Monday, May 4, 2009

Za Kale vs Maisha ya Sasa....SOLEMBA

Katika albamu yake ya mwaka 2005, mkongwe Burning Spear aliimba kuhusu Mapenzi katika wimbo wake FIX ME ambapo baadhi ya mashairi yanasomeka kuwa
"Love can make so Happy,
Love can make you so sad,
love can make you so lonely,
Love can make you accomplish,
Love can make you go places,
Love can make you so strong,
Love can make you your future,
love can make you REMEMBER THE GOOD TIMES AND BAD TIMES, ....."
Spear aliimba mengi katika ukweli wa maisha ya mahusiano miaka ya sasa, lakini pia yalikuwa hivyo tangua zamani na bila shaka yataendelea kuwa hivyo.
Mapenzi ni kitu kizuri saana kama kilivyo kibaya. Namaanisha uwezo wa uzuri wake ni sawa na uwezo wa ubaya wake iwapo yatakwenda visivyo ama kinyume na matarajio.
Katika kujikumbusha muziki wa kale, leo tunao wana Msondo Ngoma enzi hizo wakijulikana kama Juwata Jazz Band wakiwa naye marehemu Nico Zengekala ambao wanakuja na kibao chao SOLEMBA. Kisa mwanana juu ya binti aliyeamua kutotekeleza ahadi yake kwa mtindo / style ya kukomoa ambapo mwimbaji anasema alipomuuliza Solemba aliambiwa kuwa anajipendekeza kwake na yeye hampendi. Kama kuna kitu nilitamani, basi ni kusikia upande wa hadithi hii ukisimuliwa na Solemba mwenyewe kujua kama alichoimba Zengekala ndio hadithi kamili ama la. Labda itatokea, lakini kwa leo burudika na sehemu hii ya kisa SOLEMBA kama kisimuliwavyo naye Nico Zengekala

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

asante kwa kipande hiki juma3 njema

Subi Nukta said...

Jamani eeh, hiki kibao kipo sekunde thelathini tu ama ni kompyuta yangu imekula dakika tano nzima na ushee?
Ebu Mzee wa Chchzzz fanya uhakiki jamani la sivyo rudisha chenji zetu twende Msondo bana, ah, wafanya masikhara nini... tumeshachoka na mipasho ya Rostam na Mengi sasa na wewe utuletee za kuleta walahi tutakufurumusha tu maana wewe saizi yetu.

Mzee wa Changamoto said...

Da Yasinta. Heshima kwako Dada na nashukuru kwa "sala"yako kwetu kuhusu Juma3 hii.
Da Subi. Heshima kwako na karibu tena "jamvini". Mbona kwangu wimbo unacheza wote? Kwani umeangalia expiry date ya Komputer yako? Lol Ila kama kinacheza sekunde thelathini basi bofya hapo chini ya jina la wimbo inaposema "play full song here" ambapo itakupeleka kwenye "storage" yangu utakapoweza kucheza wotewote. Lakini kwangu ninacheza hata sasa na unacheza wooote.
Pole kwa hilo Dada. Naamini utaweza kuucheza na sitastahili kurejesha chenji
Hahahahahahahaaaaaaaaa.
Karibu tena

Subi Nukta said...

Ah, sikuwa nimevaa miwani tu sasa na wewe usijidai kuwa ndo umenionesha, bwana we, ah, kuumbuliwa mtu mzima nongwa!
Shukran!

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahaaaaaaaaaaa.
Usijali. Wala hakuna aliyekuwa na hakika kuwa hukuweza ku-play. Nami nilikuwa nalidha "kiingilio" changu kisidaiwe. Lol.
Kama umeweza kuona na pengine kusikiliza kwa makini utakuwa umerejesha kumbukumbu kadhaa nyuma. Labda mavazi, labda utunzi, labda maisha tu kwa ujumla, na ama labda lolote kuhusu sanaa na maisha. Na hilo ndilo kubwa. Kuangalia ZA KALE vs MAISHA YA SASA.
Karibu tena