Lakini kabla hajawa nusu ya alivyo sasa ili kuungana na nusu nyingine kuwa kitu kimoja, napenda kumzungumzia Kamala huyu wa sasa anapoelekea "countdown" ya ndoa yake
Labda ukitaka kumjua zaidi waweza kuSOMA HISTORIA YAKE na naamini hilo laweza kukusaidia kujua ni kwanini yuko alivyo ama kwanini anena anenavyo. Lakini hakuna ubishi kuwa kuna mengi mema ya kuangalia, kusoma na kujifunza kuhusu Kamala.
Kaka huyu amekuwa mstari wa mbele katika kutetea watoto na mara kadhaa amekuwa wazi kusema anavyowapenda watoto .
Na amekuwa wazi kuwa ana mapenzi na watoto kutokana na historia ya maisha yake. Kwa waliyoisoma wanaweza KUSIKITIKA kwa maisha ya utoto aliyopitia lakini bado naendelea kuamini kuwa alipewa hayo kwa kuwa Mungu alijua kuwa ataweza kuhimili na kuinuka na kisha kuwa USHUHUDA KWA WENGI. Twaambiwa "JAH WILL NEVER GIVE US MORE THAN WE CAN BEAR". Namna ambavyo Kaka Kamala ameweza kubadili huzuni kuwa ushuhuda ndicho kitu kikubwa ninachojivunia kwake. Kamala ameweza kugeuza kilio cha wengi kuwa faraja kwa wengi. Ameonesha njia kwa maisha aliyopitia na sasa amekuwa kama mtetezi na mwelimishaji kwa jamii. Nilipokutana na Kamala Dec '07.
"Kapera" huyu anayeelekea kumaliza kipindi chake cha u-moja, anapenda saana kuzungumza kile aaminicho. Na aaminicho husemwa kwa kujali zaidi mantiki kuliko "urembo" wa kisemwacho. Wanaopata tabu na maoni yake ni wale wasiomfahamu. Binafsi nilibahatika kumuona, kumsikia na kuongea naye japo kwa ufupi. Kama ilivyo kwa wengi, Kamala huandika kama anavyoongea na kama hujui ama huwezi ku-imagine uoneaji wake, lazima utapata taabu kutafsiri. Lakini dawa ni kufanya nilivyowahi kusema kuwa jikite kwenye "point of view" ya maoni yake kuliko "tone" ya maandishi yake.
"Kapera" huyu anayeelekea kumaliza kipindi chake cha u-moja, anapenda saana kuzungumza kile aaminicho. Na aaminicho husemwa kwa kujali zaidi mantiki kuliko "urembo" wa kisemwacho. Wanaopata tabu na maoni yake ni wale wasiomfahamu. Binafsi nilibahatika kumuona, kumsikia na kuongea naye japo kwa ufupi. Kama ilivyo kwa wengi, Kamala huandika kama anavyoongea na kama hujui ama huwezi ku-imagine uoneaji wake, lazima utapata taabu kutafsiri. Lakini dawa ni kufanya nilivyowahi kusema kuwa jikite kwenye "point of view" ya maoni yake kuliko "tone" ya maandishi yake.
Na sasa Kakangu huyu anaelekea kuwa Mume na twataraji awe Baba. Well!! Kuwa Mume na U-baba vyaja na vyeo vingine lukuki kama ushemeji, ujomba na menginenyo mengi. Na najua kuwa kwa kutumia uzoefu wa maisha alioshirikiana nasi hapa na kwenye vibaraza vyetu mbalimbali, kuna mengi ambayo JAMII inaelekea kupata toka katika FAMILIA hii mpya.
Na ndio maana nimeona leo ni vema nikaandika namna nijivuniavyo kuhusu Kamala. Kutoka mabadiliko ya malezi yake mpaka alivyoyabadili na kukua kwa mtazamo chanya na sasa anapoelekea kwenye mapenzi yanayotegemewa kuleta malezi kwa jamii nyingine.
Kila la kheri kwa Kaka Kamala na familia-tarajiwa nziiima na nawatakia kila lililo jema katika yale mema mtendayo.
Blessings
8 comments:
namtakia kila la heri na fanaka katika maisha yake hayo mapya ya ndoa, mungu amjazie hekima, busara, faraja na uvumilivu katika maisha hayo mapya.
Blessings
Kaka Kamala nakutakia kila lenye kheri katika maisha hayo mapya. Mungu awazidishie mshikamano , amani, upendo na furaha daima.
Kila la heri kaka.
Kila la heri Kamala.
Kila la kheri Komandoo Kamala.
Nakutakia kila la kheri katika maisha haya mapya ya ndoa. Nawatakia furaha katika ndoa yenu.Upendo daima. Mungu awabariki.
Nami nimo. Kaka Kamala, nakutakia kheri zote katika kuanza maisha mapya. Mungu akuongoze daima.
nimshukuru mzee wa changamoto n wachangiaji wote. it is realy encouraging and xpressin much love.
thanx
Your blog keeps getting better and better! Your older articles are not as good as newer ones you have a lot more creativity and originality now keep it up!
Post a Comment