Friday, July 24, 2009

Them, I & Them...HOLD ON........Lucky Dube

Maisha tuishiyo yanaungana na mchanganyiko wa mepesi na magumu. Na wakati mwingine ugumu wa maisha yetu HULETWA na wale ambao tumeamua kushirikiana nao maishani japo yanaathiri zaidi ya wale waonekanao kuathirika. Mfano ni watoto wanaoathirika kwa maisha ya mzazi wao ilhali hawana namna ya kuyazuia. Ndio maisha yalivyo hapa duniani na tunaweza kusoma tukimsikiliza Lucky Dube katika wimbo huu HOLD ON ambao ameimba akimueleza mamake kuwa maisha yatabadilika kwa kuwa sasa amefikia umri wa kufanya maamuzi na ameshachoshwa na maisha ambayo mamake ameishi na sasa anataka kuyafanya kuwa bora zaidi, na kumfanya mama yake kutokuwa "kicheko" katika jamii.
Msikilize katika wimbo huu HOLD ON toka katika albamu yake House of Exile


I knew exactly what you were going through,
It's just that I didn't have the right to discuss your problems,
I saw you struggling for our education,
I saw you struggling to get us clothes to wear
Mama
This man you got married to is dead alive
Over the years I asked myself many questions
Is he my real dad or Was I adopted
Mama
I know it's difficult for you mama
But hold on I am a little grown up now

Oh Ho

Chorus:
Hold on just a little bit longer now (x4)

You were a laughing stock in the community
The press didn't rest makin' news out of you mama
Now is the time to show them
that he who laughs last laughs the best, that's the way it is (x2)

Chorus:
Hold on just a little bit longer now

I know it's not easy for you mama but your tears will turn to laughter now that I"m a grown up mama

Chorus till fade

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ijumaa njema nawe pia na Ahasante kwa yote.

Simon Kitururu said...

Bomba la Wimbo hili!
Asante kwa hili Mkuu!

chib said...

:-)
Wikend njema

Christian Bwaya said...

Dube ni kati ya wanadamu waliofanikiwa. Sababu ni kwamba ameacha legacy.

Ukipitia kumbukumbu za watu, unaweza sema hili ndilo hasa liliachwa na Dube.

Ni legacy gani tutaacha kama tukiondoka?

Je, ni lazima tuwe wanasiasa ndipo tuache kumbukumbu nyuma? Hapana.

Ni kwa vipi tunaweza kuacha kumbukumbu yetu halisi?

Hiyo ndiyo changamoto niliyoipata mzee wa changamoto.

Ijumaa njema!