Monday, July 19, 2010

Za Kale vs Maisha ya Sasa...TOP QUEEN

Ukianza kutafuta SIFA mbalimbali ambazo anaweza kuwa nazo mtu udhaniaye ndiye chaguo lako, unaweza kushangazwa na kile utakachogundua.
Lakini kawaida ya wengi huwa twasubiri mtu mwingine atuambie sifa ya yule tunayempenda. Ina maana hatuzioni na hata tukiambiwa hatuonekani kuzithamini. Na ndio maana hata mwenye mke ama mwenye mwenye busara na upendo wa dhati (hasa kwa mazingira ya nyumbani) anaweza kuamka na kuondoka na kurejea na kuelekea kulala bila hata kumwambia ama kudhihirisha BARAKA aliyonayo kuwa na mume ama mke mwenye busara na upendo.
Kama walivyoimba Vijana Jazz kwenye wimbo wao, wamesema "hapa ulimwenguni kila binadamu Mungu kamuumba kwa sifa zake". Na huu ndio ukweli wa mambo. Lakini pia kulingana na maisha yetu, na pengine mahitaji ya nyoyo zetu, tunajikuta tuna mahitaji tofauti. Na ni kwa wale wajao na suluhisho la mahitaji yetu wanaokuwa na nafasi ya kipekee kwetu. Vijana Jazz kwenye wimbo Top Queen wamemueleza Regina (ambaye ndiye aliyeimbwa kama Top Queen) kuwa uzuri wake "..tabia njema na busara zake......zimefanya wazazi waheshimu maamuzi yake".
Na hili la kuwa na maamuzi ya busara linazidi kujidhihirisha pale ambapo aliamua kuwaweka kando wale waliokuja na magari ya fahari, pesa nyingi, waliokuja na nguo za kuazima na wenye kujionesha na kuishia kuolewa na MFUGA BATA ambaye hali yake kimaisha (naamini kulingana na wale waliomtangulia "kurusha karata" imetajwa kama HOHEHAHE.
Yes!!! Ni mimi na TOP QUEEN wangu.
Na hawa wenye fikra na mitazamo hii myema wako wengi ulimwengu wa sasa. Well!!! Nami ni mmoja wa walionufaika na TOP QUEEN wangu. Busara nyingi zilizotajwa kuwemo ama kuwa nazo Top Queen aliyeimbwa na Vijana Jazz amekuwa nazo. Na hii ndiyo sababu inayonifanya niamini NYIMBO HIZI ZIKINGALI NA MAANA MPAKA LEO.
Sikiliza wimbo huu Top Queen toka kwao Vijana Jazz Band uburudike na kuelimika.

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

nanukuu "hapa ulimwenguni kila binadamu Mungu kamuumba kwa sifa zake".mwisho wa kunukuu. Namshukuru Mungu kwa kazi hiyo fikiria kama angetuumba wote na sifa sawasawa pia tabia sawasawa nadhani dunia hii isingkuwa salama. Kaka Mubelwa hapa na Queen wako mmependeza.

chib said...

Nimesoma post yako nimeipenda, naomba niweke na utani.... si wajua tena. Kwa nni umemuweka Queen wako na nyimbo zilipendwa? Usijali, mie nimetizama upande huo. Yaani binadamu hatufikirii kitu kimoja kwa wakati mmoja, ni hayo tu Mkuu, :-)

Mzee wa Changamoto said...

Asante saana Dada Yasinta kwa kuendelea "kuchungulia" hili na lile.
Kaka Chib, nimemuweka Top Queen wangu (na mimi mwenyewe) kwa kuwa, kama ambavyo wimbo huo ulipendwa, unapendwa na utaendelea kupendwa, vivyo hivyo nasi tulipendana, tunapendana na tutaendelea kupendana.
Ati umesema "binadamu hatufikirii kitu kimoja kwa wakati mmoja". Ni kweli kabisa kwani wakati wewe wafikiria utani, mie naona jambo nichunguliapo utanio "kwa jicho la ndani"
Hahahahahaaaaaaaaa
Blessings