Friday, November 13, 2009

Them, I & Them....ONE TIN SOLDIER.....Bushman

TAFAKARI TASWIRA HAPO JUU KABLA HUJASOMA HAPA
Sehemu kubwa ya maisha yetu hutegemea namna tulivyojipanga kuyakabili. Lakini kupanga si rahisi kama hujui undani wa unachotafuta Na ndio maana wapo wanaokosa wanalotafuta kwa kuwa WANAFUATA NJIA ISIYO SAHIHI KATIKA KUTIMIZA MIPANGO YAO.
Nimewahi kuwa na mdahalo na "waamini" wanaoamini kuwa njia ya kubaki mwamini ni kuwatenga na kuwakimbia wasioamini jambo linalonifanya niwaze "Kama Mungu kawapa ukombozi ili wakomboe wasio na ukombozi, ni njia gani wanaoifuata kuusaka ufalme wa mbingu?"
Ninawaona, kuwasoma na kuwasikia wanasiasa wanaoendelea kuamini kuwa VITA ndio njia sahihi ya kusaka amani. Yaani wanajua kuwa kuna AMANI inayohitajika kutafutwa lakini wasilojua ni namna sahihi ya kuifuata amani hiyo.
Labda kwa kuwa ni IJUMAA, turejee kwenye mafunzo yetu ya kimuziki toka kwa wasanii wa Reggae ulimwenguni.
Sina hakika ni wangapi wameshausikia wimbo huu ONE TIN SOLDIER ambao uliimbwa miaka ya 1960 na ambao ni utunzi wao Dennis Lambert na Brian Potter. Kama umeusikia unaweza kuwa umejiuliza maswali mengi kuhusu maana yake. Nimeusikiliza mara kadhaa na kujiuliza kama yaliyoimbwa (ama niseme kutabiriwa) miaka hiyo ndiyo tuyaonayo hivi sasa nchini Tanzania na ulimwenguni kwa ujumla?
Wimbo unazungumzia watu wa "Mlimani" na "Bondeni" ambao kwa pamoja wanajua kuwa kuna "MALI YA THAMANI" iliyozikwa chini ya jiwe mlimani lakini hawajui ni nini. Na kwa kuwa kuna UROHO wa kutopenda kugawana mali hiyo, wale wa "bondeni" wanapoomba kushiriki katika umiliki wanahakikishiwa hilo lakini wanaishia kuuawa wanapokwenda kuiona kama walivyoahidiwa na wa "mlimani". Na baada ya "kuwafyeka" wale wa bondeni, watu wa mlimani wanakwenda kufunua ilipo mali hiyo ili kujimilikisha na wanakuta HAZINA iliyopo inaomba AMANI DUNIANI. Lakini hiyo ni baada ya kuwa wameshatenda mauaji na kuwateketeza wenzao.
Katika kufananisha nielewavyo mimi na "wachambuzi" wengine, nimekutana na mmoja wa walioelezea maana yake akisema na hapa nanukuu kuwa "greed won't get you anywhere and that betraying your friends will ultimately leave you with nothing but loneliness."
Sijui ni lini wenye imani hawa watatambua kuwa KAZI yao katika wokovu ni kusaidia wengine waokoke? Labda wanaisaka Mbingu kwa kujitenga na kazi itakayowapeleka huko. Labda hawakumbuki masomo ya yule aliyezika talanta.
Pia sijui ni lini viongozi wetu watalitambua hili na kuacha "kuwaangamiza" wananchi wakitaka kujilimbikizia mali zisizodumu? Kuishi maisha ya kifahari ilhali wale waliowapa nafasi walizonzo ili wawatumikie wanahangaika kuiona kesho.
Kaka zangu Kaluse na Kamala wameandika na kuzungumzia saana juu ya hili lakini WATAWALA wetu wameamua kufunga macho na kuziba masikio.
Ukiusikiliza na kuusoma unaelewaje? Fuatilia wimbo huu katika toleo hili lililoimbwa kwenye mapigo ya chant naye Bushman.

"Listen people to a story
that was written long ago,
Bout a kingdom on a mountain
and the valley folks below
On the mountain sit a treasure,
buried deep beneath the stone
And the valley people thought
they'd have it for their very own.

Chorus
Go ahead and hate your neighbor,
go ahead and cheat a friend
Do it in the name of heaven,
you'll be justified it in the end
There won't be any trumpets blowing,
On the judgment day
On the bloody morning after,
one tin soldier rides away.

So the people of the valley
sent a message up the hill
Asking for the buried treasure,
tons of gold for which they'd kill
Came an answer from the mountain,
"with our brothers we will share
All the secrets of our mountain,
all the riches buried there."

Now the mountain cried with anger,
"Mount your horses, draw your swords"
And they killed the valley people,
so they won their just rewards
Now they stood beside the treasure,
on the mountain, dark and red
Turned the stone and looked beneath it,
"Peace on earth" that all it said.

Chorus
Go ahead and hate your neighbor,
go ahead and cheat a friend
Do it in the name of heaven,
you'll be justified it in the end
There won't be any trumpets blowing,
On the judgment day
On the bloody morning after,
one tin soldier rides away.".... x2


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

2 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sijui n iseme nini ila kuna wanaodhani miili yao ina thamani kuliko wao wenyewe, kumbe sio. waamini wanaojitanga wakati Mungu hajawatenga watu yaani wote hupokea baraka zake bure kama vile hewa, mwanga, mwili, na hata maji au chakula, wao wanaona wajitenge.
ni muujiza huo ehe?

dina marios said...

asante kaka,nimependa ujumbe wa ubeti wa mwisho wa wimbo huo...kweli kabisa