Saturday, August 29, 2009

Miaka 7 na siku 2 baadae

Nakumbuka nilikuwa kwenye daladala nikielekea Mbagala alfajiri ya tarehe 28/8/2002 nilipomsikia Godwin Gondwe akizungumza kwa masikitiko juu ya kifo cha James Dandu. Ilikuwa kama mstuko fulani (hasa kwa wakati huo) kwa kuwa nilikuwa nimesikiliza mahojiano yake siku chache zilizopita akizungumzia mipango yake katika kuuendeleza na kuuthamninisha muziki wa nyumbani.
Kaka Gondwe alieleza sababu ya kifo na hapo nikatambua kuwa mstuko niliokuwa nao watakuwa nao wengi kwani kuna alioagana nao muda mfupi kabla ya ajali hiyo na hawakuweza kumuona akiwa hai tena.
Leo ni miaka 7 na siku 2 mbili tangu James Dandu afariki. Alikuwa mwanamuziki, alikuwa pia ameanzisha (ama kuupa umaarufu) utaratibu wa kuanza kuenzi kazi za wasanii kupitia Tanzania music Awards.
Sina hakika kama watayarishaji wa Tuzo hizi wanaenzi juhudi zake kwa kujitahidi kuzifanya tuzo hizi zienzi sanaa ya kweli ama wanafuata upepo wa mashabiki.
Dandu pia alijitahidi kurejesha nyimbo za kale katika mahadhi ama midundo ya kisasa na pia aliweza kuchanganya Bongo Flava, Dansi na mahadhi ya kikongo kwenye miziki yake.
Katika kumkumbuka, nimeona niweke nyimbo hizi Mamuu (aliourudia na Marehemu Madilu "Multi System) na Kalubandika (ambao ulitolewa na Marquiz du Zaire) ili nawe uweze kuenzi kazi za "James Dandu ama "CJ Massive"
Lakini wacha nikurejeshe kwenye SINA MAKOSA aliyoirudia na Bobo Sukari
RIP JAMES

6 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

"Kolobelaga lukumo lwane. Jaga Ng'wigulya. Jaga Ubagisha shikamoo abakolobela ng'weli..."

Hii ni korasi mashuhuri inayosikika kupitia sauti tamu laini katika nyimbo nyingi za mtoto wa Dandu (anayetaka tafsiri aseme)

Kwingineko mara kwa anasikika...

"Nabiza wa galama. Nulunagaja gubugeni nadiko gwigashiji gogo mpagi sumbi lya nghana..."

Mwenye akijiita Nzokaihenge (nyoka makengeza) alikuwa na kipaji kikubwa cha muziki, na kama walivyosema walimwengu - vizuri havidumu. Basi akiwa angali mbichi vile akavunwa. RIP MTOTO WA DANDU. Daima utaishi kupitia muziki wako!

Yasinta Ngonyani said...

Upumzike kwa amani peponi. Ni kweli utakuwa unakumbukwa daima kupitia miziki yako.

Faith S Hilary said...

"sina makosa, wataka kunia bure...", sikupata kujua muziki wake huyu bwana ila huu ndio wimbo uliokuwa unanichengua na kufanya video na yule "Sinta". Anyway how days pass by, he is RIP.

PASSION4FASHION.TZ said...

Kweli wema hawana maisha,hapo kipaji kilikuwepo,mungu ampumzishe kwa amaani.

Born 2 Suffer said...

Masikini mtoto wa dandu (Sina Makosa)alikuja vizuri na update za nyimbo za zamani lakini mungu akamtaka, pumzika mahali pema amin.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...
This comment has been removed by the author.