Tuesday, January 5, 2010

Happy Birthdate Dad

Baba na wanawe wa kiume. Lol
Leo ni siku muhimu saana familiani mwetu kwani NGUZO MUHIMU katika familia inazidi kuimarika. Ni siku ya kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Baba yetu mpendwa. Naamini nilishaeleza namna ambavyo Babangu amekuwa amekuwa na VYEO zaidi ya UZAZI kwangu. Na ninavyozidi kukua na kuchukua majukumu ya uzazi, nazidi kutambua uwezo mkubwa wa fikra na upendo aliokuwa nao na ambao anaendelea kuwa nao kwetu. Najifunza kuwa kuna mengi ambayo niliyachukulia kimzaha na sasa natazama nyuma na kuona namna ambavyo TUMEBARIKIWA KUWA NA BABA KAMA YEYE.
Baba, wakati unasherehekea siku yako ya kuzaliwa, napenda utambue kuwa ULIWEKEZA MEEENGI MEMA KWETU na sasa tunaendelea kuvuna. Tunajifunza kutokana na maisha uliyotufunza na tunaendelea kuwafunza wengine. Kuwa na Baba kama wewe ni faraja na hakuna siku nitawaza kuwa na baba tofauti nawe.
TWAKUPENDA na TWAKUOMBEA
Happy Birthdate Dad

Dadangu Yasinya wa Blogu ya MAISHA naye anakumbuka siku yake ya kuzaliwa na sina ninaloweza kukuombea zaidi ya MAISHA MEMA NA MAFANIKIO
Happy Birthadate Da Yasinta

Naye Kaka Haki Ngowi wa blogu ya Blogu ya Food For Thought anatimiza miaka kadhaa siku ya leo. Huyu ni kati ya watu wa mwanzo ku-post mabandiko yangu kwao kabla hawajanishauri kufungua kibaraza changu hiki cha Changamoto Yetu. Heshima kwako Kaka na nakutakia mafanikio na kila lililo jema. Happy Birthday Kaka Haki
HAPPY BIRTHDATE TO YOU ALL

13 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nikiona watu tunakumbuka siku za kuzaliwa huwa nabakia na lundo la maswali juu yamaisha yetu haya ya mwili ya kukimbiza kilicho mbali nasi na kuendelea kug'ang'angia tulichonacho ambacho hatukihitaji tukaacha kabisa kuishi ;sasa; ambayo kimsingi ndiyo tunayohitaji.

ukijiuliza maisha yetu yana changamoto sana wakuu\\

hongereni kwa siku hizi

EDNA said...

happy birthday to you all.
Mungu awape miaka mingi zaidi.

Yasinta Ngonyani said...

Hongera baba wa Changamoto na pia kwa sisi wote tunaotimiza miaka leo.

Simon said...

happy birthday!

chib said...

Mimi nasema ninawatakia kila la heri ili mwakani tusheherekee tena siku zao za kuzaliwa

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Nyote mbarikiwe. Happy Birthday!

malkiory said...

Kila la kheri katika kusherekea siku hii muhimu.

Christian Bwaya said...

Hongera sana kwa kukumbuka siku za kuzaliwa kwa wapendwa hawa. Tunawakia wote maisha marefu na yenye mafanikio tele.

Mija Shija Sayi said...

Happy birthdate wote kwa mpigo.

**Huu msamiati wa Birthdate nimeupenda sana.

Stay blessed all.

Faith S Hilary said...

siku ina birthday za watu wakubwa wakubwa tu! lol joking! Happy Birthday to every one of them!

Anonymous said...

Hakuna haja ya kufanya DNA. Mzee mzima aliwaprodusi wote....Happy birthday!

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

hongereni nyote

mumyhery said...

Hongereni sana Happy birthday kwenu nyote, nawatakia kila heri afya tele na mafanikio zaidi