Saturday, September 12, 2009

Happy Birthdate Brother Sheme Bandio

Kaka. Ni mwaka mwingine unamalizika na mwingine unaanza maishani mwako. Napenda kukutakia kila lililo jema maishani na napenda utambue kuwa maisha tuliyopo ni maalum na twatakiwa kuyaenzi na kuyathamini. Nafurahi kwa mafanikio uliyofikia katika mwaka mzima huu na sasa ukiwa ndio umeanza maisha ya kazi, nakuombea mafanikio katika kuyapanga na kujiweka katika nafasi njema.

Kumbuka "mkono wa Mungu" katika ajali ambayo ulinusurika bila maumivu makubwa. Ni ishara nyingine kuwa kuna "Mission In Progress" ambayo umebakizwa ili uitimize. Na naamini umeanza na utaendelea kuitimiza. Basi tuendelee kushirikiana huku tukiombeana na kutambua kuwa MAGUMU YA MAISHA TUTAYAPITIA KWA KUWA YAMEWEKWA ILI TUYAPITE, ILA KWA IMANI NA USHIRIKIANO TUTAYAVUKA KUELEKEA ULIPO MUSTAKABALI WETU.
Majira yabadilika, hatuna haja ya kukata tamaa kwani Mungu ndiye muongozaji.
HAPPY BIRTHDATE Brother

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana kaka kwa siku hii maalumu. Nakutakia kila la kheri kwa yote utayofanya. HONGERA.