Friday, January 29, 2010

MWALIKO RASMI KWENYE HAFLA YA UMODOTZ.BLOGSPOT.COM


TAARIFA NA MWALIKO RASMI KWENYE HAFLA YA UMODOTZ.BLOGSPOT.COM, SHEAR ILLUSIONS, TRUWORTHS na GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL

Siku: Jumamosi 30 Januari 2010
Mahala: Giraffe Ocean View Hotel
Muda: 11 jioni hadi 2 usiku
Hakuna kiingilio. Vinywaji na chakula kuuzwa.

Blogu ya www.umodotz.blogspot.com inawakaribisha wapenzi wote wa maswala ya mitindo, urembo na mavazi kwenye onyesho la wazi siku ya Jumamosi, Tarehe 30 Januari 2010 pale Giraffe Ocean View Hotel. Hafla hiyo imeandaliwa na umodotz blog kwa udhamini wa SHEAR ILLUSIONS, TRUWORTHS na GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL.
Hafla itaanza saa 12 jioni na kuisha saa 2 usiku.

Dhumuni kuu la hafla hiyo ni kuukaribisha rasmi mwaka 2010 kibiashara. Kuwatakia kheri wateja, marafiki, na washirika wa blogu pamoja na wadhamini kwa kuonyesha bidhaa mpya na huduma zao. Onyesho ni la wazi, hakuna kiingilio.

Watakaofika wataburudishwa na onyesho kali la mavazi ambalo litafanywa na mamodo 12 wa blog ya Umodotz. Watapita kwenye mavazi ya mbunifu mzoefu KEMMI KALIKAWE wa Naledi Fashions pamoja na mbunifu chipukizi MGESI. Nguo zote zitauzwa papohapo kwa watakaozipenda. Mamodo wamepambwa kichwani na nywele za Shear Illusions kwa mitindo tofauti iliyobuniwa na wataalamu wa urembo kutoka Paradise Uni-sex Salon (www.paradisespalon.cotz)

Shear Illusions itatoa mkataba mnono na wa kihistoria kwenye medani ya mitindo Tanzania kwa mmoja kati ya mamodo 12 wa blog ya Umodo. Mkataba huo ni wa mwaka mzima! Bila shaka utampa modo fursa nyingi za kufahamika kutokana na picha katika jarida la Shear na bango za matangazo.
Mkataba utaenda kwa msichana ambaye ataonyesha ana uwezo mkubwa wa kuwa modo wa kipekee siku hiyo.

Hili sio shindano. Mamodo 12 wa Umodo walipatikana kwa mchakato wa muda mrefu wa kuwachujwa na kuchaguliwa mmoja mmoja hadi kufikia 12.
Blog ya Umodo ilipata ushauri wa watu mbalimbali kama Steven Kanumba(filamu), Slyvia Shao(Urembo) na mbunifu Kemmi Kalikawe (mitindo) ambao wanawakilisha nyanja mbalimbali zinazoshabiiana na maswala ya mitindo.

Umodotz.blogspot.com inawakaribisha wote. Tunatumaini kuwaona mamodo wengi, wabunifu tele, wapenda mitindo, urembo na mavazi, watu maarufu katika nyanja mbalimbali, wafanya biashara, viongozi, watangazaji, waandishi, vijana na watu wazima. Hii ni nafasi nzuri kufahamiana katika jitihada za kukuza fani ya Mitindo Tanzania.
Taji


OFFICIAL ANNOUNCEMENT AND OPEN INVITATION TO THE UMODOTZ.BLOGSPOT.COM, SHEAR ILLUSIONS, TRUWORTHS and GIRAFFE OCEANVIEW HOTEL FASHION SHOWCASE.

DAY: Saturday 30th January 2010
VENUE: Giraffe Ocean View Hotel
TIME: 5PM-8PM
This is an open invitation event. Drinks and food will be on sale.

www.umodotz.blogspot.com is extending a warm welcome to all fashion and beauty aficionados to a unique event on Saturday the 30th January, at the Giraffe Ocean View Hotel from 6-8pm. The Showcase event has been organized by Umodotz blog with the kind sponsorship of SHEAR ILLUSIONS, TRUWORTHS and GIRAFFE OCEAN VIEW HOTEL.

This event is an opportunity to strengthen business and collaborative ties by ushering in the New Year with clients, customers, models, designers, stakeholders, fans and the general public. On display will be new products and services of the sponsors. The event is open to everyone.

Followers of umodotz.blogspot.com will get a chance to finally see all the 12 beautiful and unique “Uniq Modoz” finally take to stage dressed in fresh khanga cuts by KEMMI KALIKAWE of the acclaimed Naledi Designs. You will be introduced to Mgesi, an upcoming female designer who will certainly steal the lime light with her chic beach styles and casual wear!
Truworths will showcase their exquisite New Year collections while Shear Illusions will supply classy wigs and quality hair extensions to the models including make- up and accessories done by the talented folks at the Paradise Uni-sex Salon (www.paradisespalon.co.tz)!

The highlight of the event will be the awarding of a historic and lucrative contract to one of the 12 Uniq Modoz by Shear illusions. The 12 lucky girls were selected through a rigorous consultative process assisted by Steven Kanumba (Film), Sylvia Shao (Pageantry) and Kemmi Kalikawe who represented designers. Blogger, sponsor and organizer comments and opinions will go towards finally selecting a single girl; who shows unique potential to be an outstanding model, for the contract.
This is not a competition. It symbolizes the way the industry operates. It is expected that other stakeholders will follow the same example.

Come along, bring a friend! We look forward to milling with models, film stars, musicians, designers, business people, marketers, the media and fabulous YOU! This is a perfect venue for making business contacts, forging partnerships all in the name of advancing the fast growing fashion industry in Tanzania!
Taji

Kwa niaba ya Blogu ya Changamoto Yetu, napenda kukupongeza Kaka Taji kwa juhudi zako na pia kukutakia kila la kheri katika kila jema utendalo
Baraka kwako

No comments: