Tuesday, April 20, 2010

Chemsha Bongo na RUSHWA ya Tanzania

Kila ninaposikia "mheshimiwa mtarajiwa" anaeleza namna atakavyopambana na RUSHWA nchini Tanzania, nasikia wakipanga kuendesha vita wakiingia madarakani.
Na kwa walio wengi nchini Tanzania, "hawamtupi" mtu awapae rushwa kupata nafasi ya uongozi.
Sasa kama kupinga rushwa ni mpaka wawe kwenye madaraka na kama bila kutoa rushwa hawawezi kuwa kwenye madaraka, ina maana bila rushwa hawataweza kupinga rushwa.
Ina maana watatakiwa watoe rushwa ili waweze kupata nafasi za kupiga vita rushwa (ambayo inawaweka kwenye nafasi nzuri ya kupokea rushwa nono zaidi)
Swali ni kuwa, WATAPINGAJE RUSHWA IKIWA NI LAZIMA WAITUMIE KUFIKA NAFASI ZA KUIPINGA?

4 comments:

Albert Kissima said...

Mimi nadhani ijulikane wazi tu kuwa serikali ya Tanzania ni sehemu ya watu wachache kujineemesha kwa kufaidi mazuri ya nchi. Wengi wa viongozi hawakuingia uongozini moja kwa moja, waliionja joto ya jiwe kwanza,kisha wakapanda mjengoni kurekebisha afya. Kwa hiyo lengo kuu la wataka uongozi wengi serikalini sio kwa ajili ya kuwawakilisha na kuwatetea wananchi bali ni kwa manufaa yao,kuzidi kujilimbikizia, na ndio maana wengi hutafuta uongozi serikalini kwa visingizio(kama vya kupambana na ufisadi,rushwa na umasikini) na ndio maana wengi wa wanaotafuta nafasi hutumia zaidi matatizo ya wananchi ambayo inaonekana ndio njia rahisi kabisa ya kupata kura nyingi! Eeeeh,"njoo nikueleze namna fedha za serikali zilivyoliwa", njoo "utambue mbao za shule namna zilivyoibiwa kinyemela na viongozi wa chama tawala"

Tazama namna vyama vinavyogombania "kauli mbiu" ya uchaguzi.Ni wazi kabisa watu hukaa na kufikiri kwa muda mrefu maneno matamu yasiyotekelezeka lengo likiwa ni kuhadaa watu tu.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

hapo ndo shida inapokuja nani amfunge paka kengele

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Najihisi kama nimeingia katika darasa la "Logic". Tukifuata ile kanuni kwamba hasi mbili zikizidishwa eti huzaa chanya pengine hasi (rushwa) mara hasi (rushwa) = chanya (si rushwa).

Tatizo ni kwamba hiyo rushwa inayotolewa wakati mtu anagombea huku akiahidi kupambana na rushwa inabidi irudishwe (kumbuka - there is no free lunch) na mgombea huyu akishinda basi naye inabidi ale rushwa kubwa zaidi ili, mbali na mambo mengine, alipie ile rushwa ya mwanzo. Na hivyo mzunguko usio na fundo wa rushwa unaendelea...

Anonymous said...

Ukweli ni kwamba rushwa kwetu ni kama kansa ambayo haiondoki. Toka ngazi zote za taifa rushwa ni kawaida tu. Unajua sasa watu wanatoa rushwa wakati mwingine hawajui kana kwmba wanatoa rushwa. Kukomesha rushwa itabidi karibu turudi siku za mwalimu wakati waTanzania wote tulijifunza uzalendo, lakini kwa Tanzania ya sasa bila pesa hupati kitu. Nani Mtanzania wa kweli anaweza kusema ajawi toa rushwa!?? Au katumia jina la ukubwa kwenda mbele?!! Au ubabe fulani kupata anacho hitaji? Tanzania ni kama Afrika nzima tunasafari ndefu tunaitaji mabadiliko ya kweli kwa maendeleo ya wengi na sio wachache.