Sunday, May 2, 2010

Kwaheri ya Christiane Amanpour

Christiane Amanpour ni kati ya waandishi makini wa nje ya Afrika ambao wamekuwa CHACHU ya habari maishani mwangu. Nimekuwa nikimfuatilia saaana na kwa muda mrefu na UJASIRI WAKE (hasa wa kuripoti toka maeneo ya vita) ulinifanya nigande kuiangalia CNN kila wakati nikitaraji kumuona akifanya kazi. Na sasa ameondoka CNN baada ya kuwa nao kwa miaka 27.
Kuna waliosema watam-miss lakini nadhani mimi si mmoja wao. Nitaendelea kumuangalia huko ABC alikohamia na kwa hakika ataendelea kutuletea habari kamili na sahihi kama alivyofanya akiwa CNN
Mtazame katika kipindi chake cha mwisho alipoaga

3 comments:

Faith S Hilary said...

Oh she is leaving CNN? I didn't know...well now I know lol! I wouldn't know either because I don't watch CNN regularly and that doesn't mean I don't watch news channels maana nakujua wewe lazima ungesema kitu lol! Somebody in the UK is more likely to watch BBC or Sky News so yh...anyway mmh...she should be alright, she had a great time at CNN and I think she's gonna be alright at ABC :-)...but I miss Tumi Makgabo.ok outta topic...never mind

Mzee wa Changamoto said...

Mmhhhhh!!
Ninapojipanga kujibu nami natoka "outta topic". Lol
Najua uko allergic na news Da Mdogo wala usijali. Najua hilo. Unaangalia "fab lanes", "... next top model", MTV and kazalikaz nyingine.
Anyway.
SERIKALI YA MTU KICHWA CHAKE. NAWE WAIONGOZA KIVYAKO
Hahahahaaaaaaaaaaaaaaa
Much Luv Sis.

Halil Mnzava said...

Huyu mama kwa kweli wengi watamkosa,ni jasiri sana.baadhi ya habari iliyonivutie ni pale alioenda kule Korea ya wazee wa Nuklia na kuhoji wababe wa kule.
Ila maisha yataendelea.