Monday, May 18, 2009

Za Kale vs Maisha ya sasa.. BINADAMU HAWANA WEMA


Kama kuna kiumbe hatari duniani, basi ni kiumbe ambacho chaweza kuwa bora zaidi. Nacho ni BINADAMU. Ubaya na ubaya wa binadamu ni kutokana na uwezo wao wa kuonesha na kuvuta hisia na imani ya watu ambao si lazima awe ana nia aoneshayo usoni mwake mbele yao. Martin Luther aliwahi kusema kuwa binadamu anaweza kufanya ukatili ambao haudhaniki na hautendeki na kiumbe kingine chochote ulimwenguni. Anaweza kutenda kila awezacho kukuonesha anakuali ilihali anafanya juhudi mchana na usiku kukuondoa katika unyoofu wa maisha yako ikiwa ni pamoja na kukukatisha uhai wako. Sikilia kisa kiimbwacho naye Hassan Rehani Bitchuka akiwa na wana OSS katika wimbo huu Binadamu Hawana Wema



** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

6 comments:

Evarist Chahali said...

Asante kwa kutukumbushia enzi.Ntakuwa sikosekani hapa every monday

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli binadamu ni binadamu. Asante kwa kipande hiki cha ZILIPENDWA.Jtatu njema

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mimi nassema binadamu ni mzuuuuuuuri sana na dio maana mimi nawewew tu biunadamu. asemaye ni mbaya na ashindwe na alegee.

Mzee wa Changamoto said...

Asanteni nyote kwa kushiriki nasi.
Pamoja Daima

chib said...

Kamala ameniacha hoi kabisa. Ha ha haa

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

chib,
we jiagalie kwenye kioo harafu huone ulivyoumbwa kwa malingo lukuki. mara nywere nyeusi, mara macho meupe mara meusi, mara ndeve nk nk. tusishuke kote. harafu mtu aseme we ni mbaya?\we anaglia picha zoote za profiles zipendezavyo harafu vitabu vya kumwogopea mungu vinasema sisi ni mfano wake, eti alipuliza japo hana mdoma. sis wazuuri tu asikudanganye mtu