Wednesday, May 26, 2010

THAMINISHA........Da Subi wa Nukta 77

Kuna wakati ambao unakosa la kusema kuhusu mtu ama kitu. Na hiyo ni kutokana na ushiriki wa mtu ama watu kwenye jambo ama mambo fulani.
NAOMBA katika kipengele hiki kipya NIMTHAMINISHE DADA SUBI.
Mmoja kati ya wale ambao wamejitolea saaana kujenga, kuboresha na kuhakikisha blog na tovuti zaendana na wakati. Amekuwa "mtoa tip" katika masuala mazima ya teknohama katika suala la NINI CHA KUFANYA na pia NINI CHA KUEPUKA.
Kila siku nimekuwa nikimwambia Dadangu huyu mpenzi kuwa NIMECHOKA KUELEZA NINAVYOTHAMINI MCHANGO WAKE na ninaloomba ni kumthaminisha hapa Mbunifu Da Subi
ASANTE SAANA DADA SUBI NA NAPENDA UJUE KUWA LICHA YA UFUPI AMA UCHACHE WA MANENO HAUMAANISHI KUTOTHAMINIKA KWA UFANYAYO.
Najua huoni tabasamu wala ridhiko nyusoni mwetu kwa yale uyafanyayo. Na pengine ni kwa kuwa watufunza ama kutushirikisha mambo kwa mafungu ama kwa uchache huoni kama ni mengi utupayo. Lakini kwangu binafsi na wale nishirikianao yale uliyonifunza, UFANYAYO NI MUHIMU NA MAKUBWA SAANA KWETU.
Na ndio maana naona ni vema kuweka thamani yako nikianimi kuwa WASOMAO HAPA, NAO WATATHAMINISHA UWAFANYIALO
Wimbo huu hapa chini ni maalum kwa ajili ya yale mema ututendeayo. Kwangu mimi, YOU ARE A HERO.

Do you see the smiles on their faces
after you have done what you do best
do you see satisfaction on their faces
after you have blessed themw ith your gift
you don't think iit's much
but to them it means the world
they wake up in the morning and wish you were there
don't have to lie to gain their trust
you have never won a Nobel prize
they have never seen you on the TV
your little contribution makes their lives a little bit better every day

chorus
You're a hero x8

big it up, big it up for the fireman
big it up, big it upfor the street cleaners
big it up for the man aNd the woman
who take care of abandonded children
big it up, big it up for the grandmothers
who are left to take care of the children
big it up, big it up Wo!!


**THAMINISHA ni kipengele kinachounganisha makala ama matoleo mbalimbali ya watu mbalimbali wanaojitolea kuboresha maisha ya wengine na hata wale wanaoona vema kuthaminisha yale waliyotendewa na wengine. Kwa matoleo zaidi BOFYA HAPA**

15 comments:

Fadhy Mtanga said...

Kaka Mubelwa nashukuru sana umesema hilo. Dada Subi ni mtu wa aina ya kipekee. Anautumia muda wake kwa ajili ya watu. Hakika uwepo wake duniani ni jambo tunalojivunia. Nami nawiwa kushika peni na karatasi kumwandikia mistari pale bustanini kwangu.

Jana tu usiku nimejifunza kwake namna ya kuimport blog yangu katika facebook. Kwa kufuata maelekezo yake nikafanikiwa. Sasa kila nikiandika post itakwenda kule moja kwa moja.

Ubarikiwe sana mwanadada weye.

Ubarikiwe nawe Mube kwa kulisemea hili.

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Mtanga. Hiyo niliiona nami nikainyonya.
Ila SUBI kanichosha kumsema. Kweli kanichosha. Ni kama vile nahitaji kumshukuru kabla sijaingia kwenye page zake kumsoma maana kila uchao aja na lililo jipya.
Akiwa na jambo analofahamu ni faida kwetu sisi tunaopenda kuchati bila kupenda kuboresha mifumo yetu anatujuvya.
Tunapoenzi watu na ninapoendelea kuwaza kuhusu Pata Ujuzi Gawia Umma (PUGU) AWARDS, naendelea kuthaminisha waliosaidia. Kama nawe unao ama unaye aliyegusa maisha yako vema, nipatie TUM/WATHAMINISHE

Mija Shija Sayi said...

Hii safi kwa kweli, Yaani huyu Subi huyu wee acha tu. Nimeupenda sana huo mchoro wake ulioutundika.
Kwa kweli sina la kusema juu yake umemaliza yote Mzee wa Changamoto.

Kila la heri Subi wetu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mwanamke wa thamani huyu

EDNA said...

Mimi nakosa hata maneno ya kusema kwa huyo MKOMBOZI WETU,maana nikisema ASANTE naona bado haitoshi
.Labda niseme Mungu akubariki kwa moyo wako wa kupenda kusaidia wengine.

Simon Kitururu said...

Naungana nanyi katika hili! Subi bomba!

Hivi Da Subi unajua na kupika?:-)

Yasinta Ngonyani said...

Nakubaliana na wengine wote waliotangulia ni jambo la kushukuru sana kuwa na da Subi ni kweli mwanamke shujaa. Binafi ninamtumia sana mwanadada huyu. Subi bila wewe sijui tungefanya nini? Wewe ni SHUJAA WETU, UBARIKIWE SANA. NA PIA mUBELWA NAWE UBARIKIWA KWA KULIONA HILI NA KULIANDIKA HAPA

Mija Shija Sayi said...

Kitururu naona kabisa unakoanza kuelekea....Natania.

Simon Kitururu said...

@Da Mija: Nimesikia Da Subi Mchaga kwa hiyo kimila mie kama Mpare naruhusiwa kumtania.

Kwani zaidi ya Mtori, kuchemsha maji ya chai na Mbege unafikiri kunakingine Wachaga wanajua kupika?

Mzee wa Changamoto said...

Kweli namna uonavyo tatizo ndilo tatizo.
Mie nilidhani kaka Kitururu anamaanisha kuwa Da Subi anatumia muda mwingi kwenye kompyuta kwa hiyo hawezi hata kujifunza kupika. Hahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Asanteni nyooote nyooote wapendwa kwa kuona mchango wa Dadetu huyu.
Asanteni kwa kumTHAMINISHA.
Blessings

Unknown said...

Nakubaliana nanyi nyooote. Athaminiwe kwa mchango wake kwetu. Ahsante da Subi..

Subi Nukta said...

Niksema nitoe shukrani kwenu ndugu zangu, ni uongo na si kazi.

Machozi yamenitoka, nimetafakari kwa muda mrefu sana, kama mtu atakuwa ametembelea tovuti yangu leo atagundua kuwa kwa takriban saa sita na dakika kadhaa hivi sijabandika jambo lolote jipya, nimetafakari nimetokwa machozi na nimeishia kuala tu kwani sifahamu ni kwa kiasi gani nimeweza kuwagusa baadhi yenu kwa kile ninachokifanya.

Kazi hii ni rahisi na ngumu kwangu. Mtakubaliana nami wanablogu wenzangu kuwa kuanzisha blogu si jambo gumu, bali ugumu upo katika kuidumisha blogu na kuiendeleza hasa katika kupokea na kukubali maneno toka kwa wasomaji na watembeleaji wa blogu yako, aghalabu, utajikuta unashindwa kufikia lengo kwa kudhani kuwa ulichokuwa ukikifanya ni sahahi na badala yake kikawa si sahihi kutokana na mtizamo wa msomaji (the way you see the problem is the problem) na hivyo ukajikuta unasubiri na kutafakari kidogo ikiwa umeshika mwelekeo sahihi ama wahitaji kujirekebisha ili uendane kiusahihi na jamii - changamoto.

Niliposoma habari hii, niliposoma maoni ya majirani, marafiki, ndugu, jamaa, kaka na dada zangu (kaka Fadhili, kaka Mubelwa, dada Mija, kaka Kamala, dada Edna, kaka Simon pamoja an dada Yasinta) nimepatwa na hali ya kusisimka. Ni msisimko ambao kwa hakika hauandikiki wala kuelezeka, ni hali ya kipekee.

Nimepata changamoto mpya, kuwa ijapokuwa ninafanya kwa kupenda, wapo wanaoguswa na kuyaona haya.

Niliwahi kuwaambia marafiki zangu ambao tunawasiliana kwa njia ya barua pepe kuwa, mara nyingi (karibu zote) huwa sijui namna pekee ya kushukuru ninaposifiwa, huwa napatwa na soni na kutamani upenyo utokee nijifiche, ni kwa kuwa sikuzoea na kwa vile ninachokifanya ninafurahi pale mwingine anapojifunza na kufaidika, basi huwa nadhani inatosha kusema 'Asante' nami hupenda kutoa shukrani kwa yule aliyependa kusoma na kujifunza kile nilichokisema au kukifanya au kukielekeza. Ndiposa nasema, 'iko raha na faida kuu katika kutoa kuliko kupokea'.

Ninyi nyote mlioguswa kwa namna yoyote ile, nakuombeeni muendelee kujawa uwezo, hekima na maarifa katika kuenenda katika ulimwengu huu na maisha yenu yawe yenye heri, baraka na mafanikio tele, ikiwa si kwenu binafsi basi kwa vizazi vyenu vijavyo na wale wote wanaokuzungukeni.

Kazi yenu si bure, changamoto yenu yatusababisha sote tusonge mbele zaidi na zaidi.

Napenda kukosolewa nanyi kadiri iwezekanavyo ili nisilewe 'kujidai najua' na niweze kukubali tafauti zetu na kuona wazo la kila mmoja kuwa la thamani.

Historia zetu zitabaki kusomwa na vizazi vijavyo. Hayapotei bure maneno yenu.

Shukrani za dhati kwenu wana blogu na wasomaji wenzangu!

Swali: Sasa kwa nini ulilia?
Jibu: Hisia. Kwa walio wanawake wataelewa zaidi, tunatawaliwa na vichocheo vya hisia ambavyo husukuma msisimko na hata machozi kutoka. Sikupanga.

Au?
Pengine ni ushamba tu.
Mmnisamehe.

SN said...
This comment has been removed by the author.
SN said...

Hii alma-nusura inipite!

Mi' nimekutana na da' Subi kwenye mtandao kama miezi miwili tu iloyopita. Lakini baada ya kubadilishana mawazo kupitia barua pepe (wakati tunaanzisha www.vijanafm.com), nilidhani kama tulikuwa tunafahamiana kwa muda mrefu sana! Nadhani hiyo ilisababishwa na ukarimu wake.

Kwahiyo Mzee wa Changamoto, shukrani kwa kutupa nafasi ya kumueleza na kumshukuru kwa mchango wake. Anastahili hizi sifa; wale wa vijiweni tunasema mtu kama huyu inabidi apewe sifa za marehemu. Namaanisha hivi, anapaswa kuambiwa na kusikia shukrani zetu kabla hajazeeka au mauti kumfika (ni figurative speech tu). Ili ajue kuwa anachopigania hakitapotea hivi hivi tu.

Mi' toka aniambie kuwa wavuti.com inaendeshwa na yeye mwenyewe sijaamini mpaka leo. Juzi nilikuwa kwenye baiskeli yangu nakuja mzigoni nikawa nafikiria, hivi da' Subi akienda kuwaona wazee kijijini, yaani wavuti itaenda likizo? Jambo hili lilinitisha kwa kiasi fulani! Mi' nasoma sasa hivi, lakini nikifanikiwa kwenye maisha kwenye hii miaka mitano ijayo, nitajaribu kumsaidia da' Subi ili wavuti iwe kama kijikampuni hivi. Nitafanyaje, sijui kusema ukweli sasa hivi.

Kwa kifupi, shukrani sana da' Subi na Mungu akuzidishie nguvu, ujuzi, muda na kila kitu unachohitaji.

Sasa, mimi nina damu ya Kipare na itakuwa sio vema nikimaliza hivi hivi tu :).

Streit tu dhe pointi. Kuna msela hapa anauliza vipi, watu wameshachukua chao au bado unapatikana? LOL

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti said...

Yes! Huyu ni mwanamke wa SHOKA!