Tuesday, February 2, 2010

AJALI NYINGINE TANZANIA

22 wafariki, zaidi ya 37 wajeruhiwa.
Hii nimeisikia katika usikilizaji wangu wa kila siku wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika. Kwa mujibu wa Habari hiyo iliyochapwa kwenye mtandao wao, "Ajali hiyo ilihusisha mabasi mawili kati ya basi la Mzuri lililokuwa linatokea mkoa wa Dar-Es-Salaam kuelekea Mombo, Korogwe, Hedaru mpaka maeneo ya Mazinde na basi lingine la Chatco likitokea Moshi-Arusha kuelekea Dae-Es-Salaam".
Soma habari kamili na kusikiliza matangazo yao HAPA.
NIMESHAANDIKA SAANA KUHUSU MAISHA YA WATU YANAYOPOTEA KWENYE AJALI KAMA HIZI NA HATUA AMBAZO HAZIONEKANI KULETA MAFANIKIO.
NANI ANAYEONA NA KUHISI MAUMIVU YA WAHANGA? NI NANI ANAYEWACHUKULIA HAWA KAMA WATU WANAOPOTEZA MAISHA NA SI TAKWIMU?

Mungu Ibariki Tanzania

No comments: