Wednesday, August 12, 2009

Kongamano kwa BLOGGERS

Wakati umewadia ambapo sote lazima tukaribie,tuthubutu kisha tuone ni wapi tutafika.
Je wewe ni mwanablogu (Blogger) au mdau wa habari na mawasiliano kwa umma kwa kutumia mtandao? Kama jibu ni ndio, tafadhali unaombwa kujiorodhesha kwa ajili ya maandalizi ya Kongamano Maalumu la Kitaifa kwa ajili Wanablogu (Bloggers) na wadau wa habari na mawasiliano wa Tanzania (Tanzanians Bloggers Summit) linalotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu jijini Dar-es-salaam,Tanzania.

Dhumuni la kongamano hili ni Kuelimishana, Kufahamiana, Kuamsha Utambuzi Rasmi Kuhusu Tekinolojia ya Blogu na Mawasiliano ya Umma kwa Kutumia Mitandao, Kusaidia Utambuzi Rasmi juu ya mchango wa blogu nchini Tanzania kama chombo muhimu cha habari na mawasiliano, Kuelimishana jinsi gani blogu zinaweza kutumika katika kuleta maendeleo katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi, kuburudisha, kukuza utamaduni nk.

Wataalamu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wataalikwa kutoa mada na mafunzo mbalimbali kuhusiana na tekinolojia ya kublogu, zana nyinginezo za mawasiliano mtandaoni kama vile mitandao jamii(social networking), online forums nk.Kutakuwa na vipindi vya maswali na majibu.
Ili kufanikisha maandalizi ya Kongamano hili la kihistoria, kujiorodhesha kwako ni muhimu sana. Muda wa kujiodhoresha ni kuanzia tarehe 12/8/2009 (Jumatano) mpaka 12/9/2009 (Jumamosi) tu.

Kinachohitajika ili kujiandikisha ni :
Jina Lako,
Anuani yako ya barua pepe (E-mail),
Mahali Ulipo au unapoishi (Nchi,mji nk),
Namba ya Simu (sio lazima)
na
Anuani au URL(Universal Resource Locator) ya blogu yako (mfano www.kongamano.blogspot.com/wordpress.com/.com/typepad nk).
Vyeti vya Ushiriki vitatolewa kulingana na habari utakazoziorodhesha hapa.
Unaweza kujiorodhesha kwa kutuma ombi lako kwa barua pepe kwenda; summit@bongocelebrity.com.
Zingatia tarehe za kujiandikisha. Ni mwezi mmoja tu!
Asante kwa ushirikiano.
UMOJA NI NGUVU!
Jeff Msangi

2 comments:

Albert Kissima said...

Ni wazo zuri sana na natoa pongezi. Malengo yamewekwa bayana, hivyo kazi kwetu kujiandikisha.

Kwa upande mwingine,kama inawezekana kalenda ingeangaliwa vizuri ili ikiwezekana tarehe na siku ya kongamano hili iwekwe wazi.Hili litatusaidia kuwa na maamuzi yasiyokuwa na kigugumizi.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

pia watwambie mapema kama kuna malipo tunafanya sio watuite harafu walete za kuleta. time bado ipo watafutwe sposors ili hata wanaotamani kublogu, wafundihswe na sio kubakia kwa wachache wenye mihele pekee