Wednesday, January 6, 2010

JICHO LA NDANI........Kipengele kipya

Picha kwa hisani ya http://web1.d25.k12.id.us/
Ninaandika kwa mara ya tena nikijivunia tena kuwa nanyi tena kama wanajamii. Jamii ambayo licha ya umbali na kutenganishwa na maji na ardhi, bado tumebaki kuwa wamoja na tunaendelea kuusaka UMOJA ULIO NA NGUVU YA KUIKOMBOA JAMII YETU.
Nawazungumzia ndugu zangu Bloggers ambao kila kukicha twashirikiana na kuhabarishana kuhusu maendeleo katika "vibaraza" vyetu.
Nashukuru kwa UTAYARI wenu wa kutumia makala na maandishi na mawazo yenu katika kufanikisha hili. Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikipata ruhusa kutumia maandishi, taswira, mawazo na hata "style" za wenzangu ili kuendeleza UBINAFSI wa blogu hii kuandika ambayo wengine wamewekeza hapa. Nawashukuru saaana.
Nakumbuka kuomba taswira ama Video ama maoni ama kurejea makala toka kwa wenzangu karibu wote nilionao kwenye list na ambao huwa nawatembelea mara kwa mara. Labda inayokumbukwa zaidi ni makala niliyoandika mwezi wa sita ambayo niliomba style ya Mtaka"tifu" Simon Kitururu iliyosema Kama hauko juu ya juu, basi shuka chini uwe juu (Isome hapa)
Na sasa nafarijika kupata IDHINI ya Da Mija kuweza kutumia neno hili alilolitoa kama "kauli mbiu" yake ya kuutazama mwaka 2010 kwa jicho la ndani.
Kipengele hiki kitajitahidi kujikita kwenye kuangalia mambo kwa jicho la suluhisho zaidi na pia kufunua yale macho ambayo KWA MAKUSUDI AMA BAHATI MBAYA yamekuwa yakiangalia vitu kwa jicho lisilo sahihi.
Karibu tushirikiane.
Blessings

2 comments:

nyahbingi worrior. said...

amani mkuu,lakini bado sijafikiana nawe au bloggers kuhusu hili neno MTAKATIFU.

kAMA ULIVOSEMA jicho la ndani pia nani naliangalia hili jina MTAKATIFU kwa jicho la ndani zaidi na kujiuliza kwanini Simon kaamuwa kujiita au kuitwa MTAKATIFU?

Pili katika jicho la ndani nitamulika kwa uwezo wangu wote kuhusu JUMUWATA(JUMUIYA YA WANABLOGU TANZANIA.

Mija Shija Sayi said...

Tunakisubiri kwa hamu kipengele hiki kaka.