Friday, June 19, 2009

Them, I & Them...CHILDREN OF TOMORROW...Morgan Heritage

Image from http://forchildrenoftomorrow.blogspot.com/
Jumanne ya wiki hii tulishuhudia kuadhimishwa kwa Siku ya Mtoto wa kiAfrika (INTERNATIONAL DAY OF AFRICAN CHILD (Click for more)) ambayo imekuwa ikiadhimishwa tangu mwaka 1991 kukumbuka ujasiri wa watoto uliopelekea mauaji ya kikatili yaliyotokea huko Soweto Africa Kusini Juni 16, 1976.
Mauaji haya yalitokana na watoto kuomba haki yao ya kuelimishwa vema na pia kuelimishwa katika lugha yao. Kwa hakika ujasiri waliouonesha watoto hawa kwa kudai walichodai katika wakati wa ubaguzi ulikuwa wa hali ya juu na unastahili kuendelea kukumbukwa.
Lakini sasa hivi watoto wakiishi maisha ndani ya mataifa yanayojiita ya kidemokrasia wanaishi maisha ya hatari na magumu zaidi. Maisha ya wazazi na walezi wao yanawaweka katika hali mbaya kiuchumi, kiImani, kiAfya, na kuwafanya waishi maisha mabovu zaidi. Wengi wanahaha kwa vita vinavyoendelea kuuua wengi wasio na hatia, kuacha wengi wakiwa yatima na kutesa wengi wasiojua kinachoendelea.
Tumeshaandika mengi kuhusu vita na athari zake kwa watoto kama unavyoweza kusoma hapa nilipoandika kuhsu watoto wote ulimwengini katika CRY FOR THE CHILDREN ama kwa kubofya hapa (click here).
Sasa ni wakati wa kuwatengenezea watoto wetu maisha mema na mustakabali mzuri wa kule waendako.
Basi Ijumaa hii tuungane nao Morgan Heritage katika wimbo huu wa taratibu kiasi na wenye hisia kali wakiimba kuhusu "watoto wa kesho" yaani Children Of Tomorrow.

Labda kwa nyongeza tu nimjumuishe Luciano anayekuja na wimbo maalum kwa watoto wote akisema This One Is For the Children na humo anauliza maswali mengi sana. Msikilize hapa anapouliza maswali mengi juu ya watoto wa leo watakavyokuwa hiyo kesho wanavyokuzwa wakiona mabaya yote na kutoutambua mfumo mzuri wa maisha katika jamii zetu. Na wito wake ni "let's protect our children and help them to grow, Let's prepare their future, teach the youth what they need to know"

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

4 comments:

Mija Shija Sayi said...

Bless you Mubelwa.

chib said...

Naungana nawe mia kwa mia

chib said...

Naungana nawe mia kwa mia

Yasinta Ngonyani said...

nipo nawe jumamosi njema pia Mubelwa