Friday, July 30, 2010

Them, I & Them......HYPOCRITES....Nasio Fontaine

"They will smile in your face, stub you on your back,
They will smile in your face, but they wanna get you off your track.....
Their teeths are whites and smiles are brights, filled with hates and hypocrisy
Hands are stretched ready to recieve, cause they know that you're willing to give...."

Umewadia
Wakati
wa sisi waTanzania kusikiliza. Wakati wa kuongeleshwa na wakati wa kusikilizishwa.
Wakati tutakaoona tabasamu kuubwa na nyingi kuliko wakati wowote
Wakati ambao "tutapendwa" na kutoonewa kinyaa
Wakati ambao hata "waheshimiwa" watakaa nasi na kujifanya wanataka kutusikiliza
Wakati ambao watakaa chini na hata ukikaa kwenye kiti chake atasema "kaa tu maana nimekuja kukusikiliza wewe"
Wakati ambao kweli "mteja ni mfalme" (japo kwa nadharia)
Wakati ambao watacheka nasi, watagongesha viganja na ngumi kusalimiana kwa style yetu,
Wakati ambapo watatuonesha kuwa nao wanatuwaza.
Weeeelllll!!!!!!!!! Tuwe makini kwani huu ni WAKATI WATAKAODHIHIRISHA UNAFIKI ULIOMO NDANI MWAO.
Siku ya leo wala sina mengi msomaji wangu. Naomba umsikilize NASIO FONTAINE na kibao chake Hypocrites anapozungumzia hawa watu watakaokutabasamulia usoni ilhali wanatafuta namna ya kukuondoa katika mfumo wako wa maisha.
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

6 comments:

emu-three said...

Wakati ambao unaweza ukapewa shikamoo hata na mzee aliyekuzid miaka 20 mbele yako!

Simon Kitururu said...

Ijumaa njema Mkuu!

@emu-three: Duh!

Albert Kissima said...

Aliyekuwa anawajibika hatakuja kwa unyenyekevu, kwani wajao kwa staili hii, tayari wanaonyesha wakitafutacho, si viongozi wa uhakika, hawajui na hawatambui kwa muda waliokaa bungeni madhalani, ni kipi walikifanya au ni juhudi gani walizifanya ktk kuleta au kufanikisha maendeleo.

Binafsi nikimwona kiongozi wa aina hii, tunayesalimiana naye kwa kugonga ngumi, nipe tano, aniulizaye shida zangu wakati wa kampeni n.k, huyu automatically hatanifaa.

Kiongozi wa kweli kimsingi hatoi ahadi kabla ya kuelezea mafanikio yake akiwa kiongozi au utendaji wowote wenye tija, ambao hata jamii husika itakubali. Kiongozi wa kweli huja kuomba muda zaidi wa kuongoza kwa kujiamini na kujiamini hutokana na utendaji kazi wake ambao hata jamii inakubali.

Mtu amekaa bungeni miaka mitano, kumi, alafu anakuja hana hata moja la kujivunia, watu wake hawampokei kama shujaa, halafu anatoa ahadi. Huku ni kudanganya kuliko kwa wazi. Mtu huyu ni wazi anautaka uongozi kwa manufaa yake binafsi.

Watanzania, tusishabikie ahadi na sera zilizoandaliwa kwa muda mrefu vitabuni, tuangalie wale waombao kura, wameshatufanyia nini au mchango wao kwa jamii ktk shughuli za kimaendeleo ni upi, tukishajihakikishia hili, ndipo tupate kusikia mikakati yake ya baadae kwani tutakuwa na uhakika na utendaji kazi wake. Tuachane na ushabiki na umaarufu,sisi wapiga kura ndio wenye mustakabali wa taifa letu. Twahitaji kuwa makini. Kipindi hiki sisi ni wafalme, waliokuwa juu, hawangoji tuwafuate, wanashuka pamoja na kuwa huwa hawashuki(wengi wao), wale wanaolazimishwa kushuka, wanakuja kwa unyonge, wanakuja kiupande upande, wanakuja kumuua nyani kwa kutomwangalia usoni, wanakuja kututupia mawe tungali gizani, wanajishusha sasa kucheka nasi, kula nasi, ila daladala hawapandi nasi, maji hawaendi kuteka nasi visimani, hawatibiwi nasi. Tuwagoge watu hawa kama ukoma na tusiwachague, tuwakimbie,wanajulikana. Bora tumpe kura zetu watu ambao ndio kwanza wanausaka uongozi kuliko watu wa aina hii!

nyahbingi worrior. said...

aliye na macho na ayaone,aliye na sikio asikie.

Amani.