Thursday, June 18, 2009

UBAYA. Hivi una faida?

Labda kwa jina lake wengi watasema HAPANA. Lakini kabla ya kujibu najiuliza ni nani aliyeita hilo tendo UBAYA. Unadhani wa upande mwingine hafaidiki?
Hebu angalia hilo lililopo nyuma yangu. UNADHANI LINA KAZI YOYOTE YA KUVUTIA? Lakini unadhani linagharimu kiasi gani kulitengeneza? Inakadiriwa ni dola milioni 83 (kwa makadirio ya mwaka 2006) na gharama zinaongezeka kila mwaka.
1:Unadhani ni watu wangapi wameshiriki kulibuni?
2:Unadhani ni watu wangapi wameshiriki kulitengeneza?
3:Unajua ni nchi ngapi zinashiriki kulitengeneza / kulitumia? Angalia bendera hizo
4:Unadhani katika nchi hizo ni wangapi wamepata ajira kutengeneza hilo?
5:Unajua linaendeshwa / kurushwa na maaskari ambao wana marupurupu kibao?
6:Unajua wengi wa wanaorusha hayo wanasomeshwa bure ili kutekeleza kazi yake?
Sasa hesabu wanaoshughulikia kusimamia "kazi" zake, wanaolifanyia matengenezo na ukarabati, wanaonufaika na mauzo ya mafuta na vipuri vyake na wengine.
Na hili ni moja kati ya "mitambo" mingi inayoendesha shughuli zake ulimwenguni.
Sote tunajua matokeo ya uwepo wa ndege za namna hii na athari zake ndizo tunazoweza kuita UBAYA. Lakini kwa yote niliyouliza na mengine mengi, bado swali linaendelea kuwepo kuwa KUNA FAIDA ZA UBAYA?
Blessings

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kazi kwelikweli. mi sina jibu ila nimeipenda picha ya huyo kijana aliyesimama karibu kama namfahamu:-)

Anonymous said...

HA HA HA HA WEWEEEEEE KAKA KAMA NAKUONA LIVE
SOPHIA

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mzee wa changamoto;
Iliwezekanaje mpaka ukaruhusiwa kulisogelea hilo dude la bei mbaya namna hiyo? Isije ikawa wewe ni FBI au CIA?

Nadharia moja inasema kwamba kila kitu hapa duniani kina pande mbili zinazokamilishana (upande mzuri na mbaya). Wafuasi wa nadharia hii hudai kwamba hata shetani ana mambo mengi mazuri kwani yeye hasa ndiye "anayempa" maana Mungu na kumfanya kuwa "relevant" Bila shetani (ambaye anaaminika ndiye chanzo cha uovu) pengine hata Yesu asingekuja duniani, amri 10 za Mungu zisingekuwepo.... Kwa mantiki hii ukitazama vizuri karibu viti vyote vinaakisi pande hizi mbili. Naamini kwamba hata ubaya unazo faida zake - na ndiyo maana kuna uzuri!!!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Typo katika meseji hapo juu.

Nilimaanisha vitu na siyo viti...lugha bwana!

Koero Mkundi said...

Ndio maana inmasemwa kuwa kila jambao baya lina uzuri wake,
Hivi kama kiwanda cha kutengeneza hilo DUBWANA kikifungwa ni watu weangapi wataandamana na kulaani juu ya kufungwa kwake.
Hata MNYONGAJI, unadhani atafurahi akisikia kuwa sheria ya kunyonga watu inafutwa?
NAAMINI ATALAANI NA KULALAMIKA.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mh. sijui sana, lakini binadamu wa leo anashindwa kujua uzuri wa uzuri na ubaya.

dunia yetu hii inaongozwa na nguvu hasi (negative powers) na ndiyo maana kila kitu kibaya kinaonekana ni kizuri.

matondo anaongelea juu ya ajira utadhani binadamu wa leo asingeongoza na nguvu hasi asingepata chakula!

ndio uliwengu wetu. umeona vyema juu ya viongozi wa dunia hii kupigania utawala wa dunia kwa kukataa kulipa kodi! kwani biblia inawaambia kuwa ulimwengu huu ni wa nani?

chib said...

Ubaya una uzuri wake wakati mwingine, kama kupe wakiwa wengi wanakunyemelea, nawe huwawezi....

Anonymous said...

Kamala unasema nini? Kama kawaida yako, komenti yako haieleweki.

chemshabongo said...

mkuu naona umeuliza swali huku ukiwa umeweka majibu juu yake,ingawa nilikuwa sijui kama ubaya waeza kuwa mzuri lakini wewe umenifungua na sasa nataka nijifunze kutouchukia ubaya.

kaka pole na matembezi yaani umefika hadi kulee!