Thursday, October 1, 2009

Tahadhari toka kwa Dada Subi

JIHADHARI: Wizi wa mtandaoni nao wachukua kasi ya mabadiliko ya teknolojia! Changamoto Yetu imepokea ujumbe huu toka kwa Dada Subi na inapenda kuwashirikisha katika kujihadhari na wizi huu
ASANTE DADA SUBI KWA KUENDELEA KUSHIRIKIANA NASI

Huu ni ujumbe uliotumwa kwangu (soma hapo chini) nami kwa vile nilivyoona maneno kadhaa ya KiSwahili, nikaazimu nisiufutilie mbali bali niusome pengine utakuwa umetoka kwa mtu ninayemfahamu. Baada ya kusoma mistari miwilitu ya mwanzo, nimejikuta naang'ua kicheko na kushangaa sasa kwa jinsi hawa majangili wa mtandaoni walivyoamua kutumia huduma ya Google ya kutafsiri lugha "Google Translate" na kubadili utapeli wao kutoka lugha kanganya ya Kiingereza hadi iliyovunjikavunjika ya Kiswahili ili waweze kuwaibia Waswahili wengi zaidi. Masikini we, laiti wangejua thidanganyiki!.
Subi, nukta77!

---------- Forwarded message ----------
From: <yahoomsn1@centrum.cz>

Date: 2009/10/1
Subject: huu ember kukuza lucky mshindi
To:

Sisi ni radhi kwa taarifa kwamba alishinda una jumla ya kutoka 485,000.00 GBP kutoka Yahoo! MSN (Windows Live) Awards mpango.

PAYMENT wa zawadi na kudai Vinnarna atalipwa kulingana na makazi Center. Tuzo ya Nobel yahoo lazima kutekelezwa no baadaye kuliko 15 siku kuanzia tarehe ya notification Draw. Gharama yoyote alidai kipindi hiki itakuwa waliopotea.

Alisema chini nambari yako ni kitambulisho:
Batch namba: YPA/07-43658
Reference number: 2007234522
PIN: 1206

ushauri wewe kurudi kwetu wasiliana na mtu Shining Rev Dr Robert kulabu kwa madai yake.

Wasiliana akiitwa / madai ya mwakilishi na taarifa zifuatazo.
Jina: Rev Dr Robert kulabu
E-mail: rev.dr.roberthooks@live.com
rev.dr.roberthooks@safat.us
Simu: +447024067872

Sincerely,
Mrs Carol Jones
Tarehe mstari mratibu

1 comment:

Fadhy Mtanga said...

Mi ndo sizoeleki kabisa!