Tuesday, May 25, 2010

SIKU YAKO....Siku maalum Da Koero

Sijui ni lipi naweza kusema kueleza faraja niliyonayo kwa kufahamiana nawe. Najivunia mengi toka kwako. Kuanzia ukweli wa uwezo wako wa kuandika, kukosoa, kuchanganua na hata kushauri na kushaurika. Pengine niseme sifa ama umahiri wa KUSIKILIZA mbao hukufanya uwe na suluhisho ama kuwa na swali ama kupata suluhisho ama jibu la kitu.
Kwa muda mfupi tuliofahamiana na kuwasiliana nimejifunza mengi kuhusu na kutoka kwako.
Na hili lanifanya niwaze namna ambavyo wazazi wako Baba na Mama na ndugu zako, waliokuwa wafanyakazi wako, walio wanajumuiya wenzako na jamii nzima 9kama hii ya blog inavyojivunia uwepo wako
UWEPO WAKO NI BARAKA KWA WENGI WENYE MTAZAMO MPYA
Katika siku hii maalum kwako, nakutakia kila lililo jema katika miaka ijayo, nakupenda, nakuheshimu na nakuombea mafanikio.
Ni siku yako.... Siku maalum kwako Da Koero
Kwa kuwa najua kati ya nyimbo zoooote ulim-feel Nasio Fontaine, naomba nikuache na SALA hii toka kwake akimuomba MUNGU amuongoze katika maisha. Nami naomba milima na mabonde iliyo maishani mwetu uikabili kwa imani na naamini kwa msaada wa umwaminiye, UTAVUKA

Lakini pale palipo na VILIO, kumbuka kuwa ni Mungu pekee atufutaye / kuosha machozi. Sikiliza WASH AWAY TEARS yake Gramps wa Morgan Heritage

Happy BirthDATE Sis

10 comments:

Fadhy Mtanga said...

Happy birthday bibie Koero. Uwe na maisha marefu.

Mija Shija Sayi said...

Furahia siku yako Da'Koero. Mungu akulinde na kukupa nguvu ya kukabiliana na majukumu yanayoongezeka kila umri unapopanda. Hongera sana.

Yasinta Ngonyani said...

Hongera kwa siku ya kuzaliwa Da´mdogo Koero. Nakitakia mafanikio mema kwa kila utendalo.

Unknown said...

Nawashukuru kwa kumtakia mwanangu siku ya kuzaliwa.
Kwa kuwa amezaliwa leo kaniomba niwape salaam zake.

Mama Koero

Anonymous said...

Hongera sana kwa kuadhimisha kumbukumbu ya siku yako ya kuzaliwa Koero. Nakutakia mema mengi katika maisha yako.

mumyhery said...

Happy Birthday Koero nakutakia maisha marefu yenye furaha na afya tele

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Hongera daKoero

Simon Kitururu said...

Happy Birthdate Koero!

Anonymous said...

Binadamu kwa kujikomba duh!

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahaaaaaaaaaaaa.
Karibu saana Anon.
Nashukuru kuwa umesoma na kugundua kuwa kuna KUJIKOMBA humu.
Kwa lolote umaanishalo, NAKUSHUKURU.
Blessings