Saturday, January 23, 2010

Ama kweli dunia ina yake

Image from Health Initiatives for the Private Sector (HIPS),
Nianze kwa habari hii niliyoinyaka kwenye WAVUTI ya Dada Subi kuhusu hawa waTanzania waathirika wa virusi vya UKIMWI wanaopewa dawa za kuongeza / kurefusha maisha / kukata makali ya maradhi yaambatanayo na upungufu wa kinga mwilini lakini wao wanachofanya ni kuziuza kwa waganga wa kienyeji na wafugaji. Dada Subi ameendelea kuandika "Watu hawa wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI (VVU) wanaopewa dawa hizi ili ziweze kupambana na virusi waliopo katika miili yao, wao huzigeuza mtaji wa biashara na kuziuza kwa Waganga wa jadi na mitishamba. Hao nao huzifungua na kuchukua unga wake na kuwauzia watu huku wakijitapa na kujisifu kuwa nao wanaweza kutibu UKIMWI.
Vile vile dawa hizo hununuliwa na wafugaji ambao wao huwachanganyia wanyama katika lishe yao wakidai wanyama 'hunenepa haraka' na kukua chap chap tayari kwa biashara."

Hapa swali laja kuwa wanapofanya haya huwa WANAWAZA NINI? Kwanini waendekeze pesa ya siku chache na kupunguza uwezekano wa siku zijazo? Wamekata tamaa ama hawajui maana na faida za dawa? Wanaelimishwa vya kutosha kuhusu umuhimu wa dawa hizo?
Dada Subi (ambaye ni mtabibu) ameliangalia hili kwa JICHO LA NDANI na kueleza kuwa "Suala hili naona kwa kiasi na kiwango kikubwa kuwa linachangiwa sana na elimu ndogo na upeo wa ufahamu kuwa finyu. Mtu asiyekuwa na elimu ya kuweza kupambanua jambo, hata mhudumu wa Afya akitoa elimu husika kiasi gani, ikiwa hakuna namna ya ziada na ya kipekee ya kumsaidia mtumiaji kuelewa umuhimu wa dawa hizi, ni kazi bure! Mafunzo yataingilia sikio moja na kutokea jingine. Mtu kama huyu anataka kuganga njaa na mahitaji mengine muhimu kama vile mavazi, malazi nk., na sasa ukichangia kuwa dawa hizi za ARV zina maudhi madogomadogo kwa watumiaji, basi inakuwepo ongezeko ya sababu nyingine ya kwa nini mtu huyu aone ni sawa tu kuuza dawa hizi, kisha apate hela akafanyie mambo mengine anayoyajua yeye.
Vyakula tunavyokula...
TAFAKARI!"

Hii hapa chini ndipo chanzo alichopata habari ambayo unaweza kuisoma yote jamvini mwake HAPA. Bofya kitufe cha play kusikiliza

Hivi ukiwa mzazi kisha mwanao akakua na kukuliza kwanini yeye na pacha mwenzake wana miaka tofauti ya kuzaliwa UTAWAZA NINI? Inaweza kuwa rahisi akishakua, lakini wakati wa utoto ni ngumu kiasi. Hiki ndicho wanachojiandaa kukumbana nacho wazazi hawa ambao wamebahatika kupata mapacha wakiwa salama salimini lakini wanatofautiana miaka (japo miaka hiyo ni uhalisia wa masaa)
Ni uzazi ulioanza mwaka 2009 na kumalizika 2010 hivyo mama huyu kuweza kuwa mama wa mwisho kujifungua mwaka 2009 na wa kwanza kujifungua mwaka 2010 katika hospitali hiyo.

Huko Detroit Michigan, mzee mmoja ambaye alionekana kukerwa na biashara ya UKAHABA aliamua kutumia "akili" na kujifanya Polisi ili kuwatawanya waliokuwa wakijiandaa kufanya biashara hiyo. Lakini ambayo hakujua ni kuwa katika hao waliokuwepo siku hiyo ni maskari kanzu ambao walikuwa na nia ya kuwakamata wote waliokuwa wakihusika siku hiyo. Kwa kujifanya askari na kuwatawanya wahusika hao, alisababisha Polisi kushindwa kufanikisha azma yao hiyo na hivyo yeye kujikuta anakwenda jela badala ya wale waliokuwa wametegwa.
Waweza kuSOMA HABARI KAMILI HAPA
Huko Haiti wakati ambako watu wanasubiri kuokolewa, kijana huyu aitwaye Kiki aliweza kufikiwa na waokoaji baada ya kufukiwa na kifusikwa zaidi ya siku 7 lakini alipofikiwa alikuwa na uoga kiasi kwamba aligoma kutoka. Waokoaji walilazimika kumuita nduguye (ambaye naye aliokolewa nao) ili aongee naye aweze kutoka alipokuwa. ALIWAZA NINI?
Tazama video hapa chini


***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya "UJINGA" na kujikuta wakiingia matatani ama ambao wanafanya yanayoishangaza jamii. Wale watendao ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

2 comments:

Simon Kitururu said...

``Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya "UJINGA" na kujikuta wakiingia matatani ama ambao wanafanya yanayoishangaza jamii. Wale watendao ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI?´´


Chakujiuliza ni: UJINGA NI NINI?

Kiishangazacho Jamii ni lazima ni kweli kinashangaza?

Waingiao MATATANI hivi sio kawaida kwa binadamu?

Matata ni nini?


Kushangaa wengine wanawaza nini ni kitendo cha kufikiria mawazo ya wengine yanaupungufu au kitendo cha kusherehekea kuwa kama binadamu waendelee kuwa Binadamu ni lazima wengine wafikirie vingine?


Najiuliza tu MIE MWENYEWE katika kuendelea kujipa CHANGAMOTO.:-(

chib said...

Mimi bado ninawashangaa wale wanaouza dawa za kupunguza makali ya ukimwi!!!!!