Thursday, May 6, 2010

Them, I & Them......TRINITY....Lucky Dube

Eneo la tukio "likisafishwa" kwa gari-shukiwa likiondolewa eneo la tukio baada ya kuteguliwa bomu lililokuwa ndani mwake
Photo: Giancarli for NYDailyNews.com
Mwishoni mwa juma lililopita kulitokea jaribio la kulipua "milipuko" ambayo kwa hakika ingeathiri maisha ya watu wengi (hata kwa kuwashitua na kuwaogofya kama isingeua ama kujeruhi) na mpaka sasa mshukiwa mkuu amekamatwa kuhusiana na jaribio hilo. Hili si jaribio la kwanza kushindwa kufanikiwa (kwa wategaji) tangu kutokea milipuko ya Septemba 11, 2001.
Lakini hapa swali laja kuwa kwanini bado twaendelea kuweka maisha ya wasio na hatia katika hatari? Ni kwanini licha ya kupigana nao huko wanakoaminika kuwepo, kwanini wanaendelea "kuchipuka" kila mahala ulimwenguni? Luciano aliwahi sema kuwa "they kill trhe wicked but still more rise. Without proper justice we shouldn't be suprised". Na hapo tunaendelea kujiuliza kama hata wao kujaribu kuua wananchi na mataifa kujaribu kuwaua ni sehemu ya suluhisho. Ni hapa ninapomkumbuka Nasio aliyesema kuwa "War is not the solution. Never was, never will it be so". Na hapa ni kwa lolote lile.
Ila ninalohisi kuwa la kipekee katika hili la sasa ni kama hawa wahusika wa pande mbili wanajua wanachopigania. Kuna uwezekano kuwa kama kungetokea kukawa na kuelewana na kueleweshana juu ya u-mimi na u-wao, mambo mengi yangemalizika kwa mmwagiko mdoogo saana wa damu. Lakini nahisi SI MAGAIDI WALA MATAIFA YAPAMBANAYO NAO WANAOJUA UPANDE WA PILI UKO VIPI, UNAHITAJI NINI, UHESHIMIKE VIPI, WACHUKIZWA NA NINI NA WAWEZA KUSHIRIKIANA NAO VIPI KUILETA AMANI AMBAYO WOTE WANATAKA KUISAKA KWA NCHA YA UPANGA.
Ni fikra hizi zinazonirejesha kwenye wimbo huu wake LUCKY DUBE uitwao TRINITY ambao unazungumzia mambo yafananayo na haya.
Japo aliimba wakati wa harakati za kusaka amani kutoka kwa ubaguzi na ukoloni, lakini MAUDHUI NA NJIA ALIYOSHAURI KAMA SULUHISHO IKINGALI NA UWEZO WA KUTATUA HATA HILI LA SASA.
Ukimsikiliza anapoanza wimbo wake anaanza kwa kusema "I'm sleeping with my one eye open 'cause I think you gonna come for me. You're sleeping with your gun in hand, you think I'm gonna make my move..." Na huu ndio UKWELI wa maisha yaliyopo katika pande hizi mbili za ulimwengu niuzungumziao ambao ni wa mataifa yanayopambana na kile waitacho ugaidi na hao magaidi. Haya mataifa makubwa hayaishi kuchunga kila upenyo wa mawasiliano wakihisi magaidi watawaingilia, ilhali hao waitwao magaidi wanahaha kila walipo wakihisi watashushiwa shambulizi. Lakini kinachosikitisha ni kuwa unaposikia habari za upande wa pili, zinakuwa zimepotoshwa kiasi ama kuongezewa jambo (kwa makusudi ama bahati mbaya) kwa nia ya kuungwa mkono. Na kwa bahati mbaya kuna ambao wanakwenda kupigana "kwa sababu hizo wanazoambiwa ambazo wakati mwingine si sahihi". Sasa ni kwanini kusiwe na uwezekano wa kuepusha haya kwa kuweka ukweli bayana kuhusu kila upande (hasa kwa kuwa kuna ambao tumeshaona uongo ulivyotuingiza matatizono) na kuepusha yale yanayotugombanisha yasiyo ya kweli na pengine kuungana kama alivyosema "now that we know where we went wrong, Let's unite ".
Katika wimbo huu, yanaongelewa yaleyale yaliyohusika katika kugombea AMANI NA USAWA kwa njia ya kuelewana.
Msikilize LUCKY DUBE huku ukimsoma katika mafunzo mazuuuri saana akisema TRINITY

I'm sleeping with my one eye open
'Cause I think you gonna come for me
You're sleeping with your gun in hand
'Cause you think I'm gonna make my move

I've been chasing white people all my life
You've been chasing black people all your life
Now that we know where we went wrong,

it's time some truth came out here

You going to educate me about white people
I will educate you about Black people

and we'll unite
That's why they call me trinity
And my game is unity

Chorus
Trinity, unity

My brothers have been chasing racists all the time
Your brothers have been chasing freedom fighters all the time
But at the end of the day
We didn't know much about each other yeah

When you saw a black man you saw a criminal,
When I saw a white man I saw an oppressor
But now that we know where we went wrong
Let's unite

You will educate me about white people
I will educated you about black people

That is why they call my trinity
Cause my game is unity

Chorus till fade...


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

1 comment:

Koero Mkundi said...

Kila umwandikapo Lucky Dube huwa nafurahi kusoma habari zake, kama walivyo baadhi ya wanamuziki huu wa Reggae, huyu naye ni miongoni mwa wanamuziki wa reggae ambao wameacha mchango mkubwa sana katika kuzungumzia maisha ya huyu kiumbe mwanaadamu na vioja vyake.....UNAFIKI. Unafiki ni tatizo kubwa sana ambalo limeifikisha dunia hii hapa ilipo...kila nikiwaangalia viongozi wa Afrika wanavyojinyenyekeza kwa wenzetu walioimarika kiuchumi kutokana na rasilimali walizojichotea huku Afrika huwa nashangaa. Kuna wakati Rais wa Gambia Yahya Djameh aliwahi kuwataka warudishe utajiri waliojichotea huku Afrika na kulipa fidia ya ile biashara ya utumwa ambayo ndio chimbuko la umasikini huu tulio nao leo hii. wakati wanawalipa fidia waisraeli naw wajapani kutokana na madhila waliyowasababaishia, lakini wamekataa kabisa kulipa hata robo wa kile walichochukua huku Afrika.

Ni roho mbaya kiasi gani hii?

To my suprise leo wanarudi kuchota tena utajiri wetu kwa kigezo cha uwekezaji na soko huria na viongozi wetu wanasema "Halleluya"

wakati mkutano mkuu wa kiuchumi unafanyika hapa nchini, tunashuhudia mwendelezo ule ule wa kuomba huruma kutoka kwa hawa ma bwana, do you think they care about us? Nooooo....they dont and they can't even think about our welfare.....

We should wake up and say now is enough, walivyochukua vinatosha....waende wakatafute kwingine. lakini wataweza wapi wakati viongozi wetu Afika ni corrupt? All they think is about themselves and their family, wamefikia mahali sasa wanarithishana uongozi wa nchi na watoto zao ili kujihakikishia usalama wao na mali zao walizokwiba.

Juzi hapa nimemsikia Rais Mstaafu wa Nigeria Olusugun Obasanjo akihojiwa na Shaka Sally wa sauti ya Amerika...alikiri wazi kuwa viongozi wengi wa afrika walioondoka madarakani kwa hiyari yao waliishia gerezani akiwepo yeye mwenyewe kutokana na madhambi waliyoyatenda wakati wa tawala zao, ingawa alikanusha yeye kutenda jambo lolote baya, lakini je hawahisi kuwa kuna ukweli juu ya tuhuma hizo. Alinichekesha pale aliposema kuwa siku hizi wanajiita Prisoner President Graduate (PPG) kaama sikosei.....it was like joke, lakini huo ndio ukweli huwezi kufanya madudu ukiwa madarakani halafu watu wakuache hivi hivi, you will pay the price.
Tunasema utavuna kile ulichopanda.....Mbona Mandela hajakamatwa, mbona Rais Masire wa Botswana hajakamatwa, mbona Sam Nujoma hajakamatwa....wapo wengi tu ambao wamefanya mambo mazuri ambapo wananchi wao wanwaenzi mpaka leo. They are not an angel, lakini walijua kuwa wana deni na walitekeleza kile walichoamini kuwa kitakidhi matarajio ya wananchi wao, na hadi ikafika mahali wakasema sasa inatosha tuwaachie wengine waendeleze gurudumu la maendeleo ya nchi zao.