Wednesday, November 18, 2009

Mkutano wa kuanzisha chama kipya cha Waafrika Wakazi wa Marekani

Wapenzi,

Tatakuwa na mkutano wa kubadilishana mawazo kwa hoja ya kuunda chama kipya cha maendeleo ya "WAAFRIKA WAKAZI WA MAREKANI" (jina kamili/halisi litapitishwa na kukubaliwa baadaye katika mkutano mkuu) wanachama wa chama hiki kipya watakuwa ni Watanzania wenye nia ya dhati, Waganda, Wakenya na Waafrika wengine kutoka maeneo yetu ya Afrika Mashariki na Kati na hata maeneo mengine ya Afrika. Na siyo lazima wawe wakazi wa hapa eneo la Washington Metro, bali kote Marekani.

Chama hiki kipya kinalenga kuanzisha chama ambacho kitakuwa na manufaa, faida na maendeleo kwa wanachama wake.

********* Chama hiki kipya hakinuii wala kulenga kuchukuwa nafasi ya Jumuiya ya Watanzania Marekani wala kuingilia kati katika shughuli za Jumuiya hiyo au vyama vingine vyovyote vya kidini, kisiasa, kibiashara au kijamii. *********

Tafadhali fika mkutanoni Jumapili ijayo tusaidiane kubadilishana mawazo na kukiunda chama hiki kipya. Kikao kitaanza kwa sala ambayo itaongozwa na Mchungaji Malekela na Mchungaji Kadyolo saa 7 mchana. Wale ambao hawataweza/hawatapenda kushiriki katika Sala basi wahi mkutano wa kuanzisha chama ambao utaanza mara baada ya sala. Mkutano utaanza saa 8 kamili mchana hapo hapo ukumbini.

Tunawakaribisha wote, Waislamu na Wakristo, Watanzania na wasio Watanzania, katika mkutano huu muhimu.

PAHALA PA MKUTANO:

3621 CAMPUS DRIVE
METHODIST CHURCH
UNIVERSITY OF MARYLAND CAMPUS
COLLEGE PARK, MD 20740

(Down at the Basement)

Jerome D. Kassembe
301 552 9324

5 comments:

Anonymous said...

Nilipenda kumsikiza sana bw. Jerome Danford Kassembe, Sauti ya America.
Siku hizi simsikii sana, namna gani pale?
(Sanmahani kwa kutoka nje ya mada kabisa kabisa)

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Vyama vingi vya aina hii nilivyoviona vinaishia "kutawaliwa" na Wanaijeria, na kusema kweli vinakuwa havina faida yo yote kwa wanachama wengine. Pengine hiki kitakuwa tofauti!

MARKUS MPANGALA said...

Dada Subi hata mie umenikumbusha sijui huyu kiumbe kapotelea wapi nyakati hizi yaani kimyaaaaaaaa, nimebakia kumpenda Mwamoyo Hamza. Na kule Malawi kuna Mtz/Mmalawi Cosmas Cahle redio one, halafu pale redio two yuko rFrank Andowa a.k.a Fraternal Dj yaani we acha tu.

tukirudi katika vyama ni swa ninavyokataa vyama vya wanafunzi wa vyuo vikuu eti waliosoma mkoa fulani, wilaya fulani duh! bora ingekuwa mradi basi kama NYAZODE yetu poa. Lakini kaka Matondo usiogope bwana komaa nao unawamudu wanaija boys/girls

Mzee wa Changamoto said...

We Subi vipi wewe?? Huoni namba hapo upige umuulize? Ama huna long distance??? Lol
Just kidding.
Mzee Jerome Danford Kassembe alishastaafu toka VOA. Alistaafu baada ya aliyekuwa mkuu wa pale Mzee Emmanuel Muganda. Kwa hiyo hawa ndio ma-hall of famer niliokuwa najaribu kuwazungumzia kwenye post niliyoiandika (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/08/ni-lini-tutawaenzi-watu-hawa.html). Watu ambao si tu walimudu kazi zao, lakini wakawa chachu ya wengine kujifunza na kuzifanya.
Kaka Matondo nauona ukweli kwenye hilo usemalo na naamini kwa wale watakaohudhuria wanaweza kuuliza kujua ni namna gani hili linaweza kuepushwa katika CHAMA hiki. Haimaanishi kutokuwa na kiongozi ama viongozi waNaijeria, bali kama ulivyosema "KUTAWALIWA" nao na kutoonesha faida kwa wanachama wengine. Jibu litapatikana pale mwenye hofu atakapowasilisha swali na wenye kuanzisha wakaonesha mikakati thabiti ya kuhakikisha kuna "usawa" katika chama.
Kaka Markus. Kwa sasa Dk Mwamoyo Hamza ndiye mkuu wa Idhaa pale VOA- SWAHILI SERVICE.
Pia kwa wewe Markus naja kwenye inbox yako mkuu. Asante kwa kuwa nasi na shukrani kwa kila jema utendalo
Blessings

Anonymous said...

Senkyu, senkyu Markus wa Mpangala na Baba nanihii aka Mzee wa Chchzzz, nikekusomeni vyema. We mwana wa Mpangala nawe kwa 'data' hujambo, asante kwa kuwataja hao ambao nilikuwa not richabo.

'afu we Mube ww, distance call mwenyewe, watu tunahesabu txt msg we unaleta mambo ya call? kwi kwi kwi iiiii. Asante.