Thursday, July 23, 2009

Kwani vipaji / fani hufunzwa ama twazaliwa navyo?

Hapa ni TASWIRA tu kwa kinaKaka wa familia ya Michuzi. Heshima kwenu. Picha toka Michuzi Blog
Vitali na Vlladimir Klistchko, wao ni mabingwa wa Ndondi wa Dunia Uzito wa juu
Kolo na nduguye Yaya Toure wao ni soka
Laila kama Babake Muhamad Ali
Ralf na nduguye Michael Schumacher wao ni Formula One
Baba na Mwana Bush waliopishana vipindi viwili vya Urais Marekani
Nimekuwa nikijiuliza swali hili kwa muda sasa kutokana na ukweli kuwa sina hakika kama watu wa familia moja hufanya mambo yanayofanana kwa kuwayako ndani ya damu ama kwa kuwa kuna mwongozo mzuri na wa manufaa toka kwa mwanafamilia mwingine ameonesha njia katika hilo? Unawakumbuka kina Njohote kwenye soka, Uvuruge kwenye muziki na wengineo wengi?Hebu Tazama hapo kisha unisaidie kujibu.

5 comments:

Unknown said...

Kaka naheshimu sana kazi yako.
Nimepita kusalimia kama kawaida.
kazi nzuri na inafikirisha.....

Fadhy Mtanga said...

Kaka nakubali kuwa vipaji mtu huzaliwa navyo, ama niseme hurithi.
Naamini hivyo sababu mama yangu ni mshairi, nami nimejikuta mshairi.
Dada yangu mkubwa ni mchoraji mzuri (ingawa hafanyi hivyo sasa, pilika za maisha) lakini nami nikafuata mkondo huohuo wa uchoraji.

Yasinta Ngonyani said...

Inawezekana ni kote kote kuzaliwa nanvyo au kurithi. Binafi sijajua ni kipaji gani ninacho:-)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yasinta fanya utaratibu kwani kipaji chako kipo kkwani pia waweza kuona na kukijua labda kupitia kwa wengine.

vipaji tunazaliwa nao, haviridhiwi. kuna kuwa insipired na kufanya kufauatana na yule anayekuinsipire japo sio kipaji chake. sasa vipaji vyetu ni sehemu ya kazi tulizokuja kuzifanya duniani na ndio maana tunaishi. wengi tuahangaihka kutafuta kazi na pesa huku vipaji vinahangaika kujitokeza.

niliamua kusomea kompyuta na IT kwa sababu baba alikuwa mwanakompyuta kumbe pamoja na yoote kipaji changu ni vitu vingine. nimefanya kazi kadhaa zinapendeza na kupokelewa labda kuliko wale waliozisomea.

kwa hiyo kipaji hakirithiwi bali yawezekana kipaji kile kile kikajitokeza kwa watu tofauti katika familia kwani kwa ngazi ya maumile hamna ndugu, baba au mama, kuna watut tu.

na ieleweke hivyo.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ni vyote kwa pamoja. Hata uzaliwe na kipaji namna gani bila kukiendeleza na kukiimarisha (kupitia mafunzo n.k) kipaji hicho kinaweza kisijidhihirishe na kufikia upeo wake. Mifano ipo mingi kuthibitisha dai hili karibu katika kila nyanja.

Talanta ukiichimbia chini........

Nilikuwa nimepotea kwa wiki kama mbili hivi lakini sasa nimerudi. Libeneke kama kawaida.