Monday, September 14, 2009

Hakuna kibaya kisicho na uzuri...... Yategemea umeachia wapi kuoanisha na tukio

Labda ukiangalia upande wa pili wa mstari huo mweupe utenganishao "malaika" na "shetani" utaona tofauti na upande uliopo.
June 18 niliuliza swali kuwa UBAYA. Hivi una faida? (Bofya hapa kujibu kama hukuiona) na niliuliza maswali kuhusiana na mzunguko mzima wa pesa kwa yale ambayo wengine wanayaona mabaya ilhali wapo wanaonufaika nayo kwa namna isiyosemeka. Wiki kadhaa zilizopita nilikuwa nikiongea na mfanyakazi mwenzangu naye akawa anazungumzia watu walivyo "wabaya" ulimwenguni. Nikamuuliza kama anaamini kuwa kuna ubaya naye bila kusita akasema kuwa UPO. Akasema pia kuna watu wabaya sana ulimwenguni. Nikamuuliza huyo anayeamini kuwa m'baya ni nani na akanipa mfano wa HITLER. Akasema alikuwa mtu m'baya saaana ulimwenguni. Nikamuuliza umri wake na akasema ni miaka 26 kisha nikamuuliza amejuaje ubaya wa Hitler akasema amesoma vitabu, ameona movies zake na kuona documentaries kumhusu. Sikutaka kuingilia propaganda zilizomo kwenye hayo aliyoyataja, ila nikamuuliza kuwa hizo movies na Documentaries zilishirikisha watu wangapi? Akasema weeengi sana. Kisha nikamuuliza ni makala ngapi zimeandikwa kuhusu Hitler akasema nyiingi na zimehusisha uchunguzi uliohusisha watu wengi. Kisha nikamshirikisha kuwaza pamoja nami kuwa Hitler mmoja amewaweka watu wangapi kwenye ajira ya kuigiza tabia zake na kuchunguza maisha yake, kutunza kumbukumbu zake, kuwa wachambuzi wa tabia zake kwenye Tv na hata kueleza katika makumbusho mbalimbali yanayojengwa. Akasema ni wengi. Nikaaga na tukaachana.
Wiki hii nikakutana na mfanyakazi mwingine aliye kitengo tofauti ambaye hatujaonana tangu punguzo la kazi lipite. Tulifurahi kuonana kwani hakuna aliyejua kuwa mwenzake yupo. Akanieleza kuwa ANAMSHUKURU MUNGU KUWA HAKUPATA NAFASI YA PROMOTION ALIYOKUWA ANAITAFUTA KWANI KULE ALIKOTAKA KUHAMIA NDIKO WALIKOPUNGUZA WENGI NA WALIPUNGUZA WASIO NA UZOEFU NA KAMA ANGEHAMIA ANGEKUWA HANA UZOEFU WOWOTE. Hu
Sura yake ya siku hiyo ilikuwa tofauti na ile aliyokuwa nayo aliponiambia kuwa hajapata nafasi aliyokuwa akiiombea. Wakati ule alikuwa na huzuni saana na leo ana furaha. Anashukuru Mungu kuwa hakupata nafasi aliyokuwa akijiuliza kwanini ameikosa. Nikakumbuka sala ya Da Subi kwenye Facebook page yake aliposema "God, Thank you for not answering all of my prayers at times as requested, for I don't know what I would have became had YOU fulfilled some of those stupid requests. Now that I look back at them, I know exactly why you didn't grant them. I realize that, some of YOUR best answers are the un-aswered prayers. Thank YOU!"
Ina maana kama rafiki yangu angechukulia kutopata promotion kama mwisho wa hadithi, basi angesema ana BAHATI MBAYA, lakini kwa kuwa kaunganisha mpaka kilichotokea punde baada ya yeye kukoswakoswa na punguzo la kazi, basi anajiona ana BAHATI NZURI. Na ndio sasa naamini kuwa HAKUNA KIBAYA KISICHO NA UZURI WAKE (kulingana na maslahi ya watendaji) kwani ukiangalia wanaonufaika na kuendesha maisha yao kwa ubaya huo ni wengi pengine kuliko wanaotenda. Umeshajiuliza Vita kama ya Irak itawapa "ajira" watu wangapi? Kuanzia wanaopanga, wanaochimba mafuta kuendesha vita hivyo, makampuni yanayotengeneza ndege, vipuri (spare parts) zake, wanaoendesha mafunzo kwa wapiganaji, wanaosambaza zana za kivita, wanaokwenda kuripoti, wanaoshughulikia kurusha matangazo na wanaofanya propaganda mbalimbali. Ni weeengi zaidi ya wanaoteketea. LAKINI BADO WENGI WA WANAOTEKETEA HAWAKUSTAHILI KUTEKETEA.
Kwani wangapi walipoteza maisha yao kutetea uhuru wa nchi zao? Vifo vyao vilikuwa kitu "kibaya" kwa jamii yao na ndio maana sasa hivi wengi wanafurahia uhuru. Maelfu waliteketea katika majaribio ya matengenezo ya ndege, kazi za umeme, treni, magari na aina mbalimbali za usafiri tunazojivunia leo. Unadhani kwa wale waliokuwa na uhusiano nao wanasemaje? Si majaribio hayo yalikuwa na "ubaya" kwenye familia zao japo leo marekebisho yake ndiyo yakufanyayo uwe salama zaidi? Vipi wanaoendelea "kupigania dunia salama" na kuuawa ili kukulinda wewe? Unadhani wanafanya kazi kwenye mazingira gani? Mabaya. Lakini wakifanikisha lengo lao basi tutakuwa salama. Haya yote ni MAZURI YA MABAYA YALIYOTANGULIA na najisikia mgwadu kusema kuna "uzuri wa ubaya" kwani hiyo itafuta yote uzuri na ubaya na kutufanya tusiwe na uzuri wala ubaya, bali kuwa na kile tunachotaka kuamini kuwa ni kizuri ama kibaya ili kutimiza uhusiano wa yaliyopita na yaliyopo.
Naacha.
Tukutane NEXT IJAYO

7 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

The Way You See The Problem Is The Problem" = KWA HIYO PROBLEM NI WEWE UIONAYE

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli kabisa "hakuna kibaya kisicho na uzuri" Kama ulivyosema huyu rafiki yako wa kwanza kwa vile amesoma vitabu na kusikia tu kuwa Hitler alikuwa mtu mbaya basi naye anaamini bila. Je anajuaje kama yaliyoandikwa na kweli? huyo angekutana nami angetamani dunia ipasuke aingie angepata maswali mengi kweli.Ok naacha!!!

Tandasi said...

ni kweli mzee wa changamoto hoja ni ya kweli sana nakuunga mkono sana na.wasaalam huko ughaibuni.Tuzidi kuwa pamoja . asante kwa support yako

Simon Kitururu said...

Umemaliza MKUU!

Na uwepo wa shetani usifiwe kwa kukumbushia watu kuna MUNGU!AMEN!

Albert Kissima said...

Da! Hii ni zaidi ya kufikiri,wazo zuri sana, kwa hiyo maswala ya -ningelijua, -ningali si tija kabisa, yabidi kuridhika na hali iliyopo.

emu-three said...

Hakuna kizuri kisicho na kasoro na kuna kibaya kisicho na uzuri...mmh mkuu nashukuru sana kwa darasa la leo

sasha said...

nimeipenda hii thanks. Ila najiuliza maswali, kweli ubaya huleta uzuri. Ila tukihalalisha hili tunawapa chance wanaopenda kutumia ubaya kupata mazuri, then tutakuwa tumepukutisha haki za wengi.wasiwasi