Wednesday, June 3, 2009

Wajenga nchi wasiojengewa nchi

Amani, Heshima na Upendo kwenu nyote.
Nimekuwa nikijivunia saana ushiriki wa kinadada wanaBlog wenzetu ambao wanakuwa mstari wa mbele katika kuielimisha jamii kwa undani juu ya yale yawakumbao wengi wa jinsia yao ambao ni kama wanasahaulika. AMANI KWENU.
Nikirejea kwenye "toleo" langu la leo, nimesoma wasifu (sijui kama wingi wake ni nyasifu) wa wanasiasa mbalimbali walio na mamlaka na nguvu za kimaamuzi nyumbani Tanzania na sijakutana na yeyote ambaye anaonekana kuishi maisha duni saana enzi za utoto wao. Hili linaweza kuonesha kuwa wengi wao walikuwa na wazazi ambao walikuwa wakijishughulisha na pilika za maisha, hivyo kuna uwezekano mkubwa kuwa viongozi wetu walilelewa na kinadada wasaidizi wa ndani ambao wanafahamika kama WAFANYAKAZI WA NDANI ama HOUSE GIRLS.
Lakini haionekani kuwa kuna kiongozi yeyote anayeonekana kuwajali watu hawa ambao wananyanyasika kwa shida walizonazo na wanaotumiwa kuliko mipaka ya kazi zao na ambao wengine kwa umri walionao hawakutakiwa kuajiriwa.
Dada Koero aliwahi kuandika kuhusu WATUMISHI DUNI KULIKO WOTE (Bofya hapa kama uliikosa ambapo kulitolewa mchanganyiko mzuri sana wa maoni), Dada Yasinta naye mara nyingi kasema, Da Chemi pia hukemea unyanyasaji wa kinadada na pia Da Subi hukemea na kuonesha mengi akitetea haki za wanaonyanyasika. Moja ya video alizoshiriki nasi na ambayo ningependa kuiweka hapa ili ukiweza kuiona, uone jinsi Taifa linavyojengwa na wasiojengewa mazingira ya kuishi.
Poleni nyote muishio hivi na tuangalie kama kuna mwenye nia njema ya KUSAIDIANA NASI kuondokana na matatizo haya wakati wa uchaguzi ujao mwakani.
BOFYA HAPA kuitazama video hii na nyingine nyingi toka kwa Da Subi.

Asante Da Subi kwa video hii na kwa mkusanyiko wa Video ambao mara zote umekuwa msaada wa kusaidia kuelimisha kwa maono yale ambayo blogu hii na nyingine zimekuwa zikijitahidi kufanikisha
Uchaguzi Tanzania ni "label" inayozungumzia namna niionavyo nchi yangu ya Tanzania ijiandaavyo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Kwa maandishi mengine juu ya mada hii katika "label" hii BOFYA HAPA

6 comments:

Fadhy Mtanga said...

Kaka, nilipoiona video ile kwa da Yasinta niliandika maoni. Leo nirejee kwa kusema tatizo jingine ni kuwa, wanasiasa na pengine wanaharakati, huwatetea sana mahouse girl (wasio na utu wanawaita mabeki tatu) katika makongamano, warsha na mambo kama hayo.
Lakini wanasahau kuwa 'charity begins at home'. Namaanisha kuwa, wengi wa wanaharakati hawa, wanao mahouse girl majumbani mwao ambao wanakandamizwa pia. Hivyo hakuwi na dhamira ya dhati ya kuwakomboa.
Jana mchana nimepewa mkasa na binti mmoja, alichukuliwa na aunt yake aje Dar kusoma. Amefika hapa kageuzwa house girl. Ni mdogo. Anatia huruma.
Nawashukuru sana dada zangu wanaoblog, kwani wanatusaidia sana kuiweka jamii wazi dhidi ya haya mabaya yatendekayo kwa watu hawa tunaowaita mahouse girl (mi nalichukia sana hata jina lenyewe la uhouse girl)
Ni hayo tu!

Yasinta Ngonyani said...

Maisha, Maisha, Maisha haya eti house girl. Bado sijaona umuhimu wa kuwa na house girl.

Kwanza kabisa napenda kusema hii ina tokana na serikali. Kwasababu gani? Kama kungekuwa na chekechea nyingi basi natumaini wazazi wangewapeleka watoto wao huko. Ila naamini pia kuna wengine ambao ni wabahili na wanataka tu kuwaonea hao wasichana wadogo wasio na kisoma. Kuwanyanyasa.
Mfanyakazi wa nyumba halafu anafanya kazi zote yaani zoooteee hii inanipa uchungu sana kwanza wanteshwa halafu wanawapa mimba. Na pia nasikitika sana kwani kuna wengine hawajasoma kabisa hawajui hata kuandika majina yao.
Kusema kweli sioni haja ya kuuwa na mfanyakazi wa nyumba(house girl) hata mimi silipendi hili neno. Mwakani narudi na kugombea URAIS:-(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

aisee, sijui lipi jema kati ya kuwaajiri watoto na kuwaacha wakawe watoto wa mitaani na wafe njaa au watumikishwe na kuambulia kula hicho kidogo!!!

Mzee wa Changamoto said...

Asanteni kwa Maoni. Duh!! Ni wakati mchache unapokutana na points lean ambvazo ni karibu "ndio mzee" tangu mwanzo mpaka mwisho wa maoni.
Asante Kaka Fadhy, Da Yasinta na Kaka Kamala. Kaka Fadhy, hayo ni maisha ya wengi sana na inasikitisha kuona ndugu wanageuka watumwa. Dada Yasinta, kuna ukweli wa kuwanyanyasa wasioenda shule na inasikitisha. Kakangu Kamala, ni kweli kuwa kunaweza kuwa na unafuu wa kuwaajiri wasife njaa, lakini manyanyaso na mateso ambayo asilimia kubwa wanayapata ni mengi kulingana na wale wanaofaidika na kazi hiyo. Wapo waliofanya vema, waliojenga na kujiinua kimaisha kama alivyosimulia Dada Koero kwenye kisa cha Binti Yasinta. Ila unyanyaswaji uliopo unawaathiri karibu wote na mshahara wao ni mdogo hausemeki.
Asante kwa kufikirisha

Simon Kitururu said...

Inasikitisha sana!

Koero Mkundi said...

MIE SINA LA KUSEMA, KWANI NAOGOPA KUONGEZA CHOCHOTE, MAANA WALIONITANGULIA WAMESEMA YOTE....