Thursday, June 4, 2009

Them, I & Them ...ALPHA BLONDY.... Jerusalem

Wiki hii imeshuhudia mambo makubwa mengi mojawapo likiwemo la Rais wa Marekani kwenda kuhutubia nchini Misri katika kile kilichoitwa Hotuba kwa Ulimwengu wa KiIslam. Katika hotuba hiyo ambayo imepokelewa vema sehemu kubwa ya ulimwengu huku wengine wakionekana kuipinga, Rais Obama amezungumzia kuhusu kufanya kazi pamoja ili kurejesha Imani na Amani baina ya mataifa. Amezungumzia umuhimu wa kuelewana na kuonesha juhudi katika yale tunayoweza kuafikiana kuliko kukuza tofauti.
Lililoonekana kuwa kubwa zaidi, ni mgogoro wa mashariki ya kati ambapo katika hotuba yake, Rais Obama amesema ni kuwa sasa ni wakati wa kutengeneza maisha bora kwa wakazi wa mashariki ya kati, kuwatengenezea ulimwengu bora, "a world where Israelis and Palestinians are each secure in a state of their own and nuclear energy is used for peaceful purposes, a world where governments serve their citizens and the rights of all God's children are respected. Those are mutual interests. That is the world we seek. But we can only achieve it together." (Rais. B.H Obama)Bofya hapa kwa hotuba kamili
Ni katika kuutamani ulimwengu huo usio na vita wala migongano, narejesha wimbo huu toka kwake Alpha Blondy uitwao Jerusalemu ambao ulitoka kwenye kipengele hiki tarehe 10 Aprili mwaka huu
Fuatana naye katika wimbo huu uliorekodiwa nchini Jamaica mwaka 1986 akitumia bendi ya Bob Marley (The Wailers). Bob ndiye alikuwa chachu ya Blondy kukacha elimu na kujikita kwenye muziki.
Msikilize.


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Namwomba Mungu asikilize maombi yetu watu waweze kuelewana na kuwa na amani duniani kwote. Waweze kusikilizana pia. IJUMAA NJEMA NAWE PIA Mzee wa Cangamoto.

Fadhy Mtanga said...

Jerusalem, the touchful song.

Hii dunia tumeiharibu sisi wenyewe tuloumbwa tuitawale. Shukrani kwa Obama kuona umuhimu wa kuifanya iwe pahala salama.

Ijumaa njema kaka!