote' zitakuwa zinajibu kitendawili cha ugumu tulionao WaTanzania katika kupata na kuanza ajira nje ya nchi.
Kinachonishangaza, katizame magari ya kisasa waliyoanayo wakuu sana kisha wanatembelea kwenye barabara zilizotengenezwa kwa vifaa duni kama hivyo ulivyoonesha kwenye picha, halafu wao watakwambiaje, 'Vifaa vyetu vya kisasa na madhubuti sana, usifidharau....!
Mubelwa, usichoke kushangaa mzee wa chchzzzz!

Fadhy Mtanga said...

Kuna mambo ukiyafikiria lazima upandwe na hasira. Tazama jinsi watu wenye dhamana ya ukuzaji wa mitaala wanavyofanya. Inavurugwa kuanzia elimu ya msingi, vipi sasa kuhusu inayofuata?
Kuna waziri nd'o akavuruga kila kitu katika elimu.
Lakini tusiwashangae sana wahusika, wanatuandaa kuwa vibarua wa wawekezaji.
Ni hayo tu!

Mzee wa Changamoto said...

Da Subi, nikipata ntakujuvya dadangu, japo nahisi kupata majibu ya maswali haya itakuwa "ndoto".
Kaka Fadhy, umemaliza hapa uliposema "Lakini tusiwashangae sana wahusika, wanatuandaa kuwa vibarua wa wawekezaji."
Sina la ziada. Ni kama nimepata jawabu

Ivo Serenthà said...

The work in this particular historic moment, it's important, really is the true wealth of any nation.

Hello Laurel,

Marlow

ashura said...

kazi mbona tunayo wallah'mazee nakuona upo makiniki hapo kazini...hivi huwa upo busy hivi, au sometime unakula kajisingizi hapoo kwenye hicho kiti? mhhh.nitaongea na manager wako hapo MD. mzee wa changa moto leo sina comments.

Anonymous said...

duh kiukweli kaka leo umenigusa mmno katika mtima wangu mana nilipo iona learth machine nimekumbuka wakati nipo veta moshi katika swala zima la IM ( instrument Mechanics ) nikiwajibika kupiga file , kutengeza viji instrument vidogo vidogo nawakumbuka wengi sana pale kama mwalimu waikenja , dah na wengine kibao pale ila kweli elimu ya Tanzania, wakati natengesa bosh za magari, kuchonga nati zile , mambo ya electro pneumatics, lol hi hi hiiiiiiiiiii kazi kweli kweli naomba nisiseme sana kwa leo duh kaka piga kazi sana kiukweli watu wantoka mbali usione tunachonga radioni kaka tumepitia mengi mpaka kufika hapa ha ha ha ha
sophia malkia wa bambataa