Monday, June 15, 2009

Za Kale vs Maisha ya Sasa...SHUKRANI KWA WAZAZI

Tarehe 15 mwezi wa Juni ni moja kat ya tarehe zenye baraka saana katika Familia yetu. Ni tarehe ambayo (kama ilivyo leo) tunakumbuka matukio kadhaa muhimu yaliyotokea familiani. Leo wazazi wetu wanaadhimisha miaka 35 ya ndoa yao, kaka na shemeji yetu wanaadhimisha miaka 13 ya ndoa yao na pia Dada yetu anaadhimisha miaka 3 tangu aagwe rasmi (send off) kuelekea kuanza familia yake.
Kwangu mimi wazazi na walezi wangu hawa wameoninesha njia. Katika miaka yote niliyoishi na wazazi wangu nimekuwa nikijifunza maisha kwa mifano na matendo. Kuanzia Imani, Ukarimu, Heshima, Bidii katika kila jema nitendalo na hata mipango ya maisha. Nilijifunza kwa kuishi kama walivyoishi wao maana mara zote wamekuwa wakiishi kwa matendo. Vivyo hivyo kwa Kaka na Dada zangu
Leo hii tunapoadhimisha siku hii muhimu kwa familia zote tatu, ninapenda kutoa shukrani kwenu nyote na hasa wazazi kwa upendo na umoja walioonesha katika maisha yote tuliyowashuhudia na ambao unatuongoza sasa ambako tuko mbali nao.
Naomba kusema HERI YA KUMBUKUMBU YA NDOA YENU na katika kuisherehekea basi mjivunie kazi kubwa mliyoifanya kutulea. Ninaleta SHUKRANI KWA WAZAZI kama ilivyoimbwa nao wana DDC MLIMANI PARK
NB: Ubora wa muziki si wa hali ya juu na sauti ni hafifu ktk sekunde 35 za mwanzo. KUMRADHI KWA HILO na burudika

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

6 comments:

mumyhery said...

Hongereni nawatakia kila la heri

Yasinta Ngonyani said...

Nami nasema hongera sana na kila la kheri.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

familia yako ni noma kwa 15 june. duh

mimi sina cha kusema, ninahofu na wewe utafunga ndoa tarehe hiyo hiyo au vp?

Mzee wa Changamoto said...

Asanteni. Kamala, ni kweli kuwa 15 June ni big day. Sijui kuhusu mimi maana kama sijaoa basi ntajitahidi iwe hivyo, na kama nimeshaoa basi nifanye utaratibu mwana siku hiyo na kama ninaye basi niangalie ajaye.
Lol
Blessings

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Safi sana. Muendelee kubarikiwa!

Anonymous said...

Hongera kwa kumbukumbu nzuri ya familia. Muendelee kuwa wanafamilia bora!