Friday, November 6, 2009

Them, I & Them....FEEL IRIE........Lucky Dube

Ni KAWAIDA kwa binadamu anapopata shida kujiona kama aliyefika mwisho wa maisha, kama aliyeumbuka na kusahauliwa na Mungu, kama asiye na thamani na ambaye haoni pa kwenda. Ni wakati huu huu ambapo BINADAMU husahau uwezo halisi ulio ndani mwake unaomuwezesha kukabiliana na matatizo anayokumbana nayo.
Binadamu wa "kisasa" HAWATAFUTI NGUVU ILIYO NDANI MWAO ambayo inaweza kuwa SULUHISHO HALISI, ASILIA NA NAFUU kwa maisha yao.
Ndio maana mtu akiumwa kichwa (hata kama ni kwa kufikiria sana ama kutopata mapumziko ya kutosha ama kwa kufanya kazi sana) anakimbilia vidonge badala ya kutafuta CHANZO CHA TATIZO. Na kushindwa kwetu kutatua CHANZO CHA TATIZO ni CHANZO CHA MATATIZO MENGINE. Mfano, kuwaza kitu usicho na suluhisho nacho na kuendelea kuumizwa nacho kwaweza kukusababishia msongo wa mawazo (stress), vidonda vya tumbo (Ulcers) na matatizo mengine mengi kama kupungua uzito na kudhoofika kwa ujumla.
Leo hii tunaye Lucky Dube ambaye anaimba akiusiana na mtu ambaye amemkuta akilia kutokana na UGUMU WA MAISHA.
Anaanza kwa kumuuliza muda atakaoendelea KUBEBA mzigo alionao moyoni (ambao ni kama hana suluhisho nao). Anamuuliza ni muda kwa gani ataendelea kulia na kutiririsha machozi? Anamwambia sote tuna matatizo na haijalishi tunajitahidi kiasi gani kuepukana nayo bado yatatufuata. (How long shall you carry that burden on your shoulders? How long shall those tears keep running down your beautiful face? We all have troubles now and again, know what I'm saying? No matter how hard we try, trouble will find us one way or another.)
Na anaendelea na mtindo wake wa kutumia "mifano-hai-mifu" (ambayo ameitumia katika nyimbo nyingi) kumuonesha kuwa si yeye wa kwanza kuwa na matatizo kwani "watu wamekuwa na matatizo tangu Papa akiwa "mtumishi" kanisani, na watu wamekuwa na mashaka tangu ile "bahari mfu" ikiwa mahututi". (People had troubles since the POPE was an altar boy.People had worries from when the Dead Sea was only critical)
Na hiyo yote ni kumdhihirishia azungumzaye naye kuwa MATATIZO SI YAKE PEKEE NA YEYE SI WA KWANZA NA HATAKUWA WA MWISHO.
Na anazidi kumhakikishia kuwa "hakuna binadamu anayeweza kuikimbia hofu ya matatizo kwani ni sehemu ya ukamilifu wa ubinadamu wetu hivyo yatapata namna ya kujidhihirisha maishani mwetu" hivyo si jambo la ajabu kukumbana nayo.
Mwisho anampa suluhisho kuwa ANZA KUTABASAMU NA USIACHE MATATIZO (yaliyo nje ya uwezo wako) YAZUIE UKUAJI WAKO.
Basi tutambue kuwa katika wakati huu wa mkanganyiko wa uchumi na matatizo ya ajira, ndoa, pesa, afya, kazi na mengine mengi, TUNA NAFASI YETU NA NAFASI YA WENZETU. Kwa tunaloweza kuwa na suluhisho HALALI basi tulitafute, na kwa yale ambayo hatuna namna ya kuyabadili, basi tuyaache kwa wenye dhamana huku tukiendelea kuboresha maisha yetu kwa FURAHA ILIYOSALIA kwani ni makwazo, hofu na matatizo ni sehemu ya maisha yetu, tukiyaendekeza hatutaishi vema kwani hayataisha.
Msikilize ukimsoma Lucky katika FEEL IRIE

How long shall you carry that burdain on your shoulders
How long shall those tears keep running down your beautiful face?
We all have troubles now and then, know what i'm saying.
No matter how hard you try trouble will find us one way or the other

People had troubles since the pope was an altharboy,
peolple had worries from when the dead sea was only critical

Hear those drums rollingand listen to those guitarsskanking

CHORUS
Put a smile on your face don't let the troubles get you down..shoop shoop doooo
Let me tell you how it feels ... we feel irie...irie we feel irie.......irie...we feel irie..irie
we feel so irie...irie

Do you feel like we do? (tell me) do you feel like we do? (I say) do you feel like we do?

No man can hide from his fears since they are bother him (?)they always know where to find him.
Come on walk tall and keep your head high. I tell you again and again...

CHORUS


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

3 comments:

Fadhy Mtanga said...

Kaka, nakushukuru sana kwa kibao kama hiki. Kipindi hiki hiki miaka kumi nyuma, rafiki yangu Emanuel Mgina, alipenda kunipa dedication ya wimbo kila anionapo katika lindi la mawazo. Mara zote nilikuwa napata faraja sana.
Leo tena, nimepata faraja kubwa kusikia kibao hiki. I won't let the troubles get me down!
Muziki ni the healing force of the world. Muziku huivuta kumbukumbu.
Muziki ni dawa nzuri kuliko.
Narudia kusema, ahsante sana kaka.

Yasinta Ngonyani said...

Mubelwa! Asante nimejifunza kitu hapa leo. IJUMAA NJEMA NAWE PIA NA FAMILIA YAKO. UBARIKIWE.

mpango mzima said...

KAKA MKUBWA HABARI YAKO NIMEPITA KUKUSALIMU TU KAMA VP ENDELEZA CHANGAMOTO..