Tuesday, September 29, 2009

Happy Birthdate Sis Suzzie

Nikiwa na Dadangu Suzzie. Happy Birthdate Dadaa
Siku zinakimbia saana. Ni kama juzi tu tulionana kwa mara ya kwanza na kisha kufanya kazi pamoja. Kama ilivyo kwa wengi, nami nilijifunza mengi toka kwako. Na najivunia mengi niliyoyapata kwa muda tuliofanya kazi wote. Lakini zaidi nashukuru kwa muendeleo wako wa ushauri, mawazo, maoni na mawasiliano hata baada ya mimi kuondoka Bussiness Times.
Basi dadangu napenda kukutakia kila lililo jema katika maisha yako. Salaam kwa Kaka-ndani ya-sheria (brother-in-law) na Uncle wangu hapo.
Endeleza moyo huohuo uliokuwa nao na naamini mafanikio kwako litakuwa ni swali la "lini yatatokea?" na sio "kweli yatatokea?"
Nawapenda, Nawakumbuka na Nawaombea saana
Nakuacha na ujumbe huuu wa "kunyumba" kuwa vyote tufanyavyo tukumbuke kuwa vyafanywa kwa UPENDO. Byooona bikoorw'Engonzi.
Blessings
HAPPY BIRTHDATE SUZZIE

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hongera kwa siku ya kuzaliwa dada Suzzie nakuombea uwe na maisha marefu. Siku njema.

mumyhery said...

Happy birthday Dear Suzzie

Simon Kitururu said...

Umenikwaza kidogo Mkuu na sentensi niinukuuyo:

''Endeleza moyo huohuo uliokuwa nao na naamini mafanikio kwako litakuwa ni swali la "lini yatatokea?" na sio "kweli yatatokea?" '' mwisho wa nukuu!


Mbona nahisi kama kwa Dada Suzzie mafanikio yameshatokea na hata tu kwa kusoma tu ulichoandika hapa kuhusu yeye ingawasimjui? Kama vile kaolewa, anaroho nzuri, n.k....


Happy Birthday Dada Suzzie!

Faith S Hilary said...

1st. Happy BirthDAY to Suzzie, japo hatujuani ila "one love" right?

2nd. Nataka hayo maneno yote kwenye T-Shirt yako maana mwisho naona "DON'T GET TEMP..." Ooh..PLEASE..the magic word...lol

3rd. Umeniua na translation yako ya moja kwa moja, "kaka ndani ya sheria"

Nimemaliza.

Mzee wa Changamoto said...

Asanteni nyote.
Nyie hata nisipowaambia mnajua kuwa NAWAJALI NA KUWAOMBEA PIA.
Lol
Da Fai, Ur best comment ever. Maneno ya kwenye t-shirt yanasema "THEY'RE LOOKING GOOD FROM AFAR, BUT THEY'RE FAR FROM LOOKING GOOD.....DON'T GET TEMPTED"
Wako wengi wa hivyo. Wanasiasa, machangu, wezi, wanafiki, mafisadi ma........ yaani list inakwenda on mpaka off yake inakuwa off.
Endelea kusoma neno baada ya neno. Mstari kwa mstari japo wakati mwingine "J" inapowakilishwa na "K" inakukwaza kwani unaleta maana nyingine. Lol
Unakumbuka post ya UALIMU???
Hahahahaaaaaa
Thanx

Faith S Hilary said...

Aaaaw best comment ever!! I am proud of me lol anyway hayo maneno nimeyafagilia maana they make sense and they are so true!

Hahahahaha na post ya "Ualimu" kwikwikwikwi...I couldn't help it kaka maana nilivyoona tu nikaguna nikasema hapa sinyamazi lol! It was a good one though lol...ila sio vizuri kwamba J iko right next to the K hehe

Mch luv! xx