Tuesday, May 26, 2009

UTAMBUZI. Elimu ya lazima kwa wote


Sijui wewe wautafsirije UTAMBUZI lakini hakuna shaka kuwa ndio kitu kikubwa ambacho kinaifanya dunia kuwa ilivyo, na ni hicho hicho kitakachoifanya dunia kuwa mahala bora zaidi pa kuishi. Na hapa sizungumzii UTAMBUZI wa kina kama walionao Kaka zangu Shaban Kaluse, Kaka Kamala na wengine wanaochukua mafunzo pale Kimara, bali hapa nazungumzia utambuzi binafsi na wa awali ambao wao wamekuwa wakiuzungumzia mara kwa mara, wenye manufaa na wa lazima unaofunzwa na wazazi na hata DINI mbalimbali. Utambuzi wa awali ambao hata kwenye Biblia wanausema wanapoonya juu ya kutoa boriti kwenye jicho lako kabla hujaangalia kibanzi kwenye jicho la mwenzako.


Nazungumzia utambuzi ambao utamfanya kila mmoja kujijua mwenyewe na kisha kumjua mwenzake, ambao nina hakika ni chanzo cha kuheshimiana na kuthaminiana. Iwapo kila binadamu atatambua kuwa yuko sawa na mwenzake na kuwa ni muonekano wa nje tu unaotufanya kujiona wa thamani kuliko wengine, basi tutatambua kuwa sote tuko sawa na hakuna haja ya kubaguana bali tutaheshimiana. Ni hapa ambapo Lucky Dube alisema "Respect mankind for who they are, and not what they are". Maana kubwa ni kuwa mheshimu binadamu kwa kuwa ni binadamu na si kwa kuwa yuko hivi, anakaa hapa, anavaa hivi, anahusiana na fulani, kaelimika vile, ana cheo fulani n.k. Ni kundi hili hili la utambuzi ambalo hata Emperor Haile Sellassie alilizungumzia katika hotuba yake kwa Umoja wa Mataifa Oktoba 4, 1963 kuwa "...until the philosophy which holds one race superior and another inferior is finally and permanently discredited and abandoned: That until there are no longer first-class and second class citizens of any nation; That until the color of a man's skin is of no more significance than the color of his eyes; That until the basic human rights are equally guaranteed to all without regard to race; That until that day, the dream of lasting peace and world citizenship and the rule of international morality will remain but a fleeting illusion, to be pursued but never attained;...." Yote haya ni kuhusu kujitambua.


Mpaka pale viongozi wetu watakapotambua kuwa wao ni kama sisi na hakuna haja ya wao kuiba na kujilimbikizia mali za wizi ambazo kwa hakika haziwafai sana hasa pale waliowachagua wanapotaabika, basi nchi haitaendelea.


Mpaka pale vijana watakapojitambua kuwa ni sehemu kubwa ya mabadiliko na sehemu muhimu ya maendeleo ya nchi na wanahitaji kushiriki katika maendeleo ya nchi leo na si kesho, basi nchi haitaendelea.


Mpaka pale viongozi wa dini watakapojitambua na kuutambua ukweli wa kile wanachostahili kufanya na kuanza kuhubiri neno na si kutishana, basi wengi hawataandaliwa vema kwenda kuuona ufalme wa Mbingu.


Mpaka pale bloggers watakapojitambua na kutambua umuhimnu wa kile wafanyacho na kanza kuisaidia jamii kujitambua na kujielekeza kwenye kuyakabili matatizo ya jamii, basi wananchi wataendelea kupewa udaku tuuu.


Ni UTAMBUZI ambao utaleta mabadiliko katika jamii yetu, na ni utambuzi huu huu ambao kwa kukosekana kwake, tunaona tunavyoshindwa kuthaminiana na kuheshimiana na hivyo kushindwa kusonga.


Ni Utambuzi, ni Utambuzi, ni Utambuzi. Najua nahitaji kujijua zaidi, kujitambua na kisha kuwatambua wenzangu na ndio maana nasikiliza zaidi Echoes of my mind

Blessings

7 comments:

Fadhy Mtanga said...

Kaka umenifikirisha sana na hiyo speech ya Haile, ambayo kijana mwanamapinduzi kutoka St. Anns akamalizia kwa kusema, 'It's war'
Until the day, African continent will not know peace, we Africans will fight if we find it necessary, and we know we shall win. As we are confident in the victory, a good over evil. It's war.
Ni hayo tu!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

usipojitambua utajidharau na kudharauliwa, huwezi kujitegemea wala kufanya mambo kwa mkabala wako utakuwa tegemezi daima!

umeongea vyema, ni lazima tujitambue kwanza sisi na sio viongozi kwanza. ni lazima tuutambue na kuuheshimu utu wetu badala ya vitu. kujitambua muhimu kwa kila mmoja japo sisi tunatafuta pesa kwanza.

umelongo mkuu, mohyoge waitu, haibambi omwona yagamba

Yasinta Ngonyani said...

Nimenukuu kwa kweli hapa umenena nimependa ulivyonena kwani ni kweli.Ningependa wengi wangepita hapa na kusoma kujifunza. "Ni UTAMBUZI ambao utaleta mabadiliko katika jamii yetu, na ni utambuzi huu huu ambao kwa kukosekana kwake, tunaona tunavyoshindwa kuthaminiana na kuheshimiana na hivyo kushindwa kusonga.

Ni Utambuzi, ni Utambuzi, ni Utambuzi. Najua nahitaji kujijua zaidi, kujitambua na kisha kuwatambua wenzangu" Yah! ni muhumu sana kwanza mwenyewe na kisha wengine.

Ubarikiwe

Bwaya said...

Nakubaliana na wewe. Kutaka kufahamu mambo mengi pasipo kuanza na kuijua nafsi yako, ni upotevu mkubwa kuliko mwingine wowote ule.

chib said...

Barabaraa, kujitambua muhimu bro.

Anonymous said...

IDENTITY.


Rasta hapa.

Anonymous said...

Mpaka pale JUMUWATA,Itazalishwa upya na kuthaminiwa kulingana na ujumbe ndani yake,mimi mwana blogu sito achaa kusisitiza na kuomba ushauri kwa wale watakao kubali kutoa ushauri kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Rasta hapa.