Saturday, June 6, 2009

Je! Kula nyama nyekundu ni hatari kwa afya yako?

Kuna maswali mengi ambayo yamekuwa yakitokea kuhusu ulaji, faida na hasara za kula nyama nyekundu. Na maelfu ya watu (nami nikiwa mmoja wao) wameacha kula nyama nyekundu kwa sababu mbalimbali. Wapo wasiokula kwa sababu za ki-Imani, wapo wasiokula kwa sababu za kiafya na wengine kwa kuwa tu wanasikia hili na lile la kutisha kuhusu nyama hizi.
Lakini ukweli ni upi kuhusu Nyama nyekundu? Kuna faida na hasara gani kuzila? Ni kweli kuwa zinachangia zaidi kuugua maradhi ya Kansa kama isemwavyo na wengi? Je Maradhi ya Moyo na Kisukari?
Mtandao unaojishughulisha na masuala ya Afya wa WebMd unajibu maswali 10 yanaolizwa zaidi kuhusu ULAJI WA NYAMA NYEKUNDU.
BOFYA HAPA kujifunza zaidi.
JUMAMOSI NJEMA

2 comments:

Fadhy Mtanga said...

Ahsante sana mkuu kwa post hii. Nami ni mmoja ya walioitosa nyama nyekundu. Leo nimepata maarifa makubwa sana.
Ni hayo tu!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mimi nadhani sasa tunavuna matunda ya utandawazi. Ng'ombe wanalishwa mahomoni na hata nyama za ng'ombe wenzao zilizosagwa eti wakue haraka na kunenepeana. Naamini kabisa kwamba nyama ya ng'ombe wangu aliyeko kijijini Bariadi ni salama na hata siku moja sitajivunga kuila nikienda nyumbani na mama akanichinjia dume la ng'ombe. Hizi za madukani na kwenye ma-mall kwa hakika ni za kuogopa kwani huwezi hata kujua unakula kemikali gani! Na hapa ni kila nyama hata nyama nyeupe wakiwemo kuku -ni homoni na kemikali tupu! Mtu unakula kuku lakini laini na bila ladha kama unakula karatasi!

Halafu jambo jingine. Ukiwasikiliza sana hawa wataalamu wakati mwingine hutaweza kula cho chote. Leo watasema hiki na kesho wanasema kinyume chake. Leo watasema mvinyo nyekundu ni nzuri kwa moyo, na kesho watakwambia mvinyo hiyo hiyo ina kemikali mbaya sana zinazodhuru ini n.k. Mpaka mtu unafikia kujiuliza sijui ule kipi na uache kipi. Mimi nakula kila kitu lakini kwa mzunguko...