Monday, March 22, 2010

Mkaribishe Denzel Musumba ndani ya Blog Radio Talk

Denzel alipokuwa ndani ya Radio Umoja
Akiwa na askari wa Reggae LUCIANO baada ya mahojiano yake Radio Simba Fm
Jana wakati nasikiliza kipindi cha Jarida la Jumapili toka Idhaa ya Kiswahili ya VOICE OF AMERICA, nikasikia mahojiano kati ya Dada Esther Githui-Ewart na Denzel Musumba. Kijana ambaye anatumia huduma ya Blog Talk Radio kuendesha radio yake iitwayo East African Radio.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kusikia kuhusu huduma hii na kisha nikajitoma huko kujua hili na lile juu yake. Kisha nikaungana naye na kumsikiliza alipokuwa "live" kwa masaa matatu.
Kwa hakika nilivutiwa na kazi yake. Ilikuwa Jumapili hivyo alitenga muda maalum wa nyimbo za dini na kisha akaendelea na burudani ya muziki mchanganyiko toka nchi zote zizungumzazo kiswahili. Uwiano wa muziki ulikuwa mzuri.
Na kisha likaja jingine la kupiga simu na kushiriki mada ambayo ilikuwa "Nini kikukeracho zaidi". Na hapo nikashangazwa na idadi ya watu toka nchi mbalimbali zizungumzazo kiswahili walio nchi mbalimbali ambao walichangia na kutuma salaam.
Nikashawishika kumpigia simu kujua hili na lile kuhusu redio yake na ndipo aliponiambia kuwa ni redio changa kwa wale wazungumzao Kiswahili na imekuwa ikijiongezea wasikilizaji kila uchao na licha ya kuwa na "umri" wa miezi miwili tu,imekuwa ikijipatia wasikilizaji mpaka 1000 kwa siku. Denzel ana uzoefu wa utangazaji tangu 2005 na amefanya kazi kwenye vituo vya West Fm nchini Kenya, Rock Fm huko Uganda,Radio Simba na kisha Radio Umoja huko Kenya
Waweza kusikiliza matangazo yake ya moja kwa moja na yale yaliyopita kwa kutembelea mtandao wake HAPA
BLESSINGS

2 comments:

Mija Shija Sayi said...

Ubarikiwe Denzel kazi nzuri sana.

Faith S Hilary said...

I love your mbwembwe :-D