Thursday, September 3, 2009

Tunajidanganya wenyewe kudhani twawajali wengine

"Forgiveness is almost a selfish act because of its immense benefits to the one who forgives."
Lawana Blackwell, The Dowry of Miss Lydia Clark, 1999

Unapomuangalia yule unayeamini kuwa unampenda saaana unafikiriaje? UNADHANI UNAMPENDA KWA KUWA UNAMPENDA AMA UNAMPENDA KWA KUWA UNAPENDA KUMPENDA?
Kuna ukweli ulioko "nyuma ya pazia la akili zetu" kuwa kila tufanyacho ni kwa manufaa yetu hata pale tuonekanapo ama kujitahidi kujifanya kuamini kuwa ni kwa manufaa ya tumfanyiaye.
Tarehe 20 mwaka jana niliandika swali fupi tu nikuliza kuwa NI KWELI SOTE TU-WABINAFSI? (Bofya hapa kuisoma) na nilibahatika kupata majibu kadhaa.
Lakini mbali na majibu hayo, nimegundua kuwa wengi wetu TWAJIDANGANYA KULIKO TUNAVYOAMINI kwa kudhani kuwa tuko hapa kutenda mema kwa ajili ya fulani. Ukweli wa mambo ni kuwa HAKUNA JAMBO LOLOTE DUNIANI AMBALO ULIFANYA, UNAFANYA NA UNAWEZA KUFANYA NA LISIKUNUFAISHE AMA KUKUFAIDISHA KWA NAMNA YOYOTE. Ninalomaanisha ni kuwa kama itatokea ukapata faida ndooooog kuliko, ni ile ya kujua kuwa "hatimaye nimetekeleza" (wenyewe wanasema At least i did it) achilia mbali suala la kwanini umetekeleza.
Hakuna kisicho na faida maishani mwetu ambacho tunatenda.

Kama kuna ambaye anaamini kuwa alishatenda jambo lolote ambalo halikumnufaisha yeye, basi ajiulize mara mbili na kama hapati jibu la faida basi jiulize kama "uliridhika na yale mema uliyotenda?" Kama uliridhika na wema huo, basi faida yako ni hilo ridhiko.

Ni Changamoto tuuu kuwekana wazi na sawia.

Blessings

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mzee wa Changamoto umesema kweli kwanza JIPENDE MWENYEWE maana usipijipenda mwenyewe unafikiri nani atakupenda wewe. Nimeanza tu kusema na naacha ili wengine wasema labda nitaongezea baadaye.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kijanawa changamoto, nikiamua kusema kwa kirefu juu ya vifupisho hivi vinavyojieleza vyenyewe, basi ntajaza blogu. ilumenena.

umeongelea kupenda na hujagusia huruma kama kuhurumia ni msamaha au?

anyway, umetuonyesha kuwa tunafaida kubwa kwa kila tulifanyalo hata kama hatulipwi. kwa mfano kublogu kwetu faida ni kwetu wenyewe kuliko mwingineyoyete

Simon Kitururu said...

DUH!

Anonymous said...

At the end of the day, I have to live with me :D
Serina.