Wednesday, May 20, 2009

Ukweli wa ukweli na ukweli.

Ukweli kama ilivyo kwa kitu chochote kile, kina pande zote mbili ambazo ni upande mzuri na m'baya. Upande mzuri kuhusu ukweli ni kuwa japo unapita hatua mbili za awali ambazo ni za kukatisha tamaa, hatua ya mwisho ni ya faraja kama alivyosema Mwanafalsafa wa kijerumani Arthur Schopenhauer kuwa "All truth passes through three stages. First, it is ridiculed. Second, it is violently opposed. Third, it is accepted as being self-evident."
Lakini pia kuna ukweli m'baya kuhusu ukweli ambao hata Lucky Dube aliwahi kuuimba aliposema "the terrible truth about the truth is that, if you stand for it, you'll always stand alone"

Na hili (la kuwa na upande ambao unaonekana kuwa na ugumu) ndilo linaloweka ugumu wa nani anaweza kuvumilia hatua hizo mbili kabla hawajakutana na hiyo ya tatu inayodhihirisha uwazi na ukweli wa yanayojiri.
Bob Marley alisema "time will tell" na hata Nasio alisema "Truth will reveal" nami naamini kuwa kuna siku ambayo haya mengi yanayosemwa nyumbani Tanzania yatavuka hatua mbili hizi kwa wakati muafaka (when time tells) na ukweli kudhihirika.
Kisha swali la nani anasema ukweli litajibiwa. Ndio ukweli wa ukweli kuhusu ukweli.
Labda tumskilize Lucky Dube akiimba kuhusu UKWELI M'BAYA KUHUSU UKWELI kwenye kibao You Stand Alone toka albamu yake The Way It Is. Anaeleza ukweli wa kinachowafanya "waheshimiwa" kutotimiza ukweli wanaoahidi kuusema


Lucky Dube widget by 6L & Daxii

5 comments:

chib said...

Wote tunaombea wakati huo wa ukweli kuwa ukweli ufike.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kweli ilikuwepo mwanzo, ipo sasas na itaendelea kuwepo.

kweli siku zote ni nzuuuri sana na haijawahi kuwa mbaya. kweli iko vilevile, kuikataa kweli ni sawa na kujikataa mwenyewe kwani wewe ni sehemu ya hiyo kweli.

kuificha kweli ni sawa na kuuficha mto kwa kuufunika blanket.

kaweli iko vilevile ukiikubali, kuipenda na kuipokea, basi itakuweka huru. vinginevyo utaumia mzee

Yasinta Ngonyani said...

Asante kwa somo hilikwani nimejifunza kitu. nilikuwa najua tu ukweli/uhakikisho wa jambo kama lilivyo.

mumyhery said...

ni kweli, kweli ikidhihiri uongo hujitenga, haya acha tusubuiri, kweli itakapokuwa na ukweli

Christian Bwaya said...

Ukweli ni upi? Ikiwa mzuri? Je, haiwezekani ukweli ukawa mbaya? Ukweli ni ukweli unaposhahabiana na tuvijuavyo? Ukisemwa na tunaowaamini?

Ukweli una sifa zipi? Kuna anayeujua ukweli mkamilifu? Nauliza, tutaujuaje ukweli?