Sunday, November 15, 2009

Manny "Pacman" Pacquio... Mkanda wa 7 katika uzito wa 7 tofauti

AP Photo/Mark J. Terrill
Picha toka HBO.COM
Hili ndilo linalomfanya aitwe MFALME WA POUND-FOR-POUND. Ni kwa kuwa ameweza kubadili uzito anapigana na kufanya vema kote. AMETAWALA kila uzito aendao na usiku wa kuamkia leo, ameweza kuvuka kile kilichokuwa kikionekana kuwa kigingi kikubwa zaidi katika maisha yake ya ndondi pale alipomsimamisha bondia Miguel Cotto wa Puerto Rico kwa TKO katika sekunde ya 55 ya raundi ya 12.
Fuatilia tukio zima katika picha kwa kuBOFYA HAPA, ama kusoma kila kilichotokea katika raundi zote 12 kwa kubofya hapa ama HAPA
Baada ya kumaliza pambano, Manny alifanya mahojiano na ESPN ambayo unaweza kuyaangalia hapa chini
Sasa njia i-wazi kwa m-Fillipino huyo kupambana na Floyd "Money" Mayweather katika kubainisha ni nani aliye "mfalme" wa ndondi ulimwenguni.
Hata hivyo, Manny amekuwa akinukuliwa akisema kuwa Mayweather ameanza kuonesha dalili za kumkacha jambo ambalo anasifika kwa kufanya. Alishagoma kupambana na Cotto mara kadhaa, akagoma kupambana na Antonio Margarito na hata bondia ambaye anabadili uzito ili kutafuta wapinzani Paul Williams.
Kama pambano la Pacquio vs Mayweather litafanyika kama ambavyo wengi tungependa, litampa nafasi Freddie Roach ambaye ni mkufunzi wa Manny kulipiza kisasi kwa Mayweather baada ya kugomewa pambano la marudiano alipokuwa na De La Hoya.

2 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ngumi ndiyo mchezo wangu na Pacman ni kiboko. Wengi hawakufikiri kwamba angeweza "kumdhalilisha" Cotto namna hii. Ngoja tuone kama Floyd "money" Meyweather atakubali kumvaa huyu shujaa wa Kifilipino. Huo utakuwa mpambano wa kufa na kupona.

Simon Kitururu said...

Asante NDONDI kwa kunikumbusha binadamu ni wanyama !

Ngojea nikashangilie vita za kuku na mbwa sasa zipigwazo vita na binadamu.

Baadaye basi WAKUU!