Monday, November 23, 2009

Za Kale vs Maisha ya Sasa..........MWISHO WA MWEZI

Na hizi ndizo tarehe. Tarehe za UNDUGU KUKUA, tarehe za wengine kuzikimbia nyumba zao (halisi), tarehe za wengine kuvesha vimada, tarehe za kinamama wauza "pampula (pombe za kienyeji) kuona ongezeko la mapato, tarehe za watu kuzhelewa kurejea nyumbani, tarehe za nyimbo kuongezeka uziku toka kwa walevi wanaotoka vilabuni, tarehe za vipigo kuongezeka ndani ya nyumba (kwa kuwa tu fulani kauliza amechelewa wapi), tarehe za wezi kujiajiri zaidi (kwani wanajua mifuko imetuna), tarehe za wengine kuhatarisha maisha ya wengine.
Hivi nimesema kuhusu tarehe za wengi kuambukizwa maradhi (kwa kuwa tu wamelewa na kila aliye mbele yao ni mrembo hata kama kaathirika). Ndio zileee siku ambazo Prof Jay alisema ni "mwendo wa viti virefu jirani na nyama choma na toto mbili tatu ..........hii watu wa pombe wanasema ni kupoteza mawazo ingawa mara nyingi hutokea wakati unazo"
Ni mwisho wa mwezi. Wenye mambo na vijambo. Ambao kila ufikapo basi wengi twajua iwavyo. Ni "mishemishe" kila mahala, kila mtu ni "busy" kwa kwenda mbele na kwa hakika muda unaohitaji umakini kwani watu wanakuwa wanaendeshwa na pesa kuliko akili zao binafsi.

MWISHO WA MWEZI una mambo mengi na kama unashani yalianza sasa hivi, sikiliza Vijana Jazz Band (enzi za kina Hayati Hemedi Maneti na Eddie Sheggy) wanavyokukumbusha tangu enzi hizo jinsi mwisho wa mwezi ulivyokuwa.

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia siku za Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mitandao shirika hapa**

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mwizi wa mwezi una mambo mengi na sasa ndo x-mas inakaribia basi ndo kasheshe kweli.

Albert Kissima said...

Halafu niwanong'oneze, tarehe hizi ndizo zile za wachaga kurejea kutoka kule walikokuwa wanasaka mahela, yani wanakuja tena kuripoti kuwa bado wapo,wanakula Xmas na mwakampya taratibu huku wanafanya "registration" tayari kwa harakati nyingine za mwaka 2010.Wanakusanya fweza kwa mwaka mmoja halafu wanakuja kuzitumia zote kwa siku kumi. "Wawekezaji wazawa pekee nje ya mkoa wa kilimanjaro lkn ndani ya Tz".
Nisiendelee kwa sababu "wanama" wananisoma hapa, namwona Masawe, Nkya, Kissima, Mushi, Ngowi, Temba na.,....