Rais Jakaya M Kikwete
Rais Kikwete na baraza la mawaziri
Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dr Shein na baadhi ya wabunge
Rais Kikwete na baraza la mawaziri
Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dr Shein na baadhi ya wabunge
Juma lililopita nimeandika mengi kuhusu UHURU wa nchi na suala zima la nani wa kulaumiwa katika hali tuliyopo. Kuna mengi ambayo niliuliza na nashukuru kuwa wasomaji na wachangiaji wameendelea kuweka bayana ukweli waaminio. Na kwa asilimia kubwa, yaonesha kuwa TATIZO LIKO NDANI MWETU na sisi ni chanzo kikubwa cha wale watawala tulionao.
Kakangu Kamala aliandika akisema "nadhani tatizo liko kwa wananchi kuliko vingozi kwani viongozi ni sehemu ya wananchi. tutachagua tena kutoka kwa wananchi kuwa viongozi na wanaochagua ni wananchi sio viongozi harafu kikawaida sis sote ni viongozi tatizo tunasubilia kuongozwa badaa ya kujiongoza harafu tumekuwa wapigadomo wa kutafua mtwishwa lawama badala ya kucheza naasi yetu.
naamini tukiamua sisi wenyewe hata sisi bloggers tunaweza kubadilisha hali na kuleta ahueni pahala na kubadilisha mambo na kufanya jambo jipya tunalolihitaji badala ya kuwa lalamikia watu fulani"
Hili lilinifanya nirejee kwenye maoni ya Prof Mbele ambaye sehemu ya maoni yake ilisema "Watawala wetu wana matatizo makubwa. Ni kweli. Lakini sisi wenyewe ni sehemu ya tatizo. Na tatizo letu jingine ni kuwa tunatafuta mchawi, yaani serikali, hata pale ambapo wachawi ni sisi wenyewe wananchi.
Miaka 48 ya Uhuru imepita, lakini vichwani mwetu wananchi na vichwani mwa viongozi wetu, Uhuru huo haujaingia."
JE!!!!! Tunajiona tuna nafasi gani ya kutekeleza mafanikio ama kubeba lawama ya lile linaloendelea nchini mwetu?
Ni kweli twatambua kuwa VIONGOZI TULIONAO WALIKUWA WANANCHI KABLA HAWAJAWA VIONGOZI?
Ni kweli twakumbuka kuwa TABIA MBAYA walizonazo viongozi wetu (rushwa, ufisadi, kutojali wananchi, kujilimbikizia mali nk) ni tabia wanazojifunza na kuziona wakiwa WANANCHI KABLA HAWAJAWA VIONGOZI?
Labda la kukumbuka ni kuwa, KABLA YA KUWA WAO (VIONGOZI), WANAKUWA SISI (WANANCHI) HIVYO NI WAJIBU WA KUIBADILI JAMII ILI KUWEZA KUBADILI UONGOZI
Blessings

3 comments:
Baba wa taifa la India, Mahtma Ghandhi alipata kusema, "you must be the changes you wish to see in the world." Hivyo sisi ndiyo tunaopaswa kuwa mabadiliko ambayo tungependa kuyaona. Tuutumie vema uwezo na nafasi yetu. Bila hivyo, tutalalama sana huku tukibaki pale pale.
Na maamuzi sahihi yaanze kwa kura zetu.
nimeona mengi kwa kuchunguza. vijana walioko vyuoni wanailalamikia serikali na kuona kila uoza harafu baadaye wanaingia serikalini nakuwalalamikia wanaoilalamikia serikali.
kwa mfano kuna yule mwandishi wa rais Salva Rweyemamu, alikuwa mkosoaji mkuu wa serikali na upuuzi kibao, baada ya kupewa nafasi ikulu akawa wa kwanza kuyafungia magazeti yenye mitizamo kama aliyoyaandikia yeye (Mwanahalisi) kwa hiyo wale wanaoilalamikia serikali wanawaonea wivu na wale walioko serikalini wanafurahia ulaji. ndio maana wanasiasa wetu hushukuru baada yakuchaguliwa badala ya kutafakari kazi ngumu baada yakuchaguliwa.
au ndio maana watu huonga ili wachaguliwe nawengine huongwa. tatizo ni refu. ndio maana tukienda vijijini hujitenga na jamii ile hatusaidii kufanya lolote.
nilikuwa kijijini kwetu, pitapita yangu unakuta watu wamejenga majumba makubwa yakifahali na ya gharama kuubwa vijijini, harafu wanaendaga mara moja tu kwa mwaka au mara moja kwa miaka miwili na kukaa siku mbili au wakati mwingine hulala hotelini mijini. kajenga nyumba ya gharama na anatumia gharama kuitunza harafu hainafaida, jirani wanakaa kwenye mbavu za mbwa harafu shule aliyoisomea haiana madawati, majengo ya udongo.
yaani badala ya kujenga nyumba yakawaida tu napesa nyingine tuipeleke kujenga shule, zahanati au huduma nyingine za jamii, tunajijengea nyumba tusizohitaji.
tukienda vijijini tunanunua pombe na kulewesha watu badala ya kuchangia vitu vya msingi. Harusi, natarajia kufunga yangu naninaonekana kichaa na chizi kwa kukwepa kuchangiwa mamilioni. tunachangia maharusi huku tukiwa na bara bara mbovu, mitaro mibovu nk, nk
hatutaki kurudi vijijini kusaidiana na kuelmisha na wananchi, sisi ni wakazi wa tauni na kazi kuubwa ni starehe.
kama tunataka mapinduzi tuanze na yale ya kifikra. namshukulu sana Munga tehenan kwa kujitolea kunipa maarifa ya utambuzi. ni maarifa ya gharama sana nchini marekani na masikini hawezi yapata kwani bei iko juu. Munga aliyatafuta kwa gharama na kuyapata kwa shida ila akatugawia bure na kutubadilisha, aliona fedha haina maana sana. huo ndio mfano wa kuigwa wa kubadili jamii na sio kusubili tupate nafasi za uongozi wakati sisi tayari ni viongozi
naishia hapa ila mimi, wewe, yule tuanze leo kujirekebisha sisi na wengine watarekebika tu "change yourself so that you can change the world"... Sant baljit Singh
Kamala,umenipa pointi.
Post a Comment