Monday, June 22, 2009

Za Kale vs Maisha ya sasa.....PENZI HALIGAWANYIKI

Mambo mengi yanabadilika kulingana na mazingira, teknolojia, na nyakati lakini moja kati ya yaliyogoma kubadilika ni uwezo wa kugawanya penzi. Hili lilitokea tangu miaka mingi iliyopita na mpaka sasa hakuna ambaye ameweza kuligawa kwa watu wawili na kuwa na uwezo wa kusema ana hisia na matunzo yaliyo sawa kwa kila ampendaye. Ndio maana hakuna ubishi kuwa namna pekee ya kuepusha mkanganyiko wa mgawanyo wa penzi ni kutojihusisha na harakati za kuligawa.
Hii ilikuwepo tangu enzi za kale mpaka maisha ya sasa.
Tuwasikilize Vijana Jazz Band wakija na sehemu mbili za wimbo waliouita Penzi Haligawanyiki

Na sehemu ya pili hii hapa chini

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**
JUMATATU NJEMA

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Asante sana Jumatatu njema nawe pia Mubelwa!